DK. KIGWANGALLA AAGIZA MBINU MPYA ITUMIKE KUDHIBITI WANAOCHIMBA MADINI KWENYE CHANZO CHA MAJI YA MTO ZIGI JIJINI TANGA

February 23, 2018

Na Hamza Temba, WMU, Muheza Tanga
..........................................................................

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameuagiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS kujenga kituo cha ulinzi cha kudumu katika eneo la chanzo cha maji ya mto zigi kilichopo ndani ya Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani kwa ajili ya kulinda chanzo hicho.

Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari  baada ya kutembelea eneo la chanzo hicho na kukuta uharibifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya wananchi wanaodaiwa kuchimba madini ya dhahabu katika eneo hilo la hifadhi kinyume cha sheria

"Nimeagiza watu wa TFS wajenge kituo cha ulinzi cha kudumu katika eneo hili, na waweke walinzi wetu wa kudumu hapa badala ya kutegemea kufanya patrol (doria) na kuondoka, kwasababu eneo hili wananchi wanaamini lina madini ya dhahabu kwahivo kila siku wataendelea kuja kujaribu kuvuna dhahabu kutoka hapa.

"Kwasababu sisi kazi yetu ni kuhifadhi Maliasili ambayo tumepata kama urithi wa nchi yetu, niwahakikishie kwamba tutaimarisha ulinzi kwa kuanzisha kituo cha ulinzi hapa ili askari wawe wanabadilishana na kudhibiti kabisa uharibu ambao umekuwa ukifanyika, kwasababu maji yanayotoka katika chanzo hiki yanakwenda kunywesha Muheza yenyewe na wilaya wa Tanga, tukiharibu hapa yatakosekana maji safi na salama"  alisema Dk. Kigwangalla.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala huyo, Prof. Dos Santos Silayo alisema pamoja na eneo hilo kwa sasa kuwa linalindwa na askari wa Suma JKT watahakikisha ulinzi unakuwepo muda wote kwa kutekeleza agizo hilo la Waziri la kujenga kituo cha ulinzi cha kudumu ili askari wawepo katika eneo hilo muda wote.

"Lengo letu ni kuhakikisha kwamba wananchi hawaingii ili tusiwe tunawashtukiza kuwakamata na kwachukulia hatua, lazima tuwe watu wa kuzuia uhalifu usitokee, nia yetu ni kuwa na kituo mara moja kama alivyoelekeza Mhe. Waziri na hili jambo tumelichukua kama maelekezo na tutalitekeleza kwa nguvu kabisa," alisema Prof. Dos Santos Silayo.

Awali Dk. Kigwangalla alitembelea kikundi cha wafugaji wa vipepeo katika Tarafa ya Amani ambao waliiomba Serikali ifungulie vibali vya kusafirisha bidhaa hiyo nje ya nchi, aliahidi kuyafanyia kazi maombi yao huku akiwataka kutumia fursa ya ufugaji huo kama bidhaa ya utalii kuwavutia watalii wanaotembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani.

Akiwa mkoani Tanga alitembelea pia Kituo cha Mambo ya Kale cha Mapango ya Amboni na kusema Wizara yake itaboresha kituo hicho pamoja na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili kupanua wigo wa vivutio vya utalii nchini viweze kuchangia zaidi kwenye pato la Taifa.

Katika ziara hiyo ya siku moja mkoani Tanga alitembelea pia shamba la miti ya Mitiki Longuza, Makumbusho ya Shaban Robert na Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia vipepeo katika moja shamba la wafugaji katika Tarafa ya Amani Jijini Tanga jana. Mbali na biashara ya kuuza vipepeo hao nje ya nchi aliwataka wafugaji hao kutumia fursa ya ufugaji huo kama bidhaa ya utalii kwa kuandaa maonesho maalum ya kuwavutia watalii wanaotembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea zawadi ya pambo la vipepeo kutoka kwa mmoja wa wafugaji Asina Athumani muda mfupi baada ya kukagua shamba la vipepeo katika Tarafa ya Amani Jijini Tanga jana ambapo aliwataka wafugaji hao kutumia fursa ya ufugaji huo kama bidhaa ya utalii kwa kuandaa maonesho maalum ya kuwavutia watalii wanaotembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisaidia baadhi ya watu kupanda mlima baada ya kukagua chanzo cha maji cha Mto Zigi ambacho kipo ndani ya Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani wilayani Muheza mkoa wa Tanga. Ameiagiza TFS kujenga kituo cha ulinzi cha kudumu katika eneo hilo linalovamiwa na wananchi kwa madai ya kuchimba madini ya dhahabu.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya shamba la vipepeo katika Tarafa ya Amani Jijini Tanga jana ambapo aliwataka wafugaji hao kutumia fursa ya ufugaji huo kama bidhaa ya utalii kwa kuandaa maonesho maalum ya kuwavutia watalii wanaotembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani tofauti na hivi sasa wanapotegemea soko la kuuza nje ya nchi. Kulia ni Mbunge wa Muheza, Balozi Adadi Rajabu. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Kituo cha Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora kukagua kituo hicho jana Jijini Tanga ambapo alisema Serikali itaboresha kituo hicho pamoja na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili vichangie zaidi kwenye pato la Taifa. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Kituo cha Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora kukagua kituo hicho jana Jijini Tanga ambapo alisema Serikali itaboresha kituo hicho pamoja na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili vichangie zaidi kwenye pato la Taifa. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Kituo cha Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora kukagua kituo hicho jana Jijini Tanga ambapo alisema Serikali itaboresha kituo hicho pamoja na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili vichangie zaidi kwenye pato la Taifa. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Kituo cha Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora kuhusu kivutio cha utalii cha umbo la asili la ramani ya Afrika alipotembelea mapango hayo jana Jijini Tanga. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo kuhusu asali inayozalishwa na Wakala huyo kupitia shamba la Miti Sao Hill muda mfupi kabla ya kuikabidhi kwa Asha Shaban ambaye ni dada yake na aliyekuwa mshairi na mwandishi mashuhuri wa riwaya Shaban Robert alipotembelea makumbusho ya mwandishi huyo Jijini Tanga jana.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi Asha Shaban ambaye ni dada yake na Shaban Robert aliyekuwa mshairi na mwandishi mashuhuri wa riwaya zawadi ya asali inayozalishwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS kupitia shamba la Miti Sao Hill alipotembelea makumbusho ya mwandishi huyo Jijini Tanga jana. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozana na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo kukagua Kituo cha Mapango ya Amboni wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Tanga jana ambapo alisema Serikali itaboresha kituo hicho pamoja na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili vichangie zaidi kwenye pato la Taifa. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo ya namna ya kupanda miti ya Mitiki kutoka Meneja wa shamba la Miti Longuza alipotembelea shamba hilo jana wilayani Muheza Mkoani Tanga. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa Mkomazi alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Tanga. 

NAIBU WAZIRI WA MADINI AAGIZA KUTOLEWA MIKATABA YA WAFANYAKAZI MIGODINI

February 23, 2018

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua eneo la uchimbaji madini ya makaa ya mawe katika kijiji na Kata ya Magamba baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi kukagua miradi ya uchimbaji madini Mkoani Songwe, Leo 23 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisalimiana na kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Mbozi mara baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi kukagua miradi ya uchimbaji madini Mkoani Songwe, Leo 23 Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua eneo la uchimbaji madini ya makaa ya mawe katika kijiji na Kata ya Magamba baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi kukagua miradi ya uchimbaji madini Mkoani Songwe, Leo 23 Februari 2018.

Na Mathias Canal, Songwe

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ameagiza wamiliki wa kampuni za uchimbaji wa Madini kote nchini kuwapatia mikataba ya kazi wafanyakazi wote pasina kubagua.

Mhe Biteko ametoa agizo hilo Leo 23 Februari 2018 wakati alipotembelea eneo la uchimbaji wa makaa ya mawe katika Kijiji na Kata ya Magamba, Wilayani Mbozi linalomilikiwa na kampuni ya Magamba Coal Mine.

Alisema amejiridhisha kuwa wafanyakazi wengi katika migodi mbalimbali nchini ukiwemo wa Magamba hawana mikataba jambo ambalo linafifihisha uhakika wa ajira zao.

Aidha, Naibu Waziri huyo wa Madini ametoa siku 14 kuanzia Leo 23 Februari 2018 mpaka 9 Machi 2018 kwa kampuni ya Magamba Coal Mine kuwa wamekamilisha taarifa ya utekelezaji wa maelekekezo ya ukaguzi wa migodi yaliyotolewa kwao na Ofisi ya Madini kanda hiyo.

Alisema kuwa endapo watashindwa kufanya hivyo ni wazi kuwa watakuwa wamekiuka masharti ya leseni zao na wajibu wao kwa jamii inayowazunguka na hivyo Wizara itawachukulia hatua bila kuchelewa.

Sambamba na hayo pia kampuni hiyo imetakiwa kuboresha na kuwa na mahusiano chanya na kijiji cha Magamba na serikali kwa ujumla ikiwemo kusaidia kuboresha baadhi ya maeneo ikiwemo sekta ya afya na elimu.

Naibu Waziri wa Madini akiwa katika ziara ya kikazi katika Mkoa wa Songwe alisema kuwa serikali imekusudia kurejesha uchumi fungamanishi kwa wananchi hivyo kampuni haziwezi kuwa na uchumi imara kama zitasalia kuendesha migodi pasina utaratibu wa kisheria.

TAARIFA KUTOKA NDANI YA SHIRIKISHO LA SOKA TFF

February 23, 2018
MZUNGUKO WA NNE KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM KUENDELEA WIKIENDI HII
Hatua ya mzunguko wa Nne(4) wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam inaendelea Jumamosi Februari 24, 2018 kwa michezo miwili.
Singida United watakuwa Uwanja wa Namfua Mjini Singida kucheza na Polisi Tanzania saa 10 jioni na mchezo mwingine utakaohitimisha siku hiyo utakuwa kati ya KMC watakaokuwa nyumbani Azam Complex,Chamazi kuwakaribisha Azam FC saa 1 usiku.
Mzunguko huo wa Nne(4) utaendelea tena Jumapili Februari 25, 2018 kwa Buseresere kuwaalika Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Nyamagana Mwanza mchezo utakaochezwa saa 8 mchana wakati Majimaji FC ya Ruvuma watakuwa nyumbani kwenye uwanja wa Majimaji kuwakaribisha Young Africans ya Dar es Salaam mchezo ukichezwa saa 10 jioni nao Ndanda FC watakuwa ugenini kucheza na JKT Tanzania Azam Complex Chamazi saa 1 usiku.
Mzunguko huwa wa 4 utakamilika Jumatatu Februari 26, 2018 Kiluvya United dhidi ya Tanzania Prisons saa 8 mchana Uwanja wa Mabatini na Stand United watawaalika Dodoma FC saa 10 jioni uwanja wa Kambarage.
LIGI KUU YA WANAWAKE YA SERENGETI PREMIUM LITE KUZINDULIWA RASMI NA WAZIRI MWAKYEMBE JUMAPILI
Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Premium Lite hatua ya Nane bora inataraji kuzinduliwa rasmi mkoani Kigoma Jumapili Februari 25,2018 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika.
Mchezo utakaotumiwa kuzindua ligi hiyo utazikutanisha timu za Kigoma Sisterz ya Kigoma dhidi ya Simba ya Dar es Salaam.
Aidha uzinduzi utaenda sanjari na mpango maalumu wa FIFA wa kuhamasisha soka la Wanawake uliopewa jina la Live Your Goal ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dr.Harrison Mwakyembe.
Mbali na mechi ya uzinduzi mechi nyingine za ligi hiyo ya Wanawake ya Serengeti Premium Lite zinatarajia kuchezwa kesho kwenye viwanja tofauti.
Uwanja wa Samora Panama FC watacheza dhidi ya Evergreen Queens ya Dar es Salaam saa 10 jioni,huko Mbweni JKT Queens watacheza dhidi ya Alliance saa 10 jioni,mabingwa watetezi Mlandizi Queens wanasafiri mpaka Jamhuri Dodoma kucheza na Baobab Queens.
Wakati huohuo Kozi ya makocha wa kozi ya grassroots kwa watoto wenye umri wa miaka 6-12 Wasichana na Wavulana imeanza Jumatano kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Ujiji,Kigoma.
MCHEZO WA LIPULI NA NDANDA WASOGEZWA
Bodi ya Ligi (TPLB) imefanya mabadiliko ya mchezo namba 153 kati ya Lipuli na Ndanda uliokuwa uchezwe Ijumaa Machi 2,2018 kwenye Uwanja wa Samora,Iringa.
Mchezo huo sasa umesogezwa mpaka Jumapili Machi 4,2018 na utachezwa kwenye Uwanja ule ule wa Samora.
Sababu za kusogezwa mbele kwa mchezo huo ni kuipa nafasi Ndanda FC kusafiri kutoka Mtwara baada ya mchezo wao na Yanga ambao sasa umepangwa kuchezwa Jumatano Februari 28 ,2018 kwenye Uwanja wa Nangwana Sijaona ,Mtwara.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF

RAIS DKT.MAGUFULI AFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU WA RAIS WA BURUNDI PIA AKUTANA NA MRATIBU WA MAZUNGUMZO YA AMANI YA BURUNDI RAIS MSTAAFU BENJAMINI MKAPA KAMPALA UGANDA

February 23, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamini Mkapa ambaye ni mratibu wa Mazungumzo ya amani ya Burundi, Kampala nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mratibu wa mazungumzo ya amani ya Burundi Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamini Mkapa, Kampala nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Burundi Gaston Sindimwo kabla ya mazungumzo yao Kampala nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Burundi Gaston Sindimwo, Kampala nchini Uganda.
Makamu wa Rais wa Burundi Gaston Sindimwo akizungumza mara baada ya kikao chake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Kampala nchini Uganda. PICHA NA IKULU

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI SAUDI ARABIA WASHIRIKI MAONYESHO YA UTALII

February 23, 2018
Ubalozi wa Tanzania wa Riyadh nchini Saudi Arabia hivi karibuni ulishiriki katika maonyesho ya Travel and Tourism Pioneers Forum 2018 mjini Riyadh. Maonyesho haya ya kimataifa yaaliandaliwa na Al Awasat Expo chini ya udhamini wa MwanaMfalme HRH Prince Dr. Saif Al Islam. Maonyesho haya yalizishirikisha taasisi mbalimbali zinazohusika na utalii ndani na nje ya Saudi Arabia.
Ubalozi wa Tanzania ulishiriki na kufanikiwa kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini ikiwa ni pamoja na kukutana na mawakala wa utalii, tour operators, travel agencies na makampuni ya kutangaza utalii.
 Baadhi ya wananchi waliotembelea banda la Tanzania katika maonyesho ya Travel and Tourism Pioneers Forum 2018 mjini Riyadh nchini Saudi Arabia.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Iddi Mgaza(kushoto) akizungumza na Mwanamfalme HRH Prince Dr. Saif Al Islam bin Saud bin Abdel Aziz Al Saud alipotembelea banda la Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Iddi Mgaza(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja  na wahudumu wa banda la Tanzania wakati wa maonyesho ya Travel and Tourism Pioneers Forum 2018.
 Wananchi wakiwa kwenye banda la Tanzania walivutiwa na taarifa walizopata na pia kuchukua vipeperushi vyenye taarifa kuhusu Tanzania.
Wakinamama walikuwa ni miongoni mwa watu waliotembelea banda la Tanzania kwenye maonyesho ya Travel and Tourism Pioneers Forum 2018 mjini Riyadh nchini Saudi Arabia.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Iddi Mgaza(wa pili kushoto) akifanya mazungumzo na wananchi waliotembelea banda la Tanzania ili kupata taarifa za kina kuhusu masuala mbalimbali Tanzania kwenye maonyesho ya Travel and Tourism Pioneers Forum 2018 mjini Riyadh nchini Saudi Arabia.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA KENYA UHURU KENYATTA KAMPALA NCHINI UGANDA

February 23, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kabla ya kuanza mazungumzo yao jijini Kampala nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kabla ya kuanza mazungumzo yao jijini Kampala nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya mazungumzo yao Kampala nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kupiga picha ya pamoja na Mawaziri pande zote mbili za Kenya na Tanzania mara baada ya kikao chao Kampala nchini Uganda
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kikao chake na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta Kampala jijini Uganda
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi ajambo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta Kampala jijini Uganda.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta mara baada ya kumaliza kikao chao jijini Kampala jijini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir kabla ya mazungumzo yao jijini Kampala.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Kampala Uganda-PICHA NA IKULU