*MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA BUNGE MAALUM LA KATIBA MJINI DODOMA

April 23, 2014

 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,ambaye pia ni  Waziri wa Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia(kulia) akijadiliana jambo  na Madaraka Nyerere ambaye ni mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo. Kushoto ni mjumbe wa Bunge hilo,Leticia Nyerere.
 Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu Hassan (katikati) akizungumza jambo na baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo, wakati wanatoka nje katika kikao cha asubuhi.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ambaye pia ni  Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema(kushoto) akibadilishana mawazo na wajumbe wa Bunge hilo,  Shamsi Vuai Nahodha (katikati) na kulia ni  Dk. Tulia Akson mara baada ya kikao cha leo asubuhi.
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Ezekiah Oluoch, akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma ambapo aliwasisitiza UKAWA kurudi ndani ya Bunge hilo.

Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Ezekiah Oluoch, akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma ambapo aliwasisitiza UKAWA kurudi ndani ya Bunge hilo.
aadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na mwanasiasa mkongwe, mzee Kingunge Ngombale  Mwiru na mjumbe wa Bunge hilo Juma Njumayo aliyevaa mewani mweusi(kulia) baada ya mwanasaiasa huyo. Picha na Magreth Kinabo

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »