TP MAZEMBE YASAJILI BEKI LA SANGA BALENDE TP MAZEMBE YASAJILI BEKI LA SANGA BALENDE

August 07, 2015
KLABU ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya KOngo (DRC) imemsajili beki wa kati anayeweza kucheza kama kiungo pia, Badibake Mpongo.
Mchezaji huyo wa Sanga Balende amesaini Mkataba wa miaka mitatu kuhamia kwa mabingwa wa DRC, baada ya klabu yake kumalizana na Mazembe. 
Na huyo anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na mabingwa wa Ligi Kuu ya DRC ambao kikosi wana Watanzania wawili, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.
Badiabake Mpongo kulia ametua TP Mazembe

Mazembe inaimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ya DRC maarufu kama Linafoot na klabu imefurahia ujio wa mchezaji huyo ‘fundi’.
Kwa upande wake, Mpongo amesema; “Ni heshima kubwa kwangu kujiunga na TPM, klabu ambayo ni faraja ya nchi. Sasa naelekeza fikra zangu katika kucheza na kushinda mataji hapa,”amesema Badibake Mpongo, ambaye tayari ameanza mazoei na The Ravens.
MAONESHO YA WIKI YA NENDA WA SALAMA TANGA.JAMII YATAKIWA KUJIWEKEA AKIBA NA GEPF. Afisa Masoko,Usajili na Ukusanyaji wa mfuko wa hifadhi ya jamii wa GEPF Bw Eric Haule akiwa kwenye banda la mfuko huo ndani ya viwanja vya Tangamano jijini Tanga yanakoendelea maonesho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani kitaifa. Na Godwin Lyakurwa .TANGA. Jamii imetakiwa kuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba kupitia mifuko ya hifadhi ya jamii itakayo wasaidia pindi wanapokabiliwa na majanga mbalimbali kama ajali za barabarani ambazo husababisha majeraha na ulemavu wa kudumu. Hayo yamesemwa na Afisa Masoko,Usajili na Ukusanyaji wa mfuko wa hifadhi ya jamii wa GEPF Bw Eric Haule wakati akizungumza na kituo hiki kwenye banda la mfuko huo katika maonesho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yanayoendelea kwenye viwanja vya Tangamano jiji Tanga. Amesema ukweli ni kuwa hakuna mtu ajiuaye kesho yake kwani majanga ya ajali kuweza kumkuta muda wowote hivyo akiba ni muhimu. Afisa huyo amesema wanashiriki maonesho hayo ili kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara juu ya kujiwekea akiba itakayosaidia baada ya kukumbwa na ajaili hivyo kila mwananchi anakaribishwa kwenye banda lao lililoko ndani ya viwanja vya maonesho hayo. Mfuko wa hifadhi ya Jamii wa GEPF unapokea wanachama wa hiyari na lazima ambao hujiwekea akiba kwa mujibu wa sheria. Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ

Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »