Fundi
Masafa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Kenny Chitemo
(aliyenyoosha mikono) akiwaonyesha Menejimenti ya Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo moja ya mtambo wa masafa uliwekwa katika
gari la masafa wakati menejimenti hiyo ilipofanya ziara katika ofisi za
TCRA Jijini Dar es Salaam. Katikati mwenye koti la blue ni Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo Bibi. Sihaba Nkinga, na Kulia ni Mkurugenzi Mkuu TCRA
Dkt. Ally Yahaya Simba.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga
(wapili kulia) akiangalia mtambo wa masafa uliokua ukionyeshwa na
Mhandisi Mwandamizi Masafa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Bw.Robson Shaaban (kulia) wakati Menejimenti ya Wizara hiyo ilipofanya
ziara katika ofisi za TCRA Jijini Dar es Salaam.
Menejiment
ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ikimsikiliza kwa
makini Mhandisi Masafa kutoka TCRA Bi. Imelda Salum (kushoto) wakati
Menejimenti hiyo ilipofanya ziara katika ofisi ya TCRA Jijini Dar es
Salaam. Watatu kulia ni Katibu Mkuu Wizara hiyo Bibi. Sihaba Nkinga, na
wapili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu TCRA Dkt. Ally Yahaya Simba.
Katibu
Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga
akizungumza na Menejimenti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo pamoja na Uongozi kutoka TCRA wakati wa ziara iliyofanywa na
Menejimenti ya Wizara ya Habari katika ofisi za TCRA kujifunza mambo
mbalimbali yanayofanywa na Mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Habari kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bibi. Zamaradi Kawawa akifafanua jambo wakati wa ziara
iliyofanywa na Menejimenti ya Wizara Habari kujifunza mambo mbalimbali
katika ofisi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jijini Dar es Salaam
Picha na: Genofeva Matemu - Maelezo