Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo
wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja akiwa katika picha ya pamoja na
wanariadha wa Jeshi la Polisi walioshiriki Michezo ya Majeshi ya Polisi
kwa nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO).Wengine ni Viongozi wa Michezo
wa Jeshi la Polisi (Picha na Alexander Mpeka-Jeshi la Polisi)
Kamishna wa Oparesheni na
Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja akizungumza na Wanariadha wa
Jeshi la Polisi, Wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza iliyofanyika Makao
Makuu ya Polisi Jana baada ya kufanya vizuri katika Michezo ya Majeshi
ya Polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO).Kushoto ni Mkuu wa
Kitengo cha Michezo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Jonas Mahanga (Picha
na Alexander Mpeka-Jeshi la Polisi)
Kamishna wa Oparesheni na
Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja akimpongeza Mwanariadha wa
Jeshi la Polisi, PC Basil John aliyeshinda medali tatu za dhahabu katika
Michezo ya Majeshi ya Polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO),
Wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza iliyofanyika Makao Makuu ya Polisi
Jana.(Picha na Alexander Mpeka-Jeshi la Polisi)
……………………………………………………………………………………….
Michezo ya SARPCCO ilianzishwa
kwa lengo la kuwakutanisha Maafisa na Askari Polisi ili kuweza
kubadilishana mbinu za kukabiliana na uhalifu pamoja na kuwasaidia
kujenga afya na kuwa wakakamavu katika kutekeleza majukumu yao ya kila
siku.
Michezo ni sehemu ya
kuitambulisha nchi yoyote kama Taifa huru lenye utamaduni wake. Michezo
ni mojawapo ya viungo muhimu katika utamaduni wa kila jamii ya binadamu
duniani. Michezo ni chombo muhimu sana katika kuiendeleza jamii. Aidha,
michezo huweza kuwa kielelezo na utambulisho wa Taifa kwa kutoa
burudani, kujenga na kukomaza afya ya mwili na akili, kujenga nidhamu,
kujitangaza kiuwezo na vipaji. Ushiriki katika michezo ya kimataifa
husaidia kulitangaza Taifa nje ya mipaka yetu. Vile vile michezo
huwaweka pamoja Askari na kuwawezesha kufahamiana na kuondoa misongo ya
mawazo “STRESS”. Hivyo Ni wazi kuwa mmetumia vyema fursa mliyoipata
katika michezo hiyo ikiwemo ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika
kutenda kazi za polisi, Hongereni sana.
Nimepewa taarifa kuwa kulikuwa na
ushindani mkubwa katika michezo hiyo na ninyi pamoja na uchache wenu
mmfenakiwa kupata medali 12, 6 za dhahabu, 4 za fedha na 2 za shaba, Pia
timu yetu ya riadha (wanaume) ya mbio ndefu imefanikiwa kuwa timu bora
katika mashindano hayo na Askari PC Basil John aliibuka mchezaji bora wa
mashindano baada ya kushinda medali 3 za dhahabu katika mbio za mita
800, 1500 na mbio za nyika (Km 12 cross country).Nawapongeza sana
walioshinda
Mmefanya kazi kubwa na
mmehakikisha kuwa heshima ya Jeshi letu la Polisi iliyojijengea katika
michezo hiyo tangu kuanzishwa kwake inaendelea kudumu pamoja na uchache
wenu kutokana na wanamichezo wengine kutofanikiwa kwenda kutokana na
sababu mbalimbali.
Aidha nawapongeza sana kwa
nidhamu mliyoionyesha katika kipindi chote cha michezo hiyo, Nidhamu na
kujituma kwa juhudi ndio msingi wa kufanikiwa katika mchezo wowote hivyo
ninyi mmekuwa mabingwa katika kipengele hicho.
Aidha, napenda pia kutumia fursa
hii kuwashukuru wadhamini waliotuwezesha kwa kutupatia vifaa vya michezo
ambao ni Benki ya CRDB, NMB, African Life Assuarance, na PPF, kwani kwa
ufadhili wao walioutoa umefanyiwa kazi na hivyo kupata mafanikio ya
ushindi, Hivyo wakati mwingine wasisite kuiunga mkono timu yetu ya
Polisi.
napenda kuwaahidi kuwa
tutaendelea kuipa kipaumbele michezo ili kuweza kuwaimarisha kiafya na
kuwakutanisha na wenzenu katika mataifa mengine na nawatakieni
maandalizi mazuri katika michezo mingine iliyopo mbele yenu na safari
njema ya kurudi katika mikoa yenu.
AHSANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA.
EmoticonEmoticon