WATANZANIA WAASWA KUJITOKEZA KUCHANGIA DAMU

WATANZANIA WAASWA KUJITOKEZA KUCHANGIA DAMU

June 12, 2017
unnamed
NA WAMJW DAR ES SALAAM.
WATANZANIA  waaswa kujitokeza kuchangia damu mara kwa mara ili kuondokana na tatizo la vifo vinavyotokana na upungufu wa damu hasa kwa kina mama wajawazito nchini wanaopoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea katika tukio la uchangiaji damu lililofanyika Makao makuu ya benki ya KCB jijini Dar es salaam.
“Marufuku kwa mtoa huduma yeyote wa afya kuuza damu mgonjwa kwani  wananchi wanachangia damu bure kwa manufaa yao ya baadae aidha kwa wao wenyewe au ndugu zao” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amewaagiza Waganga Wafawidhi wa mikoa kuhakikisha wanaweka mabango yanayoonyesha kuwa damu ni bure kwa wagonjwa wote wanaohitaji huduma hiyo bila ya kubagua mwananchi yeyote.
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa mwananchi yeyote mwenye umri wa miaka 18, mwanamke asiye mjamzito wala  kunyonyesha na asiyekua mgonjwa kama vile kisukari,saratani na mgonjwa wa moyo  anaweza kuchangia damu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya KCB nchini Bw. Cosmas Kimario amesema kuwa wameamua kuaandaa uchangiaji wa damu ili kuisadia Serikali katika sekta ya Afya hususani katika kupunguza vifo vinavyotokana na upungufu wa damu.
NAIBU WAZIRI ANTHONY MAVUNDE AKUTANA NA BALOZI WA USWISI NCHINI TANZANIA MJINI DODOMA

NAIBU WAZIRI ANTHONY MAVUNDE AKUTANA NA BALOZI WA USWISI NCHINI TANZANIA MJINI DODOMA

June 12, 2017
MKAO01 Naibu waziri wa Kazi,Vijana ,Ajira na Watu wenye Ulemavu Ndg. Anthony Mavunde leo amefanya mazungumzo na Balozi wa Uswisi Mh Florence Mattli katika ofisi za Wizara ya Kazi,Vijana,Ajira na Watu wenye Ulemavu mjini Dodoma juu ya namna bora ya ushirikiano kati ya Tanzania na Uswisi katika eneo la Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana kupitia mpango unaotekelezwa na Wizara.
Balozi Mattli ameupongeza mpango wa Wizara wa utekelezaji wa Program ya Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana nchini kupitia mafunzo stadi ambayo yana lengo la kuwajengea Vijana wa Tanzania ujuzi stahiki na hivyo kuwawezesha kuwa na sifa za kuajiriwa,Kujiajiri na kuajiri Vijana wengine.
Balozi Mattli ameahidi kushirikiana na Serikali katika  kuunga mkono juhudi za Wizara katika uendeshaji wa Mafunzo ya Ufundi kwa Vijana kwa kufadhili kiasi cha Shilingi 34,000,000 USD kwa miaka 12 kwa ajili ya utekelezaji bora wa Mpango wa Ukuzaji Ujuzi kwa Vijana nchini
MKAO1

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA RIPOTI YA PILI YA KAMATI YA UCHUNGUZI WA MADINI YALIYO KWENYE MAKONTENA YENYE MCHANGA UNAOSAFIRISHWA NJE YA NCHI

June 12, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Nehemiah Osoro Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakiangalia Ripoti hiyo ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini wakati ikifunguliwa kwenye kabrasha.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionesha Ripoti hiyo ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini mara baada ya kukabidhiwa Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakishuhudia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Ripoti hiyo ya Kamati ya pili ya Uchunguzi Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli  mara baada ya kumkabidhi Ripoti hiyo ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini, Ikulu jijini Dar es Salaam.

AKAZI WA MANISPAA YA UBUNGO WAMPONGEZA JPM KWA MAAMUZI MAGUMU KWA MANUFAA YA WATANZANIA

June 12, 2017
Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe John Pombe Magufuli

Wakazi wa Mitaa tofauti tofauti katika Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es salaam ukiwemo Mtaa wa kimara, Ubungo, Sinza, Mabibo, Mwembechai na Magomeni wamempongeza Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe John Pombe Magufuli kwa kuunga mkono maoni/Mapendekezo ya Ripoti ya pili ya wachumi na wanasheria iliyofanya uchunguzi wa madini yaliyo kwenye makontena zaidi 250 yenye mchanga wa dhahabu yaliyokuwa yamehifadhiwa katika bandari kavu ya MOFED (zamani ZAMCARGO) iliyopo Kurasini jijini Dar es salaam.

Rais Magufuli ameunga mkono ripoti hiyo kutokana na ukiukwaji wa sheria za nchi na upotevu mkubwa wa mapato ya Serikali kupitia biashara ya Makinikia na madini yanayosafirishwa nje ya nchi.

Wananchi hao wamesifu uwepo wa Rais Magufuli huku wakieleza kuwa Tanzania imefanikiwa kupata kiongozi imara na madhubuti atakayeweza kuifanya Tanzania kuwa ya neema na mafanuikio makubwa.

Mapendekezo hayo ya kamati maalumu yaliyoungwa mkono na Rais Magufuli ni ishirini na moja kama ifuatavyo

1. Serikali, kupitia Msajili wa Makampuni ichukue hatua za kisheria dhidi ya kampuni ya Acacia Mining Plc ambayo imekuwa inaendesha shughuli zake nchini kinyume na matakwa ya Sheria.
2. Serikali idai kodi na mrahaba kutoka kwa makampuni yote ya madini ambayo yamekwepa kulipa kodi na mrahaba stahiki kwa mujibu wa sheria.

3. Serikali iendelee kuzuia usafirishaji wa makinikia nje ya nchi mpaka hapo makampuni ya madini yanayodaiwa yatakapolipa kodi, mrahaba na tozo stahiki kwa mujibu wa sheria.
4. Serikali ianzishe utaratibu utakowezesha ujenzi wa kiwanda cha uchenjuaji wa makinikia (smelter) ili kuondoa upotevu wa mapato na kutengeneza ajira kwa watanzania.

5. Serikali ifanye uchunguzi na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waliokuwa Mawaziri, Wanasheria Wakuu wa Serikali na Manaibu wao, Wakurugenzi wa idara za mikataba, na Makamishna wa madini, wanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini na watumishi wengine wa Serikali na watu wote waliohusika katika kuingia mikataba ya uchimbaji madini, utoaji wa leseni za uchimbaji wa madini na kuongeza muda wa leseni, watumishi na wamiliki wa makampuni ya madini, makampuni yaliyohusika kuandaa nyaraka za usafirishaji wa makinikia(Freight Forwarders(T)Ltd na makampuni ya upimaji wa madini kwa kuvunja sheria za nchina upotoshaji.

6. Serikali ifute utaratibu wa kupokea malipo ya mrahaba ya asilimia 90 na kusubiri malipo ya asilimia 10 kulipwa baadaye wakati makampuni hayo ya madini huyauza madini hayo na kupewa fedha taslimu kwa mkupuo.

7. Serikali ifanye uchunguzi kuhusu mwenendo wa Watumishi wa idara ya walipakodi wakubwa katika Mamlaka ya Mapato Tanzania katika kushughulikia madai ya kodi ambayo Mabaraza ya Rufaani ya Kodi na Mahakama zimekwisha yatolea uamuzi na vilevile ichunguze mienendo ya watumishi wa mabaraza ya Kodi kwa kutotolea maamuzi ya kesi za kodi kwa muda mrefu kuhusu mashauri yaliyochukua muda mrefu kukamilika katika vyombo hivyo.

8. Benki Kuu ya Tanzania ifuatilie malipo ya fedha za kigeni yanayotokana na mrahaba kwa mauzo ya madini.

9. Serikali ianzishe utaratibu wa kulinda maeneo ya migodi na viwanja ndege vilivyopo vigodini ili kudhibiti vitendo vya hujuma vinavyoweza kuwa vinafanywa na makampuni ya migodi ikiwemo utoroshaji wa madini.

10. Sheria iongeze kiwango cha adhabu zilizoainishwa kwa makosa ya ukiukwaji wa Sheria ya Madini na Sheria za Kodi.

11. Serikali kupitia wataalum wabobezi katika majadiliano na mikataba (expert in negotiation and contract) wapitie mikataba yote mikubwa ya uchimbaji madini ipitiwe (review) na kufanya majadiliano na makampuni ya madini ili kuondoa misamaha yote ya kodi isiyokuwa na tija kwa taifa na badala yake kuweka masharti yenye tija kwa pande zote mbili kwa kuzingatia maslahi ya nchi;

12. Sheria iweke kiwango maalum cha asilimia ya hisa ambazo zitamilikiwa na Serikali katika makampuni yote ya madini nchini. Aidha, Sheria ielekeze Serikali kufanya majadilaino ili kuwezesha Serikali kununua hisa katika makampuni ya uchimbaji madini ili kuiwezesha kupata mapato zaidi na ushiriki katika maamuzi muhimu katika biashara ya madini.

13. Serikali iunde chombo cha kusimamia biashara ya usafirishajibidhaa nje ya nchi kupitia bandari kama ilivyokuwa kama lilivyokuwa shirika la NASACO ili kudhibiti biashara haramu na kuondoa mianya ya ukwepaji kodi.

14. Sheria itamke bayana kuwa madini ni mali asili ya watanzania na iwekwe chini ya udhamini na uangalizi wa Rais kwa manufaa ya watanzania.

15. Sheria itamke bayana kuwa mikataba yoyote ya uchimbaji mkubwa wa madini (Mining Development Agreement) isiwe ya siri na lazima yaridhiwe na Bunge kabla ya kuanza kutekelezwa.

16. Sheria itoe masharti ya wazi ya kuzingatiwana iondoe uhuru wa mamlaka ya (discretionary powers) za Waziri wa Nishati na Madini, kamishna wa madini na maafisa madini wakanda katika utoaji wa leseni za uchimbaji madini.

17. Sheria ya madini iweka masharti kwamba mwombaji wa leseni ya uchimbaji mkubwa wa madini lazima yaoneshe mchanganuo wa kina kuhusu namna mafunzo kwawazawa yatakavyotolewa kwa lengo la ajiri kama wataalam na kuchukua nafasi za uendeshaji wa migodi husika na kupunguza au kuondoa kabisa wataalam kutoka nje ya nchi.

18. Sheria ielekeze makampuni ya madini kuweka fedha zinazotokana na mauzo ya madini katika benki zilizopo nchini ili kuimarisha uchumi wa nchi na kuondoa mianya ya ukwepaji wa kodi na tozo mbalimbali.

19. Serikali ipitie na kufanya marekebisho au kufuta na kubadili kabisa Sheria ya Madini na Sheria za Kodi ili kuondoapamoja mambo mengine masharti yote yasikuwa na manufaa kwa taifa ikiwa ni pamoja na masharti yaliyomo kwenye kifungu thabiti (stability provision).

20. Serikali igharimie nakutoa mafunzo kwa watumishi wa Serikali ili kuwapatia uelewa na weledi katika nyanja ya majadiliano na uendeshaji wa mashauri yatokanayo na mikataba ikiwemo ya mikataba ya madini (skills in negotiation and arbitration).

21. Serikali kupitia Kamishna wa Madini iwe inafanya ukaguzi wa mara kwa mara kaw makampuni ya madini ili kujihakikishia uzingatia au ukiukwaji wa Sheria na taratibu za uendeshaji na kuchukua hatua ipasavyo.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO

Dkt. Shein atoa wito kwa Baraza la Wauguzi na Wakunga la Zanzibar

June 12, 2017
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametoa wito kwa Baraza la Wauguzi na Wakunga la Zanzibar kusimamia vyema Sheria ya Baraza hilo sambamba na maadili kwa lengo la kuwahudumia vyema wananchi na kuzifanya huduma za afya zizidi kuimarika na kuendelea kuijengea sifa Zanzibar kama ilivyokuwa hapo siku za nyuma.

Dk. Shein, aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Wajumbe wa Baraza la Wauguzi na Wakunga waliofika Ikulu mjini Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha kwa Rais wakiwa wameongozana na uongozi wa Wizara ya Afya chini ya Waziri wa Wizara hiyo Mahmoud Thabit Kombo.

Katika maelezo yake Dk. Shein aliwaeleza Wajumbe hao haja na umuhimu mkubwa wa kuipitia na kuisoma vyema vifungu vyote na hatimae kuifanyia kazi Sheria ya Baraza la Wauguzi na Wakunga la Zanzibar ya mwaka 2014 ili waweze kuliongoza vyema na kwa ufanisi zaidi Baraza hilo.

Dk. Shein, alisema kuwa iwapo Sheria hiyo itasimamiwa vyema  fani ya Uuguzi itaendelea kuwa na mafanikio makubwa sana hapa Zanzibar.

Alieleza matumaini yake makubwa kwa wajumbe hao ambao wamechaguliwa kutokana na kuwa kazi hiyo wanaiweza na kuwapongeza kwa kufanya mambo mengi tokea kuzinduliwa Baraza hilo lenye Wajumbe 13 Mrajis na wasaidizi wake wawili mmoja Pemba na mmoja Unguja mnamo mwezi June mwaka 2015.

Aidha, Dk. Shein alisisitiza suala zima la maadili ambalo ndio jambo muhimu katika fani yoyote duniani na kueleza kuwa katika fani ya Uuguzi suala la maadili ndio jambo la kulipa kipaumbele ili kuweza kutoa huduma nzuri ya afya kwa jamii.

Sambamba na hayo, Dk. Shein alieleza umuhimu wa kuwepo kwa usimamizi katika suala zima la uuguzi kwani hatua hiyo itaipelekea Zanzibar iweze kutajika na kuirudisha katika hali yake ya zamani ambapo wananchi kutoka ndani na nje ya Zanzibar walikuwa wakija hapa nchini kufuata huduma za afya.

Akieleza suala zima la upungufu wa wauguzi, Dk. Shein alisema kuwa upungufu wa wauguzi ni suala la muda mrefu na kusisitiza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea na juhudi zake za kuhakikisha inatatua changamoto hiyo hatua kwa hatua.

Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa Baraza hilo kwa hatua yake ya kusimamia vyema suala la mafunzo kwa wauguzi ambapo tayari kwa maelezo ya Wajumbe hao kuna wauguzi 893 wenye Diploma ya Uuguzi, 97 wenye Digirii ya Kwanza, 25 wenye Digrii ya Pili na 1 anaefanya Shahada ya Uzamivu (Phd) katika kada hiyo.

Aliongeza kuwa kwa kutambua umuhimu wa kada hiyo, Baraza lina kazi kubwa ya kuteua Kada muhimu za mafunzo katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) sambamba na wajibu mkubwa wa kusimamia utafiti.

Katika kutilia mkazo jambo hilo, Dk. Shein alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wake imeamua kwa makusudi kuanzisha Taasisi ya Utafiti ya Afya kwa kutambua kuwa utafiti husaidia kutoa huduma bora za matibabu katika sekta ya afya.

Mapema Waziri wa Wizara ya Afya Mahamoud Thabit Kombo  alieleza kuwa mkutano kati ya Rais pamoja na Baraza hilo umekuja wakati muwafaka ambapo Wizara yake imeahidi mambo mbali mbali katika Baraza la Wawakilishi linaloendelea na kwa mashirikiano ya pamoja kati ya Wizara na Baraza hilo yanaweza kutekeleza kile alichokiahidi katika Baraza hilo hivi karibu katika Bajeti yake.

Waziri Kombo alieleza miongoni mwa changamoto ni pamoja na kuwekwa pembeni maadili ya uuguzi, lugha isiyofaa zidi ya wagonjwa, wagonjwa kutozwa fedha za dawa ambazo zipo hospitalini na zimenunuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ajili yao mambo ambayo ameahidi kuyavalia njuga katika kupambana nayo kwa mashirikiano na Baraza hilo.

Nae Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee alieleza haja ya kujua mahitaji ya wauguzi pamoja na upangaji wa wauguzi katika hospitali za hapa nchini kwani licha ya kuwepo kwa idadi ndogo ya wauguzi lakini suala zima la usimamizi limekuwa likikosekana katika eneo hilo kama ilivyo kwa taasisi nyengine za Serikali.

Dk. Abdulhamid alisisitiza kuwa licha ya Utumishi kufanya juhudi za makusudi katika sekta ya afya lakini kinachoonekana ni kuwa wengi wanaoajiriwa katika sekta hiyo hufanya kazi kinyume na ajira yao na ndipo unapotokea upungufu wa wafanyakazi huku akieleza kuwa ni vyema mafunzo yakawa yanaleta mabadiliko ya kiutendaji kwa watendaji wa kada hiyo ya Uuguzi pamoja na kada nyengine ndani ya taasisi za Serikali.

Nae Mwenyekiti wa Baraza hilo Bi Amina Abdulkadir Ali alitumia fursa hiyo kutoa historia kwa ufupi ya Baraza hilo hapa Zanzibar pamoja na hatua, utekelezaji na maendeleo ya kazi za Baraza sambamba na mafanikio na changamoto zilizopo.

Akitaja miongoni wma mafanikio, Bi Amina aliseama kuwa ni pamoja na kupata ofisi na vitendea kazi, kuweza kufungua akaunti,kudumisha mashirikiano na Wauguzi wa Tanzania Bara pamoja na wale wa nchi za Afrika ya Mashariki na Jumuiya za Kimataifa.

Aliongeza kuwa kuweza kuwachukulia hatua kwa onyo au kusimamisha kwa wauguzi waliokuwa na makosa ya maadili na kosa la kughushi vyeti, idadi ya wanafunzi wanaotaka kusoma Uuguzi imeweza kuongezeka ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita sambamba na kuadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani tarehe 12, Mei mwaka huu huko Pemba kwa pesa za Baraza kupitia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar bila ya kuwahusisha wahisani.

Hiyo inatokana na ahadi yake Waziri wa Afya ya kushuka chini Ngazi ya Utendaji ili kuhakikisha ufanisi, Uwajibikaji na Usimamizi na kuwataka Watendaji wote waungane nae mkono badala ya kulalamika kuwa wanaingiliwa katika majukumu Yao. 

Majukumu yote ya Wizara ya Afya na Hospitali pamoja na Vituo vyake vyote Vya Afya vipo chini ya Dhamana ya Wizara Ya Afya ambapo yeye Waziri wa Afya ndiye aliye na Dhamana Kuu ya Wizara hiyo katika Usimamizi na Utendaji ulio bora katika kutoa Huduma kwa Wananchi wote wa Zanzibar bila ya Ubaguzi wa Aina yoyote. Pia Mhe. Waziri wa Afya ametoa tamko la kushirikisha Kitengo cha Huduma kwa Jamii na Ustawi Wa Jamii kushirikishwa kikamilifu pale panapokuwa na tatizo ama upungufu wa Huduma au Mawasiliano kwa Wagonjwa na Wauguzi wanaotokana na Familia zao

Mbio za mwenge wa uhuru zazindua ujenzi wa kiwanja cha Philip Morris Tanzania mjini Morogoro

June 12, 2017

Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Philip Morris Tanzania Ltd Dagmara Piasecka akipokea mbio za mwenge wa Uhuru baada ya kuzindua ujenzi wa kiwanda mjini Morogoro Jumamosi .
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi wa kiwanda cha Philip Morris Tanzania jana mjini Morogoro. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro. Ujenzi wa kiwanda hicho ambao utagharimu zaidi ya 60bn/- utawaongezea faida wakulima wa zao la tumbaku hapa nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akizungumza baada ya uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa kiwanda cha Philip Morris Tanzania jana mjini Morogoro. Kulia ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour na kushoto ni mkurugenzi wa kampuni Dagmara Piasecka. 
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo akizungumza baada ya uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa kiwanda cha Philip Morris Tanzania jana mjini Morogoro. Kulia ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour na kushoto ni mkurugenzi wa kampuni Dagmara Piasecka.
 

Wakulima wa zao la tumbaku nchini wanatarajia kufaika na ulimaji wa zao hilo baada ya kampuni yaPhilp Morris Tanzania Limited kuwekeza zaid ya Sh. Bilioni 60 kwenye ujenzi wa kiwanda kipya, eneo la Kingolwira katika Halmashauri ya Morogoro mjini.

Kampuni ya Philip Morris ambayo imekuwa ni mnunuzi mkubwa zaid wa tumbaku inayolimwa zaidi hapa nchini ikiwa inanunua zaidi ya asilimia 40, inatarajiwa kuongeza ununuzi wake baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kiwanda.

Akiongea wakati wa kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho, kiongozi wa kitaifa wa mbio za mwenge wa uhuru Amour Hamad Amour amesema amefurahisha na uamuzi wa kampuni ya Philip Morris Tanzania kuamua kujenge kiwanda hapa nchini kwani mbali na kuongeza ununuzi wa zao la tumbaku na kuongeza kipato kwa wakulima wetu, lakini pia kitatoa ajira kwa watanzania na pia kuongeza na kukuza uchumi wa taifa.

‘Nimepata taarifa kuwa kampuni hii imekuwa ndio inaongoza kwa kununua tumbaku ya Tanzania na sasa mmeamua kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda. Nawapongeza sana kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ambapo kauli mbiu yake ni Tanzania ya viwanda. 
 
Lakini pia serikali imekuwa kwa muda mrefu ikitaka makampuni kuwekeza kwenye viwada na hasa vya mazao ya kilimo kwa kunaongeza thamani ya mazao yetu na kuongeza kipato kwa wakulima wetu,’ alisema Amour huku akiongeza kuwa makampuni mingine yanayonunua bidhaa za mkulima ni muhimu wakawekeza kwenye viwanda ili kupata bidhaa za mwisho zinazotengenezwa hapa nchi.

Serikali imekuwa msitari wa mbele kuunga juhudi zozote za kuinua kipato cha wakulima wetu. Hii imejidhiirisha baada ya budget ya mwaka kufuta baadhi ya kodi ambazo zimekuwa ni changamoto kwa wakulima. Hii yote inaonyesha ni jinsi ngani tumekuwa msitari wa mbele kukuza sekta hii kwa vyovyote mwekezaji yeyote inakuja na kuwekeza kwenye kilimo ni wa kupongezwa, aliongeza Amour.

Nawapa changamoto wakulima wetu wa tumbaku kuongeza bidii ya kulima zao hilo kwani mnunuzi mkubwa wa zao lao kwa sasa ameamua kuja na kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda. Hii ni faida kwa upande wao. 


Aliongeza Amour huku akitoa rai kwa wafanyikazi ambao watapata ajira kwenye kiwanda hicho cha Philip Morris Tanzania kufanya kazi kwa bidii kwani kutakuwa ni chachu ya kuvuta wawekezaji zaidi.’Uwekezaji kama huu ni taji kwa wasomi wetu kwani kunapanua ajira hapa nchini lakini nawaomba Watanzania ambao watapata hiyo fursa kuheshimu kanuni za ajira na kuwa na uhusiano mwema na wawekezaji kwani kiwanda kikifanya kazi zake kwa faida wafanyakazi pia nao watanufaika, alisema Amour.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uhusiano Philip Morris Tanzania Evans Mlelwa amesema uamuzi wa kampuni yake kuamua kujenga kiwanda hapa nchini kunatokana na mazingira mazuri ya biashara, amani na utulivu, kiwango cha ukuaji wa uchumi pamoja na sera nzuri ya viwanda hapa nchini  Tanzania.

‘Manufaa ya kiwanda hiki ni katika kuongeza mapato yatokanayo na na kodi kwa serikali, kodi ya mapato, kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na pia kuongeza kwa ulimaji wa zao la tumbaku na kutoa ajira katika nyanja mbali mbali kama uzalishaji na usambazaji, alisema Mlelwa huku akiongeza kuwa kampuni yake itajikita zaidi kwenye huduma za jamii kama elimu na kuhahakisha Wananchi wanaozunguka kiwanda wanapata maji salama kwa matumizi ya nyumbani.

‘Wanawake wamekuwa wakisahaulika sana. Sisi tuna mpango mzuri wa kuwawezesha na kuwainua kichumi na ndio maana nasema kiwanda kiwanda hiki kitakapokamililika kitakuwa na manufaa mengi kwa Wananchi wetu, alisema Mlelwa.
MAFUNZO KWA WATAFUTAJI KAZI KWA WILAYA YA MJINI ZANZIBAR YATOLEWA.

MAFUNZO KWA WATAFUTAJI KAZI KWA WILAYA YA MJINI ZANZIBAR YATOLEWA.

June 12, 2017
unnamed
Baadhi ya washiriki wa mafunzo kwa watafutaji kazi kuhusu mfumo wa Taarifa za soko la ajira kwa Wilaya ya Mjini wakimsikiliza Mgeni rasmi hayupo pichani katika ufunguzi wa mafunzo hayo aliofanyika katika Ukumbi wa Hospitali ya Wagonjwa wa akili Zanzibar.
1
Mkurugenzi Ajira kutoka Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Ameir Ali Ameir akitoa hotuba ya kumkaribisha mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo kwa watafutaji kazi kuhusu mfumo wa Taarifa za soko la ajira kwa Wilaya ya Mjini yaliofanyika katika Ukumbi wa Hospitali ya Wagonjwa wa akili Zanzibar.
2
Baadhi ya washiriki wa mafunzo kwa watafutaji kazi kuhusu mfumo wa Taarifa za soko la ajira kwa Wilaya ya Mjini wakimsikiliza Mgeni rasmi hayupo pichani katika ufunguzi wa mafunzo hayo aliofanyika katika Ukumbi wa Hospitali ya Wagonjwa wa akili Zanzibar.
3
Mkuu wa Wilaya ya Mjini Marina Joel Thomas akitoa hotuba ya ufunguzi katika mafunzo kwa watafutaji kazi kuhusu mfumo wa Taarifa za soko la ajira kwa Wilaya ya Mjini yaliofanyika katika Ukumbi wa Hospitali ya Wagonjwa wa akili Zanzibar.
4
-Mkurugenzi Ajira kutoka Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Ameir Ali Ameir akitoa mafunzo kwa watafutaji kazi kuhusu mfumo wa Taarifa za soko la ajira kwa Wilaya ya Mjini yaliofanyika katika Ukumbi wa Hospitali ya Wagonjwa wa akili Zanzibar.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

MARAFIKI WA BAHARI WAUNGANA KUSAFISHA FUKWE ZA MBEZI BEACH

June 12, 2017
Taswira kabla ya kuanza kwa usafi wa fukwe ya Mbezi Beach ambapo ni fukwe inayotumiwa na wakazi wa Mbezi Beach  na maeneo ya jirani , lakini kuna uchafu mwingi uliokusanyika pembeni hapo na kuleta kero kwa wakazi hao wanaotumia fukwe hii kwa mapumziko .
Wadau na marafiki wa bahari wakiendelea kufanya usafi katika maeneo ya fukwe hii ya  Mbezi Beach  ikiwa ni moja ya juhudi za kuweka mazingira safi ya bahari ikiambatana na kuunga kampeni ya kimataifa ya kutunza fukwe na mazingira ya bahari kuelekea kutimiza  Agenda ya mwaka 2030 ya mpango wa maendeleo ya Umoja wa mataifa .Kampeni hiyo inaratabiwa na kampuni ya KONCEPT ,Nipe Fagio na Marafiki wa Bahari na usafi huo ulifanyika mapema mwisho wa wiki iliyopita.

Baadhi ya sindano zilizopatikana wakati wa usafi wa fukwe ya Mbezi Beach uliofanyika mapema mwishoni wa wiki iliyopita ,Sindano hizi ni hatari kwa watumiaji wa fukwe hasa kwa watoto wanaocheza bila kuwa na tahadhari.
Taswira ya Fukwe ya Mbezi Beach wakati wa usafi ukiendelea 
Taswira za baadhi ya takataka na chupa zilizopatikana katika fukwe ya Mbezi Beach
Mkazi wa Mbezi Beach Beatrice   aliyeungana na marafiki wa bahari katika kusafisha fukwe hizo za  Mbezi Beach akiendelea na usafi mwishoni wa wiki iliyopita .

Usafi ukiendelea katika fukwe ya Mbezi Beach ikiwa ni moja ya juhudi za kuweka mazingira safi ya bahari ikiambatana na kuunga kampeni ya kimataifa ya kutunza fukwe na mazingira ya bahari kuelekea kutimiza  Agenda ya mwaka 2030 ya mpango wa maendeleo ya Umoja wa mataifa .Kampeni hiyo inaratabiwa na kampuni ya KONCEPT ,Nipe Fagio na Marafiki wa Bahari na usafi huo ulifanyika mapema mwisho wa wiki iliyopita.

 Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT  Krantz Mwantepele ambao ni waratibu wa kampeni hii ya TANZANIA  OKOA BAHARI na Afisa wa NIpe Fagio  wakiwa wameshikilia moja ya sindano zilizopatikana katika fukwe hizo za Mbezi Beach katika usafi uliofanyika mapema mwishoni wa wiki iliyopita.
Baadhi ya wakazi wa Mikocheni B na Mbezi Beach waliojitokeza kusafisha Fukwe ya Mbezi Beach mapema wiki iliyopita wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza usafi huo.Usafi huo ni moja ya juhudi za kuweka mazingira safi ya bahari ikiambatana na kuunga kampeni ya kimataifa ya kutunza fukwe na mazingira ya bahari kuelekea kutimiza  Agenda ya mwaka 2030 ya mpango wa maendeleo ya Umoja wa mataifa .Kampeni hiyo inaratabiwa na kampuni ya KONCEPT ,Nipe Fagio na Marafiki wa Bahari na usafi huo ulifanyika mapema mwisho wa wiki iliyopita.
Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT  Krantz Mwantepele ambao ni waratibu wa kampeni hii ya TANZANIA  OKOA BAHARI akifanya mahojiano na mahojiano na mwandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kutunza fukwe na mazingira ya bahari mara baada ya kufanya usafi katika fukwe za Mbezi Beach.  



PICHA ZOTE NA FRED NJEJE WA BLOG ZA MIKOA