Modo
maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick ‘Jack Patrick’ amepandishwa
kortini kwa mara ya kwanza huko Macau nchini China, Aprili 10, mwaka huu
kwa kukutwa na madawa ya kulevya tumboni aina ya heroin kete 57 au kilo
1.1 yakiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 223 huku ishu kubwa
kwa muda wote aliokuwa mahakamani ikiwa ni kuangua kilio kila wakati.
Kete zinazosadikiwa kukutwa na modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick ‘Jack Patrick’ akiwa amezimeza.
Jack
alipandishwa kwenye korti hiyo ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu
alipokamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’ Desemba mwaka jana akitokea
Bongo kupitia Thailand na kuingia nchini humo.
ILIKUWAJE?Kwa
mujibu wa chanzo chetu makini kilichopo Macau, Jack alifikia hatua hiyo
dakika 15 baada ya kupanda kizimbani na kukutana na nyuso za Wachina tu
zikimwangilia.
“Yeye
alijua angekuta Wabongo au hata watu weusi wakimpa kampani, lakini
matokeo yake alikutana na sura za Wachina tu,” kilisema chanzo chetu.
Kikaendelea: “Unajua kwa kawaida mtu anapopanda kizimbani mara zote
anafarijika sana endapo atawaona anaowafahamu, hasa ndugu zake ambao
watafika kumtia moyo, sasa yeye hakulipata hilo.”
DAKIKA 10 ZATUMIKA KUMSOMEA MASHITAKA
Jack akiwa karibu na madawa aliyonaswa nayo.
KUNA MADAI ALIZOMEWA
Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, mbali na kukutana na upweke huo
mahakamani, pia Jack alipata kisanga kingine pale baadhi ya raia wa nchi
hiyo walipomzomea kwa sauti ya chini wakati akitoka kortini.
Inadaiwa kuwa, kwa Wachina kumzomea au
kumsema vibaya mtu aliyedakwa na madawa ya kulevya ni kawaida kwani
hakuna biashara, inapigwa vita nchini humo kama ya unga wakiamini
unaangamiza nguvu kazi ya kizazi kijacho.
NDUGU WADAIWA KUMKATIA MAWASILIANO
Habari nyingine kutoka chanzo chetu
zilidai kwamba, kwa sasa Jack amebaki yeye na Mungu wake baada ya
nduguze waishio Bongo kumkatia mawasiliano kwa kile walichodai kuwa
kitendo alichokifanya kimeiaibisha familia nzima.
“Unajua ndugu zake walikata mawasiliano
kabisa? Nchi nzima au tuseme dunia nzima kilio ni jinsi vijana
wanavyoharibika kwa madawa ya kulevya, sasa kule kubainika kwamba Jack
alibeba unga tumboni kwenda kuuza kumeifanya familia kujisikia vibaya
sana,” kiliongeza chanzo hicho kikiomba chondechonde kisitajwe gazetini.
KAMA ATARUDI BONGO SALAMA
Habari zaidi zinadai kwamba modo huyo
ambaye pia ni Miss Ilala No 3, 2005, aliwahi kumwambia mshirika wake
mmoja akiwa mahabusu kwamba, kama atabahatika kurejea Bongo salama,
atakwenda kupiga dua juu ya kaburi la mama yake ili amsimamie katika
kumwondolea nuksi kama siyo mabalaa. Baba wa Jack anadaiwa kuishi nje ya
nchi.
TUJIKUMBUSHE
Jack alikamatwa Desemba 19, mwaka jana
kwenye Uwanja wa Ndege wa Macau nchini China akitokea jijini Bangkok
nchini Thailand kuelekea Guangzhou, Mji Mkuu wa Jimbo la Guangdong
Kusini mwa China ambako ilidaiwa ndiko alikokuwa anafikisha unga huo.
Ilidaiwa kuwa
miongoni mwa mambo yaliyochangia kukamatwa kwake ni kuonesha uso wenye
uchovu, kuanza kuwa na hali mbaya ya mwili, kushindwa kujibu maswali
vizuri na hati yake ya kusafiria, yaani ‘passport’ kukutwa imegongwa
mihuri ya kuingia nchini humo kila mara jambo ambalo wakaguzi waliliona
si la kawaida kwa msichana kama yeye.
-GPL
EmoticonEmoticon