Wateja wa Tigo mjini Morogoro wajishindia Tiketi za kwenda kushuhudia Tamasha la Tigo Fiesta

November 05, 2017

Wasanii Roma(kulia) na Zaiid wakimkabidhi mteja wa Tigo, Francis Wamonje(katikati)zawadi ya tiketi ya kwenda kishuhudia Tamasha la Tigo Fiesta litakalofanyika leo mjini Morogoro
Mteja wa Tigo mjini Morogoro, Idrissa Bakari (katikati) aliyejishindia tiketi ya kwenda kushuhudia Tamasha la Tigo Fiesta uwanja wa Jamhuri leo, akipokea tiketi yake toka kwa Wasanii, toka kushoto Barnaba,Mimi Mars, Maua Sama na Country Boy.

Tigo Yatangaza Mbinu za Usajili kwa Washiriki wa Dodoma Marathon

November 05, 2017
Kaimu Mkurugenzi wa Tigo kanda ya kaskazini, Henry Kinabo(kulia) akizungumza na waandishi wa habari jana namna ya kujisajili mbio za Dodoma Marathon zitakazotimua vumbi jumapili ya tarehe 12 mwezi huu, ambapo utaweza kujisajili kwa Tigopesa kwa namba 0674 444 444 kwa punguzo la asilimia 10%. Pembeni ni Meneja wa Maendeleo wa Vision Sports, Raymond Mchani.
Watakaojisajili kupitia Tigo Pesa kupata asilimia 10% punguzo la bei. 
 Dodoma.  Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali, Tigo Tanzania wakiungana na Vision Sports wametangaza kuanza kwa usajili wa washiriki katika mbio za Dodoma Marathon. Mji wa Dodoma utageuzwa kuwa kitivo cha mazoezi na furaha kwa familia nzima tarehe 12 Novemba wakati shindano hilo litakapohitimishwa. 
Usajili kwa Dar es Salaam unafanyika katika vituo maalum vya Duka la Tigo Shop lililopo Mlimani City, Duka la Simply Elegant lililopo Dar Free Market, Ghorofa ya Chini ya Kibo Complex eneo la Tegeta na Duka la Imalaseko SuperMarket lilipo eneo la Posta katikati ya jiji. Kwa Dodoma, usajili unafanyika katika eneo la Dodoma Hotel, Carnival, Cape Town Complex iliyopo Kisasa na Duka la Tigo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). 
‘Wale watakaojisajili kwa njia ya Tigo Pesa watapata punguzo la bei la asilimia 10%. Wanaweza kufanya hivyo kwa kutuma kiasi cha shilingi 13,500/- kutoka kwenye simu zao za mkononi kwenda namba ya Tigo Pesa 0674 444 444. Hapo hapo watapokea ujumbe utakaowataarifu kujisajili na eneo ambalo wanafaa kwenda kuchukua vielelezo vyao vya usajili,’ Meneja wa Tigo, Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo alisema. 
Kwa upande wake,Meneja wa maendeleo wa Vision Sports, Raymond Mchani kwa niaba ya  Ally Nchahaga, Mkurugenzi Mtendaji wa Vision Sports aliwashauri washiriki kusoma vigezo na masharti ya ushiriki pamoja na taarifa nyingine muhimu kutoka kwenye tovuti ya Dodoma Marathon na katika vituo vya usajili. ‘Pia ni muhimu kwa washiriki kuhudhuria kikao cha maelezo kuhusu ushiriki na usalama wa washiriki kitakachofanyika kabla ya mbio kuanza saa kumi na mbili asubuhi, pale katika Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma. 
Tigo inathamini mbio za kilometa 21 za Tigo Dodoma Half Marathon. Dodoma Marathon pia itahusisha mbio ndefu za kilometa 42, mashindano ya kilometa 10 pamoja na yale ya kilometa 5 yatakayohusu wanafamilia na jamii yote kwa ujumla. Zawadi murwa zitatolewa kwa washiriki ikiwemo vyeti vya ushiriki, medali na zawadi za fedha kwa washindi wa mbio zote. Wanariadha mashuhuri kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kushiriki katika mbio hizo. 
“Tuna furaha kubwa kudhamini shindano hili ambalo linahamasisha watu kuzingatia afya bora kwa kushiriki katika michezo, na pia kuinua vipaji katika michezo,” Henry Kinabo, Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini alisema. 
Kuhusu Tigo:
Tigo Tanzania ni kampuni ya simu inayotoa huduma bora za maisha ya kidigitali nchini Tanzania. Tigo ilianza kuendesha shughuli zake nchini Tanzania mwaka 1995.
Kupitia huduma zake za kipekee za sauti, ujumbe mfupi, intaneti yenye kasi na huduma za kifedha kupitia simu za mikononi, Tigo inaongoza kwa ubunifu wa kidigitali kwa kuwa kampuni ya kwanza Tanzania kuzindua facebook na smartphone zenye lugha ya Kiswahili, huduma ya TigoPesa, pamoja na huduma ya kwanza inayowezesha wateja kufanya miamala ya fedha kupitia simu za mkononi kwenda nje ya nchi yenye uwezo wa kubadili thamani ya fedha kwa sarafu ya nchi husika Afrika Mashariki.     
Tigo ni kampuni ya simu ya pili kwa ukubwa nchini na ni kampuni ya simu inayokuwa kwa kasi zaidi nchini kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo. Kupitia mkakati mkubwa wa kupanua na kuboresha huduma zake, kati ya mwaka 2015 hadi 2016, Tigo  ilizindua mtandao wa 4G LTE jijini Dar es Salaam na katika miji mingine 22 nchini
Tigo inajivunia jumla ya watumiaji milioni 10 wa simu waliosajiliwa, na imetoa nafasi za ajira za moja kwa moja na zile zisizokuwa na moja kwa moja kwa Watanzania wapatao 300,000; hii ikiwa ni pamoja na wawakilishi wa huduma kwa wateja, wafanyabiashara wakubwa wa fedha kupitia simu za mikononi, mawakala wa mauzo na wasambazaji.   
Tigo ni nembo ya kibiashara ya Millicom, kampuni ya kimataifa inayoongoza mageuzi ya maisha ya kidigitali katika nchi 13 duniani. Ikiwa inaendesha shughuli zake za kibiashara katika bara la Afrika na Amerika ya Kusini, Ofisi kuu za Millicom zipo Ulaya na Marekani. 
Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz
UVCCM: UTENDAJI MIAKA MIWILI YA SERIKALI YA JPM KIELELEZO CHA UZALENDO

UVCCM: UTENDAJI MIAKA MIWILI YA SERIKALI YA JPM KIELELEZO CHA UZALENDO

November 05, 2017

pongezi tanga5
Kaimu katibu mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCM) Shaka Hamdu Shaka (wa tatu kulia)akishiriki kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa kongamano la tathmini ya uchambuzi wa utendaji wa miaka miwili wa serikali ya Rais John Magufuli kwenye Ukumbi wa BKM Mkoani Tanga jana.Kulia ni Mweyekiti  wa ccm wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Khamis Mkoba(picha na Fahdi Siraji)
pongezi tanga6
Chipukizi wa CCM Mkoa wa Tanga wakiimbisha Wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa kongamano la tathmini ya uchambuzi wa miaka miwili ya serikali ya Rais John Magufuli kwenye Ukumbi wa BKM Mkoani humo.
pongezi tanga9
Sehemu ya washiriki kwenye kongamano lililoandaliwa na uvccm kuhusu tathmini na uchambuzi wa miaka miwili ya utendaji wa  serikali ya Rais Dk John Magufuli  lilifanyika Mkoani humo (picha na fahd Siraji)
pongezi tanga11
Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Allan Kingazi akihutubia katika kongamano lililoandaliwa na uvccm kuhusu tathmini na uchambuzi wa utendaji wa miaka miwili ya serikali ya Rais Dk John Magufuli (picha na Fahdi Siraji)
pongezi tanga12
Katibu wa uvccm wilaya ya Tanga mjini Abdurahman Killo akisoma tamko la uvccm kuunga mkono utendaji wa miaka miwili wa serikali ya  Rais  John Magufuli lilifanyika ukumbi wa BMK Mkoani Tanga(Picha na Fahdi Siraji)
pongezi tanga15
Sehemu  ya uwakikisjinwa Jumuiya ya Wanawake Mkoa Tanga walioshiriki kwenye kongamano la tathmini ya Uchambuzi wa utendaji wa miaka miwili ya serikali ya Rais dk John Magufuli likifanyika mkoani Tanga.
pongezi tanga18
Mwenyekiti wa uvccm Mkoa Tanga Abdiely Makange akizungumza kabla ya kumkaribisha Kaimu katibu mkuu wa uvccm Shaka Hamdu Shaka azungumze na makundi ya vijana wa vyuo na vyuo vikuu.mama lishe.na boda boda kwnye Ukumbi bwa  BMK Mkoani Tanga(picha na Fahdi Siraji)
pongezi tanga20
pongezi tanga21
Kaimu katibu mkuu Shaka Hamdu Shaka akizumgumza kwenye kongamano lilioandaliwa na uvccm kuhusu  tathmini ya uchambuzi wa utendaji wa miaka miwili  wa serikali ya Rais dk John Magufuli kwenye ukumbi wa bmk Mkoani Tanga jana.(picha na Fahdi Siraji)

DC WA HANDENI MH GODWIN GONDWE APOKEA MSAADA WA VIFAA VYA UJENZI WA ZAHANATI WENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 14.7

November 05, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe amepokea msaada wa vifaa vya ujenzi wa zahanati wenye thamani ya Shilingi Milioni 14.7 za Kitanzania kutoka Darworth Ltd, Mwekezaji wa kiwanda cha usindikaji matunda, kama shukurani baada ya kupewa ardhi yenye ukubwa wa ekari 10 kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho Kitongoji cha Mkomba katika Kijiji cha Michungwani Wilayani Handeni..

Akizungumza wakati wa mapaokezi ya vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya amewataka Viongozi ngazi ya Kata kuhakikisha wanasimamia na kutumia vifaa kwa kadri ilivyokusudiwa na kwamba asitokee mtu yeyote kupindisha matumizi au kusimamisha ujenzi wa zahanati hiyo ambayo itakuwa na manufaa kwa wananchi wote.

Ameongeza kuwa yote hayo yanafanywa kwaajili ya wananchi wa Handeni na kwamba maendeleo hayana itikadi, hivyo roho ya maendeleo iliyopo waishikilie ili wasonge mbele kwa pamoja kwakuzingatia kuwa wanatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi.

Gondwe amesema kuwa Mh.Rais ameagiza kuwepo kwa maeneo yanayotengwa rasmi kwaajili ya viwanda , na sisi kama viongozi tumejumuika kwa pamoja kusimamia agizo la Mh.Rais, kwa Handeni ni wajibu wetu kuhakikisha tunaendelea kutenga maeneo kwaajili ya viwanda kama ambavyo kiwanda hiki kitakavyojengwa.

“Asitokee mtu akauondoa umoja huu, huu ni mwanzotu, viongozi tunakazi ya kuhakikisha vifaa hivi vilivyoletwa vinafanye kazi yake na wananchi waone matunda ya rasilimali yao” amesema Gondwe

Kadhalka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe ameahidi kusimamia na kuhakikisha vifaa vyote vinatumika ipasavyo na kutoa ushirikiano kwa mwekezaji ili kufikia malengo ya ukamilishaji wa kiwanda cha kusindika matunda.

Kwa upande wake mwekezaji John Kessy kutoka kamupni ya Darworth Ltd amesema kuwa ujenzi wa kiwanda utakuwa si wa manufaa kwa wananchi wa michungwani tu, bali na hata kwao wawekezaji na ndiomaana wameona vyema kuchangia ujenzi wa zahanati sababu hata wafanyakazi watakaokuwa wanafanya kazi kwenye kiwanda watanufaika na huduma za afya zitakazotolewa hapo.

Aliongeza kuwa watafurahishwa kama vifaa hivyo vitasaidia kufikia lengo lililokusudiwa kwakuwa huo ni mwanzo na kwamba watendelea kufanya kazi bega kwa bega kwa kushirikiana na Serikali ili kufikia uchumi wa Tanzania ya Viwanda.

Mkuu wa Wilaya amepokea vifaa ambavyo ni Mabati (ya geji 28) 200, nondo Tani3,mifuko 200 ya saruji na mabomba lora 3 ambayo yatatumika kusambaza maji kutoka kwenye zahanati hadi kiwandani na kufanya jumla ya Mil.14.7, hatua ya ujenzi kwa sasa ipo kwenye michoro ambapo kiwanda kinatarajiwa kujengwa kuanzia Januari 2018 na kukamilika Desemba 2018. Mapokezi hayo yalijumuisha viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya Wilaya hadi ya Kata.


Imetolewa na:
Kitengo cha Teknolojia,Habari na Mawasiliano.
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni
4/11/2017 

 Mkuu wa Wilaya ya Handeni MH. Godwin Gondwe  (mwenye koti jeusi akipokea nondo kutoka kwa mwekezaji John Kessy kwa ishara ya kupeana mikono na viongozi wengine wakishuhudia
 Mkuu wa Wilaya ya Handeni  kulia name Mwekezaji upande wa Kushoto akipokea mfuko wa saruji kuwakilisha mifuko mingine  ,pembeni ni viongozi mbalimbali wa Halmashauri
 Mapokezi ya mabomba kwa ajili ya kusambazia maji,  Mkuu wa Wilaya ya Handeni  mwenye koti jeusi akipokea kutoka kwa mwekezaji John Kessy, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh Godwin Gondwe akizungumza na uongozi wa Kata kwenye ofisi ya Kijiji cha Michungwani.

Wateja wa Tigo Dodoma wafurika kujinunulia tiketi kwa Tigo Pesa kushuhudia Tamasha la Tigo Fiesta

November 05, 2017
Mtoa huduma ya mauzo wa duka la Tigo Dodoma mtaa wa CDA, Alli Mshana akimhudumia mteja aliyefika kupata huduma dukani mapema mwishoni wa wiki hii.
Mteja wa Tigo, Mwajuma Hassan akikabidhiwa simu na msanii Jux huku wasanii Roma na Ben Pol wakishuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika duka la Tigo Dodoma mara baada ya wasanii kutembelea duka hilo. Ndani ya msimu huu wa Tigo Fiesta kampuni ya Tigo imeweka punguzo la bidhaa mbalimbali kwenye maduka yake yote nchini.
Wateja waliofurika  Duka la Tigo mtaa wa CDA Dodoma wakipata huduma za Tigo Pesa kwa kununua tiketi za Tamasha la Tigo Fiesta Dodoma.

WAZAZI MBURAHATI SACCOS YAIVA, KUPATA HATI YA USAJILI HIVI KARIBUNI

November 05, 2017
 Mwenyekiti wa muda wa Wazazi Mburahati Saccos, John Mapunda akifungua mkutano wa wanachama wa Saccos hiyo, uliofanyika kwenye ukumi wa Jengo la Kitegauchumi la CCM, Mburahati, Dar es Salaam, jana. Amesema ameamua yeye na wenzake kuanzisha ushirika huo wa Akiba na mikopo siyo kwa maslahi ya kisiasa bali kuwasaidia kuwasaidia kiuchumi wanachama wa Jumuiya ya Wazazi katika Kata ya Mburahati ili nao waweze kuwa na maisha bora wakiwa ni miongoni mwa Watanzanaia wenye mahitaji hayo. Kushoto ni Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo ambaye alifika kwenye mkutano huo kutoa mafunzo ya namna bora ya kuanzisha na kuendesha Saccos. Kulia ni Mhazini wa muda Boniface Chigenda na Katibu wa muda Sofia Kiroboto.
 Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo akitoa mafunzo ya namna bora ya kuanzisha Saccos na kuifanya idumu wakati wa mkutano huo. Amesema Saccos hiyo kwa sasa imeshatimiza masharti yote ya kupatiwa usajili na inapatiwa usajili huo hivi karibuni, alisema katika Kadirio lake Saccos hiyo inatarajia kupata zaidi ya Sh. milioni 13 kutokana na ada na michango ya wanachama ambao hadi sasa wamefikia 68, pia kufanya matumizi ya zaidi ya Sh. milioni 13 na kubaki na ziada ya zaidi ya Sh. milioni 29.
 Kitabu au Masharti ya Saccos hiyo
 Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo, akionyesha orodha ya wananchama 68 waliokwishajiunga na Saccos hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa muda John Mapunda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Kata ya Mburahati.
 Ofisa Ushirika wa Manispaa ya Ubungo Emmanuel Philipo akifafanua jambo wakati akionyesha orodha hiyo 
 Baadhi ya wanachama wa Saccos hiyo wakisikiliza Ofisa huyo kwa makini  Mwenyekiti wa muda wa Saccos hiyo John Mapunda akitoa nafasi kwa wanachama kuuliza maswali

Ben Pol awaamsha Wabunge vitini kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Dodoma

November 05, 2017

Wabunge wa bunge la Tanzania wakicheza pamoja na msanii Ben Pol(mwenye shati nyeupe) kwenye Tamasha kubwa la Tigo Fiesta lililofanyika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma usiku wa kuamkia jana.
Msanii Ben Pol akipongezwa na Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Antony Mavunde kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia jana uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Msanii Mimi Mars mdogo wa Vanessa Mdee akifanya yake kwenye Tamasha la Tigo Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia jana uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

DK. KIGWANGALLA ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA ZIWA MANYARA NA KUKAGUA SHUGHULI MBALIMBALI ZA UHIFADHI NA UTALII

November 05, 2017
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akisalimiana na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Manyara, Noelia Myonga alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara, Noelia Myonga (wa pili kushoto) kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akizungumza na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara, Noelia Myonga alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na  Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara, Noelia Myonga alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha. 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara, Noelia Myonga kuhusu hifadhi hiyo alipoitembelea jana mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akiongozwa na Mhifahdi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara, Noelia Myonga kwenda kuangalia kivutio cha Maji ya Moto ya Asili ndani ya hifadhi hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akigusa maji ya moto ya asili ambayo ni kivutio cha kipekee cha utalii kilichopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini. Maji hayo yanakadiriwa kuwa na nyuzi joto 80 ambapo imeelezwa kuwa baadhi ya watalii huweza kuchemsha mayai katika maji hayo. Nyuma yake anayeshuhudia ni Mhifadhi Mkuu wa hifadhi hiyo, Noelia Myonga.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akionyeshwa maeneo ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara na Mhifadhi Mkuu wa hifadhi hiyo, Noelia Myonga alipoitembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa ‘Lodge’ ya AndBeyond Lake Manyara Tree, Mei Saimon (kulia) kuhusu ‘lodge’ hiyo ambayo ipo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa ‘Lodge’ ya AndBeyond Lake Manyara Tree, Mei Saimon (kulia) kuhusu mazingira ya nje ya ‘lodge’ hiyo ambayo ipo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini. 
 Waziri, Dk. Kigwangalla akikagua miundombinu ya lodge hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pili kulia) akikagua mazingira ya Lodge’ ya AndBeyond Lake Manyara Tree ambayo ipo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini. Kulia kwake ni Meneja wa hoteli hiyo, Mei Saimon. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua baadhi ya miundombinu ya kupumzikia wageni katika Lodge’ ya AndBeyond Lake Manyara Tree ambayo ipo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara alipotembelea hifadhi hiyo jana mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini. Kulia kwake ni Meneja wa hoteli hiyo, Mei Saimon. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua baadhi ya miundombinu ya kupumzikia wageni katika Lodge’ hiyo ya AndBeyond Lake Manyara Tree ambayo ipo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa tatu kulia waliosimama) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Nyumba ya Kulala Wageni ya AndBeyond Lake Manyara Tree Lodge ambayo ipo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara wakati alipotembelea hifadhi hiyo jana kwa ajili ya kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi na utalii kwa lengo la kuimarisha uhifadhi endelevu na utalii nchini. 
Simba katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.
Baadhi ya miundombinu ya daraja katika hifadhi hiyo ambayo huwarahisishia watalii kuona wanyamapori mbalimbali.
Pundamilimilia
Ndege na nyati katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.
Ndege aina mbalimbali wanapatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.
Mtoto wa Tembo katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.
Baadhi ya Tembo katika Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara. (PICHA NA HAMZA TEMBA - WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)