Kikosi cha timu ya Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) kimeodoka leo saa 6 mchana jijini Dar es salaam kuelekea kisiwani Zanzibari, ambapo kitaweka kambi ya mwezi mmoja kujiandaa na fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) mwezi Septemba.
Msafara
wa Twiga Stars umeondoka na boti ya Azam (Kilimanjaro) ukiwa na watu 32,
wakiwemo wachezaji 25, benchi la ufundi 6 pamoja na kiongozi wa msafara, ambapo
TFF imegharamia kambi hiyo ya mwezi mmoja
Wachezaji
waliosafiri leo ni Fatuma Omari, Belina Julius, Happiness Hezron, Fatuma
Hassan, Anastazia Anthony, Fatuma Bashiru, Fatuma Issa, Fatuma Khatibu, Maimuna
Hamis, Donizia Daniel, Sofia Mwasikili, Etoe Mlenzi.
Wenigine
ni Amina Ally, Thereza Yonna, Mwanahamisi Omari, Stumai Abdallah, Shelder
Boniface, Asha Rashid, Najiat Abbas, Estha Chabruma, Mwajuma Abdallah na Fatuma
Mustapah.
Twiga
Stars itakua kambini kisiwani Zanzibar kwa kipindi cha mwezi mmoja, kujiandaa
na fainali hizo za michezo ya afrika, ambapo imepangwa kundi A pamoja na
wenyeji Congo – Brazzavile, Ivory Coast na Nigeria.
Fainali
za Michezo ya Afrika (All Africa Games)
zinatarajiwa kuanza kutivua vumbi Septemba 4 – 19 nchini Congo-Brazzavile.