RAIS DKT SAMIA APOKELEWA RASMI NCHINI INDONESIA

January 24, 2024

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mhe. Joko Widodo wakiangalia Vikosi vya Gwaride la Heshima vikipita mbele wakati wa Mapokezi Rasmi yaliyofanyika kwenye viwanja vya Bogor Presidential Palace tarehe 25 Januari,2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mhe. Joko Widodo wakati wakielekea kwenye mkutano katika Ofisi za Rais huyo Bogor Presidential Palace tarehe 25 Januari,2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la heshima wakati wa mapokezi yake Rasmi katika viwanja vya Bogor Presidential Palace tarehe 25 Januari,2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la heshima wakati wa mapokezi yake Rasmi katika viwanja vya Bogor Presidential Palace tarehe 25 Januari,2024.


RAIS DKT SAMIA AKINAWISHWA MIKONO NA RAIS WA INDONESIA MHE JOKO WIDODO MARA BAADA YA KUPANDA MTI KWENYE MAKAZI YAKE

January 24, 2024

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akinawishwa mikono na Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mhe. Joko Widodo mara baada ya kupanda mti wa kumbukumbu katika viwanja vya Makazi ya Rais huyo Bogor Presidential Palace tarehe 25 Januari,2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akinawishwa mikono na Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mhe. Joko Widodo mara baada ya kupanda mti wa kumbukumbu katika viwanja vya Makazi ya Rais huyo Bogor Presidential Palace tarehe 25 Januari,2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akinawishwa mikono na Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mhe. Joko Widodo mara baada ya kupanda mti wa kumbukumbu katika viwanja vya Makazi ya Rais huyo Bogor Presidential Palace tarehe 25 Januari,2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akinawishwa mikono na Rais wa Jamhuri ya Indonesia Mhe. Joko Widodo mara baada ya kupanda mti wa kumbukumbu katika viwanja vya Makazi ya Rais huyo Bogor Presidential Palace tarehe 25 Januari,2024.

RC SENDIGA AKABIDHI PIKIPIKI 42 KWA JUMUIYA ZA MAJI RUWASA

January 24, 2024

 

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga amekabidhi pikipiki 42 kwa jumuiya za watoa huduma za maji katika wilaya zote za Mkoa wa Manyara ili kurahisisha utendaji kazi kwa watumiaji hao.

Pikipiki hizo zimetolewa na Wakala wa Maji Safi na Salama na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoa wa Manyara.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki hizo Mhe. Sendiga amesema ni vyema kwa watumishi hao kuzitunza kwani ni mali ya serikali.

"Niwasihi tukahakikishe pikipiki hizi zinaenda kutumika kama ilivyokusudiwa na kuhakikisha skimu za maji zinakuwa endelevu na Wananchi wanapata huduma ya maji muda wote kwani ni haki yao ya msingi", amesema Mhe. Sendiga.

Aidha, Mhe. Sendiga amewataka wakuu wa taasisi mbali mbali kukusanya fedha za Umma kwa uadilifu kwa kuzingatia taratibu, kanuni na sheria zilizopo na kusitokee chombo chochote kukiuka kwa sababu yoyote huku akiwasihi wakuu wa wilaya wote kuendelea kusimamia vyema uhai wa miradi iliyojengwa.

"Serikali imewekeza fedha nyingi sana kujenga miradi hii ya maji, fedha hizi ni zenu kupitia kodi na tozo mbalimbali, tunajukumu kubwa la kuitunza miradi ili kuhakikisha kusudi la Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan la kumtua mama ndoo kichwani linafikiwa", amesema Mhe. Sendiga.

Akitoa shukrani zake kwa RUWASA Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange amesema kuwa atasimamia na kufuatilia kwa Ukaribu kama watumisji waliokabidhiwa pikipiki hizo wanazifanyi kazi kama ambavyo kusudio la Serikali ilivyowaagiza.
Kwa upande wake Meneja wa RUWASA mkoa wa Manyara Injinia Wolter Kilter amesema lengo la kuwapa pikipiki hizo kwa watumiaji hao ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma za maji kwa uharaha zaidi.

Amesema kuwa Mkoa wa Manyara unajumla ya Vyombo hivi 88 vinavyosimamia Skimu za maji 346 na kuhudumia wananchi 1,268,239 ambapo mpaka Septemba 30, 2023 zilikusanywa jumla ya Tshs 2,113,232,529", amesema Injinia Kilter.

Ameongeza kuwa RUWASA inaendelea kuvipatia mafunzo jumuiya za watumiaji Maji kama jinsi ya kuandaa mpango wa biashara na ufungaji wa hesabu, vyombo 32 vimeshapatiwa mafunzo hayo mpaka Julai 23, 2023.
-- Cathbert Angelo Kajuna, Founder and Mananging Director Kajunason Blog, P.O Box 6482, Dar es Salaam. Tel: +255 787 999 774 Alt: +255 735 997 777 www.kajunason.blogspot.com "Everything is Possible Through Peace & Stability''
WATANZANIA WAPEWE KIPAUMBELE MRADI WA EACOP-DKT. BITEKO

WATANZANIA WAPEWE KIPAUMBELE MRADI WA EACOP-DKT. BITEKO

January 24, 2024

 

*Ataka uwiano wa malipo kati ya Watalaam Wazawa na kutoka nje*

…………………….. 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Watendaji katika kampuni inayotekeleza Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kuhakikisha kuwa, Watanzania wanapewa kipaumbele katika hatua zote za utekelezaji wa mradi ikiwemo ajira na utoaji huduma kama vile ulinzi, chakula, usafiri, bidhaa za ujenzi, huduma za mawasiliano na huduma nyinginezo ikiwa ni utekelezaji wa Sera ya Nishati ya mwaka 2015.

Dkt. Biteko amesema hayo mara baada ya kufanya ziara katika kata ya Chongoleani jijini Tanga na kujionea kazi mbalimbali za ujenzi wa miundombinu zikiendelea katika eneo hilo ambalo mafuta kutoka nchini Uganda yatakuwa yakipokelewa na kuhifadhiwa kabla ya kusafirishwa. Katika ziara hiyo aliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Bendera na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba.

“Serikali inataka kuona watanzania wengi zaidi wanapewa kipaumbele cha ajira katika hatua zote za mradi na hii inajumuisha kampuni za Watanzania zinazotoa huduma mbalimbali, kwa kada ambazo ujuzi wake unapatikana ndani ya nchi, watanzania wapatiwe nafasi na kwa kada ambazo zinahitaji wataalam wa nje lazima kuwe uwiano wa malipo kati ya Wazawa na wageni.” Amesisitiza Dkt. Biteko

Kuhusu ujuzi unaotolewa na kampuni ya EACOP kwa watanzania wakiwemo kutoka vijiji vinavyozunguka mradi, Dkt. Biteko ameitaka kampuni hiyo kuhakikisha inatoa ujuzi ambao ni endelevu utakaowawezesha kuendelea na kazi hata pale mradi utakapokamilika akitolea mfano kuwawezesha kupata mashine za uchomeleaji ambapo ametaka Halmashauri zishirikiane na kampuni ili kutekeleza suala hilo.

Akizungumzia utekelezaji mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi litakalokuwa na urefu wa kilomita 1,443 amesema kuwa, unaendelea vizuiri na sasa umefikia asilimia 32 na mabomba yatakayopitisha mafuta yanaendelea kuingia nchini kwa ajili ya kuwekewa mifumo ya upashaji joto na plastiki itakayozuia upotevu wa joto kwenye mabomba hayo katika kiwanda kilichopo Sojo wilayani Nzega.

Ameeleza kuwa, ulipaji fidia kwa wananchi wanaopisha mkuza wa bomba umekamilika, kambi za ujenzi zimekamilika na kazi mbalimbali zinazoendelea ni pamoja na ujenzi wa gati katika kata ya Chongoleani mkoani Tanga ambapo meli zitakuwa zikipakia mafuta tayari kwa kusafirishwa nje ya nchi.

Amesema kuwa, Serikali inayo kiu ya kuwaletea Maendeleo Watanzania na ikiamua kutekeleza jambo inafanya bila ulegevu wowote, akieleza kuwa, Tanzania imeshatoa zaidi Dola za Marekani milioni 240 EACOP kama mwanahisa ambaye ana asilimia 15 kwenye mradi huo na kwamba fedha hizo zimekuwa zikitolewa kwa wakati.

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amekagua eneo mafuta yanapopokelewa katika bandari ya Tanga na kukagua mita za kupimia mafuta (flow meter) ambapo aliridhika kuwa mita hizo zinafanya kazi vizuri na hivyo kuleta ufanisi katika shughuli za upakuaji na upakiaji mafuta katika Bandari ya Tanga.

Amesema kuwa, baada ya kurekebishwa kwa kanuni za mafuta, Serikali imeshaagiza mafuta yote ya Ukanda wa Kaskazini yachukuliwe jijini Tanga pamoja na yale yanayoenda nchi za nje kama vile Kenya na mafuta ya Ukanda wa Kusini yachukuliwe bandari ya Mtwara.

Kutokana na hilo, ameziagiza Taasisi zinazosimamia mafuta ikiwemo EWURA, PBPA, TBS na TPA, kufanyia kazi haraka agizo hilo la Serikali kwani kanuni tayari zilishasainiwa kwa ajili utekelezaji wa suala hilo ili kuwawezesha watanzania kupata mafuta kwa bei nafuu.

Akiwa jijini Tanga, Dkt. Biteko pia ametembelea eneo la hifadhi ya mafuta ya kampuni ya GBP ambayo inahifadhi mafuta kwa ajili ya matumizi ya ndani na nje ya nchi na kuwaeleza wawekezaji hao kuwa, Serikali inathamini uwekezaji huo na ipo tayari kuwaunga mkono katika mipango yao ya uwekezaji.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Waziri Bendera, amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka nguvu kubwa kwenye utekelezaji wa mradi huo, akieleza kuwa mradi wa EACOP utakuza pia mapato ya Mkoa wa Tanga pamoja kipato cha mtu mmoja mmoja.


MABINGWA WA KOMBE LA MAPINDUZI CUP 2024/2025 TIMU YA MLANDEGE YATINGA IKULU ZANZIBAR

January 24, 2024



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi katikati akipokea Kombe la Mapinduzi kutoka kwa Mfadhili wa Timu ya Mlandege Ndg.Abdulsatar Daudi baada ya kuifunga Timu ya Simba Sport 1-0 mchezo wa Fainal uliochezwa uwanja wa Amani Complex ,wakati wa hafla ya Chakula cha Usiku alichowandalia timu hiyo na Kamati ya maandalizi ya Sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar jana Ikulu Zanzibar (kulia) Rais wa timu ya Mlandege Kamal Abdulsatar Daudi na Hussein Abdulsatar Daudi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (katikatri) akiteta jambo na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemedi Suleiman Abdulla katika viwanja vya Ikulu katikati hafla ya Chakula cha Usiku alichowaandalia Kamati ya maandalizi ya Sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar pamoja na Timu ya Mlandege kwa kuchukua Kombe la Mapinduzi walipoishinda Timu ya Simba Sport 1-0 mchezo wa Fainal uliochezwa uwanja wa Amani Complex (kulia) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akitoa Shukurani zake kwa Makampuni,wafadhili na wananchi mbali mbali kwa michango yao katika viwanja vya Ikulu wakati hafla ya Chakula cha Usiku alichowaandalia Kamati ya maandalizi ya Sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar pamoja na Timu ya Mlandege kwa kuchukua Kombe la Mapinduzi walipoishinda Timu ya Simba Sport 1-0 mchezo wa Fainal uliochezwa uwanja wa Amani Complex

Wachezaji wa Timu ya Mlandege na Viongozi wao wakiwa na Kombe la Mapinduzi walilolipata katika mchezo wa Fainali ya sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa kuifunga Timu ya Simba Sport kwa 1-0, katikati hafla ya Chakula cha Usiku walichoandaliwa pamoja na Kamati ya maandalizi ya Sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika viwanja vya Ikulu ya Zanzibar

Baadhi ya Wananchi walioalikwa katika hafla ya Chakula cha Usiku walichoandaliwa Kamati ya maandalizi ya Sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika viwanja vya Ikulu ya Zanzibar jana na Timu ya Mlandege kwa kutwa Kombe la Mapinduzi walilolipata katika mchezo wa Fainali ya sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa kuifunga Timu ya Simba Sport kwa 1-0,katika mchezo uliochewa Uwanja wa Amani Complex Zanzibar

Wachezaji wa Timu ya Mlandege Sports Club wakiwa katikati hafla ya Chakula cha Usiku kilichowaandaliwa kwa kupongezwa Timu hiyo kwa kuchukua la Kombe la Mapinduzi walipoishinda Timu ya Simba Sport 1-0 katika mchezo wa Fainal uliochezwa uwanja wa Amani Complex na Kamati ya maandalizi ya Sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. [Picha na Ikulu] 22/01/2024.
WAZIRI MCHENGERWA AIPONGEZA TARURA KWA UTENDAJI KAZI MZURIRI

WAZIRI MCHENGERWA AIPONGEZA TARURA KWA UTENDAJI KAZI MZURIRI

January 24, 2024





NA JOHN BUKUKU, DAR ES SALAAM

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Mohamed Mchengerwa ameupongeza utendaji wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa kufanya kazi kwa ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake na kuleta tija kwa Taifa.

Akizungumza leo Januari 24, 2024 Jijini Dar es Salaam kwenye kikao kazi cha Waziri wa TAMISEMI, TARURA , Makatibu Tawala, Wasaidizi Miundombinu, Wakandarasi Wazawa, Wataalam pamoja na washauri wa Taasisi, Mhe.
Mchengerwa, amesema kuwa TARURA wamefanya kazi kubwa kwa kutengeneza barabara kwa kiwango la lami.

Mhe. Mchengerwa amesema kuwa ujenzi wa barabara wa kiwango cha lami umeongezeka kutoka kilometa 1,449.04 hadi kufikia kilometa 3, 224.12 sawa na ongezeko la asilimia 122.4.


Amesema kuwa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha changalawe umeongezeka kwa asilimia 98.44 kutoka kilometa 24, 405.4 hadi kufikia kilometa 41, 107.52.

“Hadi kufikia mwaka 2025 TARURA watakuwa wamejenga barabara kwa kiwango cha lami mjini na Vijiji kwa asilimia 85” amesema Mhe. Mchengerwa.

Ameeleza kuwa wataendelea kutengeneza mazingira rafiki kwa
Wakandarasi Wazawa kwa kuwainua ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kuleta ushindani kwa wakandarasi kutoka Mataifa mbalimbali.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff, amesema kuwa kwa sasa wanatekeleza awamu ya pili ya mpango wa miaka mitano.

Mhandisi Seff amesema kuwa lengo ni kuhakikisha hadi kufikia mwaka 2025-2026 asilimia 85 ya mitandao ya barabara katika Wilaya zote nchini ziwe zinapitika.

Amebainisha kuwa kwa mwaka wa fedha 2023/24 wametengewa shilingi bilioni 818 ambapo bilioni 710 ni fedha za ndani, huku bilioni 107.7 zinatoka kwa wadau wa maendeleo.

Mhandisi Seff amesema kuwa hadi kufikia Desemba 2023 wamefanikiwa kutekeleza asilimia 38 kwa kufanya matengenezo ya barabara ya kawaida kilometa 21,000, lami kilometa 338, changalawe kilometa 8,546 pamoja na madaraja 4, 372.

DK. NCHIMBI AFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU MKUU WA ANC KOMREDI MBALULA

January 24, 2024

 

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Komredi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akipokea zawadi ya kitabu kiitwacho "Dare Not Linger: The Presidential Years" kilichoandikwa na aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Hayati Nelson Mandela na Mandla Langa, kutoka kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Africa National Congress (ANC), chama tawala cha Afrika Kusini, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS),  leo Jumatano, Januari 24, 2024. 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Komredi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwa kwenye mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama cha Africa National Congress (ANC), chama tawala cha Afrika Kusini, Komredi Fikile Mbalula, ambaye yuko nchini kwa ajili ya kushiriki kikao cha Makatibu Wakuu wa Vyama Sita Rafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, kitakachofanyika Januari 25, 2024, nchini Tanzania. Mazungumzo ya makatibu wakuu hao wawili yamefanyika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS),  leo Jumatano, Januari 24, 2024.



Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Komredi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Chama cha Africa National Congress (ANC), chama tawala cha Afrika Kusini, Komredi Fikile Mbalula, leo Jumatano, Januari 24, 2024, walipokutana kwa ajili ya mazungumzo yaliyofanyika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, Kibaha, mkoani Pwani.  




KITUO CHA MAFUTA CHA VICTORIA KUTOA HUDUMA YA BIDHAA ZA CASTROL

January 24, 2024

 NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV


KAMPUNI ya usambazaji wa mafuta na vialinishi vya Castrol nchini, Wambi Lube wamezindua huduma ya Castrol katika Kituo cha Mafuta Victoria ambapo kitaweza kusaidia wateja kupata huduma ya vilainishi na sehemu maalum ya kusubiri huduma yenye huduma za michezo mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 24,2024 Jijini Dar es Salaam, mwakilishi kutoka kwa Castrol Makao Makuu na Meneja wa Afrika Mashariki Bw Ed Savage amesema kuwa wateja wanaweza kupata huduma ya Castrol za daraja la kipekee na pia uhakika wa upatikanaji wa mafundi na wahudumu wa duka walioelimishwa.

Aidha amesema kuwa huduma hiyo inalenga kuhakikisha wateja wa bidhaa za Castrol kuendelea kupata bidhaa bora yenye kupendekezwa kutumika na watengenezaji magari mahiri wanaongoza duniani ili kuhakikisha upatikanaji wa vilainishi halisi vya Castrol 100%.

Na Meneja wa Mauzo wa kampuni ya Wambi Lube, Bw. Steven Jonathan amesema kwasasa ukishafika katika kituo cha mafuta cha Victoria utakutana na mafundi ambao wamefundishwa kuhusu bidhaa za castrol.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Kituo cha Mafuta Cha Victoria Bw. Renald Kyando amesema watumiaji wengi wa magari wamekuwa wakipendekezwa kutumia bidhaa za Castrol wakati wakitaka kubadili vilainishi kwenye magari yao, hivyo basi kituo hicho cha mafuta watakuwa wanatoa huduma bora kwa wateja wao kupitia bidhaa za Castrol ambazo ni bora na za kuaminika.

Amesema kupitia uzinduzi wa huduma hiyo, watahakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa wale ambao watahitaji bidhaa za castrol hasa vilainishi ambavyo watakwenda kuvitumia kwenye magari yao

.
Mmiliki wa Kituo cha Mafuta cha Victoria Bw. Harold Matemba (katikati) akipokea cheti cha uwakala wa uuzaji wa vilainishi vya Castrol Oil hapa Tanzania kutoka kwa Meneja wa Afrika Mashariki Bw Ed Savage wakati wa uzinduzi wa huduma za Castrol katika Kituo cha Mafuta Victoria leo Januari 24,2024 Jijini Dar es Salaam


Mmiliki wa Kituo cha Mafuta cha Victoria Bw. Harold Matemba (katikati) akipokea zawadi ya saa kutoka kwa Meneja wa Afrika Mashariki Bw Ed Savage wakati wa uzinduzi wa huduma za Castrol katika Kituo cha Mafuta Victoria leo Januari 24,2024 Jijini Dar es Salaam



Uzinduzi wa huduma za Castrol katika Kituo cha Mafuta Victoria uliofanyika leo Januari 24,2024 Jijini Dar es Salaam

DKT. NCHEMBA AISHAURI ANGLO GOLD ASHANTI KUIUZIA DHAHABU BENKI KUU YA TANZANIA

January 24, 2024

 Na. Benny Mwaipaja, Dodoma

WAZIRI wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameushauri uongozi wa Kampuni ya Uchimbaji Dhahabu ya Anglo Gold Ashanti, inayomiliki Mgodi wa Dhahabu wa Geita (Geita Gold Mine-GGM), kuanza kuiuzia Serikali dhahabu kupitia Benki Kuu ya Tanzania ili kuiwezesha Serikali kuhifadhi dhahabu kama akiba ya fedha za kigeni.


Dkt. Nchemba ametoa ushauri huo Jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mkuu wa masuala ya Fedha wa Kampuni hiyo, Bi. Gillian Doran, ambapo wamejadili masuala kadhaa ya ushirikiano kati ya Kampuni hiyo na Serikali.


Alisema kuwa hatua hiyo itaifanya Serikali kuwa na chanzo cha uhakika cha kupata dhahabu pamoja na kuwatumia wachimbaji wadogo ambao hivi sasa ndio wanaofanyabiashara ya kuiuzia dhahabu Benki Kuu ya Tanzania.


“Lengo la hatua ya Serikali ya kuanza kuhifadhi dhahabu kama fedha za kigeni ni kuifanya nchi kuwa na chanzo cha uhakika cha fedha za kigeni kitakachotumika kama dhamana wakati inapohitaji fedha hizo kwa ajili ya matumizi mbalimbali badala ya kutegemea mikopo” alisema Dkt. Nchemba.


Aidha, Dkt. Nchemba alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameilekeza Wizara ya Fedha kuanza kununua dhahabu na kuitunza kama fedha za kigeni, maelekezo ambayo tumeyatekeleza na Benki Kuu imeanza kununua dhahabu.


“Akiba ya Dhahabu itatusaidia kununua bidhaa muhimu zitakazokuwa zinahitajika nchini ikiwemo mafuta na bidhaa nyingine, wakati wa changamoto ya upatikanaji wa fedha za kigeni na hatua hii inafaida kubwa kiuchumi” alisisitiza Dkt. Nchemba


Vilevile Dkt. Nchemba alisema kuwa mitambo ya kuchenjua dhahabu iliyojengwa Geita na Mwanza, itakuwa na manufaa endapo dhahabu inayozalishwa nchini itachakatwa na kuongezwa thamani hapa hapa nchini na kuchangia pato la Taifa.


Katika Mwaka wa Fedha 2023/2024, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imejipanga kununua tani sita za dhahabu kwa ajili ya kuweka akiba katika mfumo wa fedha za kigeni.


Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa masuala ya Fedha wa Kampuni ya Anglo Gold Ashanti, Bi. Gillian Doran, aliipongeza Serikali kwa kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji biashara na kuahidi kuwa itaimarisha zaidi ushirikiano na Serikali kupanua uzalishaji wa madini nchini.


Aliahidi kuufanyia kazi ushauri uliotolewa wa kuiuzia Serikali dhahabu kama njia ya kutunza fedha za kigeni lakini pia kuendelea kusaidia huduma za kijamii katika aneo la mgodi wa dhahabu wa Geita kwa manufaa ya wananchi.

WAZIRI wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb)(kulia), akisalimiana na Afisa Mkuu wa masuala ya Fedha wa Kampuni ya Uchimbaji Dhahabu ya Anglo Gold Ashanti, inayomiliki Mgodi wa Dhahabu wa Geita (Geita Gold Mine-GGM), Bi. Gillian Doran, walipokutana kujadili masuala kadhaa ya ushirikiano kati ya Kampuni hiyo na Serikali, jijini Dodoma.


WAZIRI wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb)(katikati), akimshuhudia Afisa Mkuu wa masuala ya Fedha wa Kampuni ya Uchimbaji Dhahabu ya Anglo Gold Ashanti, inayomiliki Mgodi wa Dhahabu wa Geita (Geita Gold Mine-GGM), Bi. Gillian Doran (Kushoto), akisaini kitabu cha wageni, wakati uongozi wa kampuni hiyo ulipomtembelea jijini Dodoma, ambapo wamejadili masuala kadhaa ya ushirikiano kati ya Kampuni hiyo na Serikali.


WAZIRI wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) ( wa tatu kulia), akiagana na Afisa Mkuu wa masuala ya Fedha wa Kampuni ya Uchimbaji Dhahabu ya Anglo Gold Ashanti, inayomiliki Mgodi wa Dhahabu wa Geita (Geita Gold Mine-GGM), Bi. Gillian Doran (wanne kushoto), baada ya kumalizika kwa kikao kati ya Serikali na Kampuni hiyo ambapo wamezungumza masuala kadhaa ya ushirikiano kati ya Kampuni hiyo na Serikali, jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Kamishna wa Sera Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja (wa pili kulia), Makamu wa Raisi wa Kampuni ya GGM, Bw. Simon Shayo (wa tatu kushoto) na Kamishna Msaidizi wa Sera Wizara ya Fedha, Bw. Cyril Chimilila (kulia).

WAZIRI wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) ( wa tatu kulia), na Afisa Mkuu wa masuala ya Fedha wa Kampuni ya Uchimbaji Dhahabu ya Anglo Gold Ashanti, inayomiliki Mgodi wa Dhahabu wa Geita (Geita Gold Mine-GGM), Bi. Gillian Doran (wanne kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa kikao kati ya Serikali na Kampuni hiyo ambapo wamezungumza masuala kadhaa ya ushirikiano kati ya Kampuni hiyo na Serikali, jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Kamishna wa Sera Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja (wa pili kulia), Makamu wa Raisi wa Geita Gold Mine, Bw. Simon Shayo (wa tatu kushoto) na Kamishna Msaidizi wa Sera Wizara ya Fedha, Bw. Cyril Chimilila (kulia).

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)