LULU AOMBA BASATA WARUHUSU KUFANYA MOVIE NUSU UTUPU WAENDANE NA SOKO LA KIMATAIFA
DIVA wa filamu za Kibongo, Elizabeth
Michael ‘Lulu’ ameziomba mamlaka zinazosimamia maadili ya filamu nchini
ziwaruhusu wasanii waigize nusu utupu ili kuendana na soko la kimataifa.
Akitetea hoja yake mbele ya paparazi
wetu, staa huyo aliyeitendea haki filamu ya Foolish Age alitolea mfano
Tamthiliya ya Shuga iliyomtoa Lupita Nyong’o ambayo alicheza akiwa nusu
utupu.
“Wanasema hatufuati maadili wakati kuna
muvi ambazo zipo theatre na watu wanaangalia hazina maadili, wao
wanataka tufanye vitu kwa kudanganya wakati sasa hivi tuko dunia ambayo
tuna takiwa tuweke vitu wazi, wasibane sana,” alisema Lulu.
Na Andrew Carlos, GPL
EU KUISAIDIA TANZANIA MSAADA WA SHILINGI BILIONI 134
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacious Likwelile (kulia) akisaini mkataba wa
msaada wa sh. Bilioni 134 kwa niaba ya Serikali ya Tanzania leo jijini Dar es
salaam. Kushoto ni Balozi EU nchini Filberto Sebregond.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
Dkt. Servacious Likwelile (kulia) akibadilishana hati ya mkataba wa msaada wa
sh. Bilioni 134 waliosaini kwa niaba ya Serikali ya Tanzania leo jijini Dar es
salaam. Kushoto ni Balozi EU nchini Filberto Sebregond.
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
SERIKALI ya Tanzania
imetiliana saini mkataba wa msaada wa zaidi ya Shilingi Bilioni 134 sawa na
Euro milioni 59.5 kutoka Umoja wa Ulaya (EU) kusaidia sekta ya kilimo na
usafirishaji nchini.
Mkataba huo ulisainiwa
na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile kwa niaba ya Serikali
ya Tanzania na Balozi wa EU nchini Filberto Sebregond leo jijini Dar es salaam.
Akizungumza baada ya
kutia saini mkataba huo, Dkt. Likwelile alisema kuwa sehemu ya msaada huo ambao
ni Shilingi Bilioni 82.4 ambazo ni sawa na Euro milioni 36.5 utatumika
kuendeleza sekta ya kilimo na kukuza uchumi nchini kwa kupitia kituo maalum cha uendelezaji kilimo ukanda wa
Kusini Tanzania (SAGCOT) na kuboresha miundombinu ya barabara za ukanda huo.
Vilevile Dkt. Likwelile
alisema kuwa sehemu iliyobaki ya msaada huo ambao ni Shilingi Bilioni 51.9 ambazo
ni sawa na Euro milioni 23 itatumika kuimarisha biashara na ushirikiano katika jumuiya
kwa kuanzisha kituo cha pamoja cha
ukaguzi mipakani (OSIS).
“Vituo hivyo vya
ukaguzi mipakani vitakuwa na manufaa si kwa Tanzania tu, bali hata katika nchi
mbalimbali zinazopakana na Tanzania” alisema Dkt. Lkwelile.
Alifafanua kuwa msaada
uliosainiwa unamanufaa kwa wananchi kwa kuboresha miundombinu vijijini na kusambaza
umeme vitu ambavyo vitasaidia kukuza uchumi na kupunguza umaskini nchini.
MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA WAANZA LEO MKOANI TANGA.
KUSHOTO WA KWANZA NI KAIMU MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE NCHINI,CHARLES CHACHA AKISISITIZA JAMBO KWENYE MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA ULIOFANYIKA LEO KWENYE HOTEL YA TANGA BEACH RESOT.
SEHEMU YA WAJUMBE KWENYE MKUTANO HUO LEO |
WAJUMBE WAKIFUATILIA HOTUBA YA MGENI RASMI KWENYE MKUTANO HUO |
Subscribe to:
Posts (Atom)