WAKINA BABA WATAKIWA KUTOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WATOTO WAO

June 08, 2017
 Ofisa Programu wa TGNP Mtandao, Anna Sangai (kushoto), akitoa mada katika kongamano la siku moja lililohusu elimu ya afya ya uzazi lililofanyika Makao Makuu ya TGNP Mabibo Dar es Salaam jana. Kongamano hilo liliandaliwa na TGNP.

BULEMBO AFUNGA KAZI WILAYA YA MISENYI NA BUKOBA MJINI MKOANI KAGERA

June 08, 2017
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Tanzania Alhaj Abdallah Bulembo akiwasili ukumbini kuendesha kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Misenyi, Mabalozi, viongozi wa Jumuia za CCM na watendaji wa Serikali katika Wilaya hiyo mkoani Kagera, leo
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwaili ukumbini
 Wajumbe wakiwa ukumbini tayari kumsikiliza Alhaj Bulembo
 Katibu wa Jumuia ya Wazazi Tanzana, Wilaya ya Misenyi Rehema Mtawala akimkabidhi zawadi maalum Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo kabla ya kikao kuanza
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akionyesha zawadi hiyo maalum baada ya kukabidhiwa. Zawadi hiyo ina maneno ya kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa Mbunge. 
 Mwenyekiti wa CCM wa CCM Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Haji Seruhu akifungua kikao hicho
 Katibu wa CCM Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera Mwajuma Mboha, akieleza maneno ya utangulizi katika kikao hicho
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akifurahia jambo na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Misenyi Haji Seruhu, wakati wanapita taarifa iliyosomwa na Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo
 Wajumbe wakihamasika kwenye kikao hicho
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na wajumbe wakati wa kikao hicho
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akitulia kumsikiliza kwa makini mshairi Mansur Athan wakati akighani shairi mwishoni mwa kikao hicho
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akipokea zawadi ya Mbuzi aliyopewa na Jumuia ya Wazazi Wilaya ya Misenyi wakati wa kikao hicho leo.
 Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera  Yahya Kateme (kushoto) akibadilishana mawazo na Vijana wa wa CCM nje ya ukumbi baada ya kikao
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Ajhaj Abdallah Bulembo akiendelea kuwasikiliza nje ya ukumbi badhi ya wadau waliotaka ufafanuzi wa baadhi ya mambo baada ya kikao hicho 
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM akiwafafanulia jambo nje ya ukumbi baadhi ya wadau  
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj abdallah Bulembo akiendelea kuwasikiliza wadau hata baada ya kupanda gari lake tayari kwa kuondoka
Baada ya wadau kuridhika wakamuaga kwa furaha na kumtakia safari njema kwenda Wilaya ya Bukoba mjini
 Safari ya Alhaj Bulembo kutoka Misenyi kwenda Wilaya ya Bukoba mjini ilipitia kwenye daraja hili la Mto Kagera, eneo la Kyaka.
 Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera  Yahya Kateme akizungumza na vijana waendesha bodaboda aliowakuta Bukoba Mjini, baada ya msafara wa Alhaj Abdallah Bulembo kuwasili
 Mwenyekiti huyo wa UVCCM akapiga picha ya pamoja na vijana wa green Guard wa Bukoba mjini
 Baada ya kuwasili tu Bukoba Mjini, Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo alieanda ofisini kwa Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Mustafa Kijuu na kuwa na mazungumzo naye kwa muda. Pichani, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo hayo. Wengine kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Lahel Ndegeleki na Mwenyekiti wa CCM mkoa huo Costansia Buhiye
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimweleza jambo Mkuu huyo wa mkoa kabla ya kuondoka 
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akiwasalimia vijana wa green Guard nje ya Ofisi ya Mkuu wa mkoa.
KIKAO BUKOBA MJINI🔽
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akimwelekeza jambo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba mjini Yusuf Ngaiza wakati wa kikao cha Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya hiyo, Mabalozi, viongozi wa Jumuia na Watendaji wa serikali, leo
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bukoba Mjini mkoani Kagera Yusuf Ngaiza akifungua kikao hicho
 Wajumbe wakiwa ukumbini katika kikao hicho
Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza na wajumbe wakati wa kikao hicho Bukoba mjini mkoani Kagera, leo. PICHA; BASHIR NKOROMO

Cisco msiba wa Dar es Salaam

June 08, 2017

Na Benny Kisaka
Abdulkarim Omary Mtiro, almaarufu Cisco  Mtiro, umelala Brother tangulia. 

Umelala usingizi. Usingizi ambao hautaamka wakati huu. Hautaamka brother kwa kuwa wanaolala usingizi huu wanamngoja aliyewaumba awaamshe.

Kwa neema yake kuu iko siku utaamka Brother. Mara hii ukiamka hutalala tena.

Naam, hutalala. Maana utakuwa umevuka ng'ambo ya pili ya mto. Huko hakuna uchungu na maumivu makali kama uliyoyapitia nyakati zako za mwisho za uhai wako ukiwa hospitali ya Aga Khan. Pumzika kaka yetu.

Leo June 7, saa 7 mchana tunakuzika kwenye makaburi ya Kisutu mahali ambapo miezi michache iliyopita tulimzika rafiki yako wa karibu Afande Chicco. Pumzika kwa amani, mpaka tutakapoonana tena huko juu Ng'ambo ya pili.

Mwanadiplomasia uliyewahi kuwa balozi mdogo Nigeria na pia Balozi Kamili nchini Malaysia.

Tunakuita brother kwa wakazi wa Temeke tukijua umezaliwa peke yako kwa Mzee Omary na Bi Ummi Seif. 

Akiwa amezaliwa mtaa Kipata Kariakoo mwaka 1950, baada ya miaka miwili alihamia Temeke hadi anamaliza elimu ya Chuo Kikuu, alihama pale alipoanza kazi wizara ya mambo ya Nje.

Cisco ni jina la utani lililochepua hadi kuliweka rasmi hata kwenye passport yake ikisomeka Abdul Cisco Mtiro amefariki akiwa na miaka 67.

Leo Temeke itanyanyuka eneo ulilokulia na kusoma elimu yako ya msingi shule ya Temeke, na kumaliza elimu hiyo mwaka 1965.

Itakumbukwa 1997 aligombea Ubunge Temeke akishindana na Mrema, viongozi wote wa ngazi za juu wa CCM walikuja kukupigia debe lakini kura hazikutosha.

Umaarufu wako upo Chang'ombe, Ilala, Wailes, Kurasini  Masaki, Magomeni, Mbezi Beach, Kariakoo na hata Kinondoni yote.

Ameishi Mikocheni B hadi umauti umemkuta, lakini muda mwingi amekuwa akikutana na marafiki zake viunga vya Kinondoni kwa John Fedha ama nyuma ya ubalozi wa Ufaransa kijiwe cha Octa.

Ni mmoja wa waanzilishi wa bonanza la kila jpili pale Leaders Club, mshabiki mkubwa wa Yanga, rafiki wa kila tabaka na rika na hakuwa mtu wa kujikweza, umaarufu wake ulitawala kwa kuwa mtu mwenye utani mwingi...

Ni mtoto wa mjini hasa, hakuhitaji aimbwe redioni kutokana na sababu zozote.

Nilikuwepo Kisutu kukuzika bro, ulishiriki msiba wa baba yangu Christopher kisaka, ambaye alikuwa mwalimu wako shuleni Temeke, ulitukaribisha nyumbani kwako kupata chakula cha jioni mara kadhaa tulipofika Kuala Lumpur, Malaysia 2011 nikiwa na Juma Pinto, ulinialika arusi ya mwanao Omary, pia nilishiriki.

Mwanadiplomasia, mkuu wa Itifaki mstaafu kwa Mwalimu Nyerere, Mzee Mkapa na awamu ya nne ya Jakaya Kikwete.
Ulikuwa mgeni rasmi miss Temeke 2003. Ulikuwa judge miss Tanzania 2004.

Cisco ana marafiki lukuki kiasi kila mmoja anaweza kumwandika amjuavyo, tena zaidi na vizuri kutipa mimi, ila kwa udogo huu naomba mwenyezi Mungu akupumzishe kwa Amani🙏

INTANETI INAVYOCHOCHEA UKUAJI WA UTALII BARANI AFRIKA

June 08, 2017

Na Jumia Travel Tanzania

Afrika ni bara la pili kwa kuwa na idadi kubwa ya watu ambapo inafikia takribani bilioni 1.2 (wengi wao wakiishi mijini) na inatarajiwa kongezeka mpaka bilioni 2.5 kufikia mwaka 2050 (25% ya watu wote duniani).
Kwa mujibu wa ripoti ya utalii kwa Afrika mwaka 2017 iliyofanywa na Jumia Travel imebainisha kwamba mtu mmoja kati ya watatu ni sehemu ya watu wa daraja la kati (watu wanaofanyakazi kwenye taaluma na biashara mbalimbali pamoja na familia zao) na wanatarajiwa kuongezeka mara mbili zaidi kufikia 2050. Watu wa daraja la kati ni muhimu katika uchangiaji wa ukuaji wa utalii wa ndani na ukanda mzima tuliopo.