*MALINZI AWAPONGEZA SUKER, LEKJAA

April 23, 2014

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewapongeza marais Davor Suker na Fouzi Lekjaa kwa kuchaguliwa tena hivi karibuni kuongoza mashirikisho ya mpira wa miguu katika nchi zao. 

Suker amechaguliwa tena kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Croatia (CFF) wakati Lekjaa amechaguliwa kuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Morocco (FRFM).
Katika salamu zake za pongezi, Rais Malinzi amesema ushindi waliopata ni uthibitisho kuwa familia ya mpira wa miguu katika nchi zao ina imani kubwa kwao katika kuendeleza mchezo huo ndani na nje ya nchi hizo.

Rais Malinzi amesema Lekjaa na Suker wana uwezo wa kuendeleza kazi nzuri ambayo tayari imefanyika, lakini vilevile kuja na mawazo mapya ambayo yatakuwa changamoto kwa ustawi wa mchezo huo nchini Morocco na Croatia kwa ujumla.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »