MKURUGENZI
Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMRI), Dk. Mwele
Malecela akifungua mkutano huo wa pili wa mwaka wa kimataifa wa
wataalam wa kudhibiti Mbumbu kwa Nchi zisizofungamana Afrika (PAMCA)
ulioanza leo jijini Dar es Salaam.
Washiriki
wa mkutano huo umeshirikisha Wanasayansi watafiti kutoka nchi
mbalimbali za Afrika. Mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa PAMCA ulifanyika
jijini Nairobi Kenya 2014.
Dk
Malecela amesema kuwa mkutano huu unakutanisha wataalam wa kupambana na
Mbu Afrika nzima wataweza kukaa na kubadilishana uzoefu wao juu ya njia
za kupambana na mbu.
“Wataalam
hawa wanakutana kupitia umoja wao wa PAMCA utawawezesha wataalam hawa
kujadiliana njia mbalimbali za kuweza kupambana na mbu hasa kutokana na
tabia za mbu za kubadilika badilika na kufanya kuwa sugu kwa madawa
mbalimbali,”alisema Dk Malecela.
Amesema
wataalm wa Mbu wanapokutana katika mikutano kama hii huwawezesha
wataalam kupata ujuzi mpya wa kuweza kupambana na kukabiliana na mbu.
Mbu
huambukiza magonjwa mengi, hivyo kuwa na taasisi ya wataalm wa Waafrika
wenyewe ni jambo la kujivunia sana hivyo mkutano huu utaweza
kufanikisha kupata vitu mbalimbali kutokana na mada zitakazo wasilishwa
na ambazo zitaingizwa katika mipango na sera mbalimbali katika nchi
zetu.
Mapema
akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kimadawa
Kenya (KEMRI), Musau Kyanesa amesema lengo la kuanzishwa kwa PAMCA ni
kutafuta njia stahiki ya kupambambana na mdudu mbu ambae hueneza
magonjwa mbalimbali ambayo huathiri binadamu.
“Itakuwa
ni jambo jema sana kama tutaweza kumdhibiti mdudu huyu mbu ambaye
anaeneza magonjwa haya na kufanikiwa kwa hilo tutaweza kuendeleza afya
za wananchi wetu kwa nchi za Afrika, maana Afrika ndio tunapata shida
sana na mdudu huyu mbu,” alisema Kyanesa.
Aidha
Kyanesa ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa KEMRI amesema wameandaa mpango
wa kuhamasisha wanafunzi vyuoni kujikita katika sayansi ya Mbu ili
kupata watalaam wengi wakuweza kukabiliana mbu Kenya na Afrika kwa
ujumla.
"Tunaandaa
mpango wa kuhamasisha vijana kusomea na hatimaye kuwa na utaalm juu ya
mapambano na kufanya tafiti za mbu, kwa kugharamia masomo yao kutokana
na upungufu wa wataalam kulingana na tatizo lenyewe,"alisema Kyanesa.
Mwenyekiti wa Bodi ya PAMCA, Prof Charles Mbogo akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo.
Washiriki wakisikiliza mada mbalimbali katika siku ya kwanza ya mkutano huo, Dar es Salaam leo.
Rais wa PAMCA tawi la Tanzania, Dk Stephen Magesa akizungumza katika mkutano huo.
Mkuu wa NIMRI Tanzania, Dk. Mwele Malecela akizungumza na Mkurugenzi Msaidizi wa KEMRI kutoka Kenya, Musau Kyanesa baada ya ufunguzi wa mkutano huo.
Prof Wen Kilama akiwasilisha mada juu ya Maadili ya Utafiti wa Afya hususani Maleria Afrika .
Prof Wen Kilama akiendelea na uwasilishaji wa mada yake. Prof Kilama ni Mkurugenzi Mstaafu wa NIMR.
Dk Mwele Malecela na washiriki wengine wakifuatilia mada ya Prf Kilama.
Washiriki wakifuatilia mada hiyo.
Picha ya pamoja ya washiriki mkutano huo wakiwa na mgeni rasmi.