MAMLAKA ZAZUZUNGUMZIA AJALI YA DALADALA KUZAMA ZIWA VICTORIA.

October 09, 2017
Watu 12 wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa baada ya daladala waliyokuwa wakisafiria, kutumbukia katika fukwe za Ziwa Victoria katika eneo la Kingo Feri wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa tano asubuhi baada ya daladala hiyo yenye nambari za usajili T.229 DDW Toyota Hiace iliyokuwa ikitokea Buhongwa Jijini Mwanza kwenda kivukoni hapo kudaiwa kukatika breki ikiwa kwenye mwendo kasi.

IHEMBE MABINGWA KOMBE LA MBUNGE WA KARAGWE

October 09, 2017
 Mbunge wa Karagwe Mheshimiwa Innocent Bashungwa akimpokea mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba
 Mgeni rasmi akiwasili katika uwanja wa changarawe ilipofanyika fainali ya Bashungwa Karagwe Cup
 Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akikagua vikosi vya Ihembe na Nyaishozi
 Mchezaji wa Ihembe akipiga mpira wa kona
 Uwanja wa Changarawe ulihosheheni mamia ya mashabiki wa mpira wa miguu
  Ihembe wakishangilia baada ya kupata bao la kwanza
 Wadau wakishuhudia mtanange toka jukwaa la “mzunguko”
 Wachezaji wa Ihembe wakiwa wamemzunguka golikipa wao baada ya kupata kash kash
 Mashabiki wa Nyaishozi wakifuatilia kwa makini mchezo wa Bashungwa Karagawe Cup
 Kombe likikabidhiwa kwa mgeni rasmi
Mbunge wa Karagwe Mh. Innocent Bashungwa akitoa neno la pongezi kwa timu zote shiriki
 Kocha wa Kagera Sugar Meck Mexime akimkabidhi kombe nahodha wa Ihembe
 Ihembe wakifurahia kombe lao la ubingwa wa Bashungwa Karagwe Cup
Furaha na shangwe baada ya kutangazwa mabingwa

Timu ya kata ya Ihembe imeibuka mabingwa wa Bashungwa Karagwe Cup 2017 baada ya kuifunga Nyaishozi mabao 2-1. Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Changarawe huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Mambo ya ndani Mheshimiwa Mwigulu Nchemba uliteka hisia za mamia ya wakazi wa jimbo la Karagwe waliojitokeza kwa wingi.

Ihembe walikuwa wa kwanza kupata goli dakika 25 kupitia kwa Athumani Chuji aliepiga shuti kali la mpira wa adhabu uliomshinda golikipa wa Nyaishozi na kuingia wavuni. Bao hilo lilionekana kuwachanganya Nyaishozi ambao walionyesha kutoelewana katika eneo la ulinzi na kujikuta wakiruhusu bao la pili katika dakika ya 35 lililofungwa na Mshauri Kato aliewatoka walinzi wa Nyaishozi na kufunga goli la kiustadi.  Kipindi cha pili Nyaishozi waliuanza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya  78 lililofungwa na mshambuliaji MC, hata hivyo jitihada za kusawazisha matokeo zilikwamishwa na mlinda mlango wa Ihembe alieokoa michomo mingi.

Kufuatia ushindi huo Ihembe walijipatia kombe na kiasi cha fedha shilingi milioni moja na nusu huku Nyaishozi wakipata shilingi laki saba na nusu kama kifuta jasho kwa kushika nafasi ya pili. Akizungumza baada ya mchezo huo mbunge wa Karagwe Mheshimiwa Innocent Bashungwa alisema mashindano hayo yatakuwa endelevu kila mwaka ili kuibua vipaji vya vijana wa Karagwe waweze kujiajiri kupitia michezo na kuahidi kuboresha mashindano yajayo kwa kusaka wadau wengine watakaohakikisha wilaya ya Karagwe inakuwa na timu bora ya kushiriki ligi kuu.

Nae kocha bora wa ligi kuu msimu uliopita ambaye pia ni kocha wa Kagera Sugar Meck Mexime aliyapongeza mashindano hayo na kuahidi mchezo wa kirafiki baina ya Kagera Sugar na  kikosi cha wachezaji bora waliochaguliwa toka mashindano hayo.

KAIMU MKURUGENZI RAHCO AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA USIKU KATIKA MRADI WA RELI YA KISASA

October 09, 2017
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa (wa pili kulia) akiongozwa na  Meneja Mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge kutoka RAHCO, Maizo Mgedzi (kushoto) pamoja na Meneja mradi huo kutoka kampuni inayotekeleza mradi huo ya YAPI Merkezi kutoka Uturuki, Abdullah Milk mara baada ya kufika eneo la Soga - Kibaha jumamosi usiku kuona endapo wakandarasi wa mradi huo wanafanya kazi usiku na mchana kama walivyosema katika mkataba wao na serikali.
 Meneja Mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge kutoka RAHCO, Maizo Mgedzi akitoa ufafanuzi juu ya mradi.
 Watanzania waliopata nafasi ya kufanyakazi katika mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge wametakiwa kufanya kazi kwa uweledi na kuacha ubabaishaji. Ujumbe huo aliutoa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa wakati alipofanya ziara ya kushtukiza usiku wa jumamosi katika kambi mbalimbali za mradi huo zilizopo Pugu mpaka eneo la Soga Kibaha ili kuona endapo wakandarasi wa mradi huo wanafanya kazi usiku na mchana kama walivyosema katika mkataba wao na serikali. Kadogosa alisema mradi huo unatakiwa kwenda kwa kasi na kukamilika haraka hata kabla ya muda husika hivyo kila mtu atakayefanya kazi katika mradi huo anakikishe anafanya kazi na sio ubabaishaji utakaopelekea mradi huo kuchelewa. Aidha Kadogosa alisema wamefikia makubaliano ya kufanya kazi usiku na mchana ili kuharakisha mradii huo na wakandarasi wanafanya haraka na kwa ukubwa wa mradi huu ni lazima tufanye kazi usiku na mchana. “Kama mnakumbuka wakati Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa alipokuja hapa alisema ni lazima twende kasi na wakandarasi wetu wameamua kwenda na kasi na sasa mnaona tuta linaendelea vizuri ni lazima mradi huu ufanywe usiku na mchana kutokana na ukubwa wake,”alisema.

WAFANYAKAZI WA BIMA YA BRITAM WATOA MSAADA KATIKA KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA CHA CHAKUWAMA.

October 09, 2017
Mkuu wa operesheni wa Bima ya Britam, Farai Dogo  akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto yatima cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza jijinini Dar es Salaam ikiwa ni kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka wiki ya kwanza Oktoba duniani Kote.
Meneja masoko wa bima ya Britam,Godfrey mzee akimkabidhi Katibu Mtendaji wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha CHAKUWAMA, Hasan Khamis msaada huo ni shukrani kwa wateja wa bima iyo ambapo wameona watoe faida kwa watoto yatima wanaolelewa katika kituo kilichopo sinza jijini Dar es Salaam.

WAFANYAKAZI wa bima ya Britam ambayo hutoa bima za magari, bima za nyumba, bima za wakandarasi, bima za usafiri wa majini pamoja na bima za safari bima za afya pamoja na nyingine nyingi wametembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza jijini Dar es Salaam.

Wafanyakazi hao wametoa vitu mbalimbali kama vile Unga kilo 300 Maharage 250,Sukari kilo 200,sabuni za unga,Karatasi nyeupe (limu bunda)200,Daftari boksi 500, Mafuta ya kula lita 100,chumvi pamoja na vifaa mbalimbali vya shule.

Vitu hivyo vyote vimegharimu shilingi milioni Saba ambayo wameona wagawane faida waliyoipata katika kushaherekea wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka wiki ya kwanza ya Oktoba duniani kote.

Kwa upandewa  Katibu mtendaji wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha CHAKUWAMA, Hasan Khamis  amewashukuru uongozi kampuni ya bima ya Britam  kwa kuwaona wao kwani kunavituo vingi hapa nchini "Tunashukuru kwa kutuona sisi CHAKUWAMA na kwa kuona mchango wetu.
 Wafanyakazi wa bima ya Britam wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakikabidhi vitu mbalimbali kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha CHAKUWAMA kilichopo sinza jijini Dar es Salaam. 
Katibu mtendaji wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha CHAKUWA, Hasan Khamis akizungumza na wafanyakazi wa bima ya Britam na kuwaelezea historia ya kituo hicho pamoja na changamaoto pamoja na mafanikio waliyoyapata.
Pia amewashukuru wafanyakazi wa bima ya Britam kwa kuwapa msaada huo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa bima ya Britam wakimsikili katibu Mtendaji wa kituo cha kulelea watoto yatima cha CHAKUWAMA kilichopo Sinza jijini Dar es Salaam.
 Wafanyakazi wa Bima ya Britam wakimsikiliza Mlezi Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha CHAKUWAMA, Saida Hasan walipotembelea katika kituo chake jijini Dar es Salaam.
 Wafanyakazi wa Bima ya Britam wakiwa katika picha ya pamoja na Mlezi Mkuu wa Kituo cha CHAKUWAMA, Saida Hasan walipotembelea katika kituo chake kilichopo Sinza jijini Dar es Salaam.
 Mfanayakazi wa Bima ya Britam akiwahudumia wateja walipita kupata taarifa mbalimbali za bima hiyo ikiwa ni kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ambayo hufanyika kila mwaka iki ya kwanza ya mwezi Oktoba.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Bima ya Britam wakiwa katika picha ya  pamoja jijini Dar es Salaam.
-- Othman Michuzi Editorial Director & Chief Photographer CELL: +255 713 775869 /+255 789 103610 WEB: issamichuzi.blogspot.com mtaakwamtaa.co.tz michuzijr.blogspot.com EMAIL: othmanmichuzi@gmail.com Dar Es Salaam. Tanzania. East Africa.

BENKI YA CRDB YACHANGIA UJENZI WA VYOO WILAYANI CHATO

October 09, 2017
Meneja wa CRDB tawi la Mwanza, Wambura Calystus, akizungumza kwenye zoezi la kukabidhi vifaa hivyo katika halmashauri ya wilaya ya Chato mkoani Geita.

Walioketi ni Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato, Mwl.Delphina Cosmas (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wakubwa Goodluck Nkini, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji CRDB.

Na Binagi Media Group
Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, benki ya CRDB imechangia vifaa vya ujenzi wa vyoo katika shule za halmashauri ya wilaya ya Chato mkoani Geita ili kusaidia utatuzi upungufu wa vyoo katika shule za halmashauri hiyo.

Mkurugenzi wa CRDB tawi la Mwanza, Wambura Calystus alisema vifaa hivyo vitasaidia ujenzi wa vyoo katika shule za msingi za Kalema, Muungano na Katemwa A na kwamba vifaa hivyo vimejumuisha mifuko 150 ya theruji, mabati, sinki za vyoo pamoja na vyombo vya kukusanyia taka na tenki la maji kwa ajili ya halmashauri ya Chato.

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato, Mwl.Delphina Cosmas aliishukuru benki hiyo na kubainisha kwamba bado kuna uhaba wa vyoo kwenye shule nyingi na kuiomba kuendelea kusaidia utatuzi wa changamoto hiyo ili kutoa chachu kwa wadau na benki nyingine kuiga mfano huo.

Zoezi la kukabidhi vifaa hivyo lilifanya ijumaa Oktoba 06,2017 katika halmashauri ya wilaya ya Chato ikiwa ni muda mfupi baada ya benki ya CRDB kutoa semina kwa wateja wake wilayani humo na pia kutoka maeneo jirani ikiwemo Muleba, Katoro na Biharamulo.
Meneja wa CRDB tawi la Chato, Msigwa Mganga, akizungumza kwenye zoezi la kukabidhi vifaa hivyo.
Zoezi la kukabidhi vifaa vya ujenzi wa vyoo katika shule za halmashauri ya Chato.
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato, Mwl.Delphina Cosmas (wa pili kushoto) pamoja na viongozi wengine wakipokea vifaa hivyo.

TAMASHA LA TIGO FIESTA LAACHA GUMZO MKOANI NJOMBE

October 09, 2017

Wasanii wa kizazi kipya wa kundi la Rostam wakiwa kwenye staili ya aina yake kwenye jukwaa la tamasha la  Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa sabasaba mjini Njombe usiku wa kuamkia jumamosi.

Msanii Ommy Dimpoz akitoa burudani kwenye jukwaa la tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika  uwanja wa sabasaba mjini Njombe usiku wa kuamkia jumamosi.

KAMPUNI YA BIMA YA RESOLUTION YAZINDUA NJIA YA IRAP ILI KUWAJENGEA UWEZO WAFANYAKAZI WAKE,JIJINI DAR.

October 09, 2017
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Resolution na Kampuni ya Mikopo ya Resolution Bw. Peter Nduati akielezea mabadiliko mbalimbali ya kampuni,katika utendaji kazi na kuwajibika kwa wafanyakazi na kuwasisitiza kuchapa kazi zaidi.

WASHINDI WA TIGO FIESTA SUPANYOTA 2017 NJOMBE

October 09, 2017
Mshindi wa Tigo Fiesta Supanyota 2017 Njombe,  Diana Matimbwa  wa Njombe  akiimba kwa hisia wakati wa mashindano hayo mwishoni wa juma lililopita.
Mashabiki wakimnyanyua Mshindi wa Tigo Fiesta Supanyota 2017 Njombe, Tigama Chanika kutoka Makambako  
Mshindi wa Tigo Fiesta Supanyota 2017 Njombe, Tigama Chanika kutoka Makambako  na Diana Matimbwa  wa Njombe  wamaeibuka washindi namba moja kati ya wasanii watano walio ingia kwenye mchuano wa kutafuta mshindi na wamefungana kwa viwango vilivyo pelekea wote waingie namba 1 bora Supanyota fiesta 2017 Njombe.