Team Nimes'tuka yavamia Shinyanga na kufanya mikutano na wananchi

October 06, 2015
Kundi la wasanii wanaomuunga mkono Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Dk John Pombe Magufuli jana niliingia mkoani Shinyanga kuhamasisha wananchi umuhimu wa kusikiliza sera kwa kina na kupima ukweli katika utekelezaji wake.
Kundi hilo linaloundwa na muunganiko wa wasanii wa folamu na muziki, limetomiza siku ya 15 ya ziara zao za Kijiji kwa  Kijiji ambapo lengo kuu ni kuwastua vijana wenzao kuacha kufuata mkumbo, na badala yake kusikiliza sera kwa umakini na kupima ukweli wa utekelezwaji wake bila ya kuwa na mihemko ya kidemokrasia.
PICHANIO JUU: Miss Tanzania 2014 Lilian Kamanzima akiongea na umati wa watu uliojitokeza kulisikiliza kundi la Nimestuka, Shinyanga mjini jana
Mmoja kati ya viongozi wa kundi la Nimestuka, Aunt Eze akiongea na wananchi katika mkutano mkutano uliofanyika Shinyanga mjini ambapo walisimama kuhamasisha vijana wenzao kusikiliza sera kwa umakini na kumuunga mkono Mgombea wa Chama cha Mapinduzi, Dk John Magufuli

Msasnii wa filamu dende, akimwaga sera
Msanii wa vichekesho, Kitale a.k.a Mkude, akiwastua wananchi wa Shinyanga katika viwanja vya Buhangija jana

Inspekta Haroun, `Babu', akipagawisha wafuasi wa chama tawala waliohudhuria mkutano wa wasanii wanaounda kundi la Nimes'tuka 
-- Henry Mdimu Mgaya Blogger www.mdimuz.blogspot.com Entertaniment Editor Mwananchi Communications Limited P.O BOX 19754, Dar es Salaam Cell: +255 787 000 880 +255 767 000 880 +255 715 000 881

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »