Mkurugenzi
Mkuu wa Takukuru nchini, Dkt. Edward Hoseah akizungumza katika sherehe
za uzinduzi wa jengo la ofisi mpya ya TAKUKURU Mkoa wa Mbeya ambapo
amesema kuwa Taasisi hiyo imeweza kufanikiwa kupambana na rushwa kwa
kiasi kikubwa ambapo jumla kesi kubwa za rushwa 1,993 kuanzia mwaka
2004-2015 zimeweza kufunguliwa ambazo ni sawa na ongezeko la asilimia 81
ikilinganishwa na kesi 384 zilizokuwepo miaka 10 ilioyopita
(1995-2004) .
Amesema
,ongezeko hilo la kesi kubwa limetokana na jitihada za Taasisi hiyo
katika kupambana na kuzuia rushwa nchini hasa katika kipindi cha
serikali ya awamu ya nne, chini ya rais Jakaya Kikwete.