UMOJA WA WASANII WA FANI MBALIMBALI WAMTANGAZA RAIS DR. JAKAYA KIKWETE KUWA SHUJAA WA SANAA YA MUZIKI NCHINI

August 07, 2015

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani),waliofika ndani ya ukumbi wa Mlimani City  katika hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10 na pia kumtambulisha Mgombea wa Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli,Dkt Jakaya Kikwete alizungumza mambo mbalimbali zikiwemo haki na hatimiliki za wasanii wa muziki pamoja na Bongomovie na pia alikubali kuwa mlezi wa tasnia hizo na kuhakikisha mambo yanakwenda sawa ndani ya tasnia hizo mbili adhimu kwa sasa hapa nchini.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete katikati pichani akiserebuka na wadau wa muziki na huku akipiga nao picha,ndani ya ukumbi wa Mlimani City  katika hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10 na pia kumtambulisha Mgombea wa Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akipiga ngoma huku akishirikiana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga gitaa ndani ya ukumbi wa mlimani City jijini Dar.
Mwanadada Wema Sepetu akimtunza midola Dkt John Magufuli alipokuwa akipiga ngoma jukwaani kwa ustadi mkubwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na Mgombea Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC Itikadi na Uuenezi Nape Nnauye na pamoja na Januari Makamba wakifurahia jambo kwa pamoja na wageni waalikwa mbalimbali waliofika ndani ya ukumbi wa Mlimani City kushiriki hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na Mgombea Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli pamojoa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  (mwisho kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Paul Makonda wakiwasili ndani ya ukumbi wa Mlimani City kushiriki hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10.
PICHA NA MICHUZI JR.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »