Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mbeya
Shindano
la Tanzania Movie Talents Kwa kanda ya Nyanda ya Juu Kusini, Mkoani
Mbeya limefikia Tamati hapo jana kwa washindi watatu kutoka kanda hii ya
nyanda ya juu Kusini Kupatikana na Kutangazwa na Majaji watatu.
Washindi
waliotangazwa na Jaji Mkuu wa Shindano hilo, Roy Sarungi kwa
kushirikiana na Majaji wawili Single Mtambalike na Yvonne Chery ni
Steven Mapunda, Issalito Issaya na Mtawa Kaparata "BABU"
Mmoja
kati ya washindi watatu waliopatikana Jana na Kutangazwa na Jaji Mkuu wa
Shindano hilo Roy Sarungi ni mchezaji wa zamani wa timu ya mpira wa
Miguu ya Majimaji ya Songea, Bw Mtawa Kaparata.
Mtawa
Kaparata aliibuka mshindi kwa kuweza kuonyesha kipaji chake cha kuigiza
achilia mbali uwezo wa mpira aliokuwa nao kipindi hiko.
Kwa
upande wake mmoja wa washindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents
ambae pia alikuwa mchezaji wa zamani wa Majimaji ya Songea , Bwa Mtawa
Kaparata alithibitisha kuwa 'Tanzania
Movie Talents imepokelewa vizuri na watanzania wa Mkoa wa Mbeya kwani
ameona usaili ulivyokuwa mgumu kutokana na vipaji vilivyoonyeshwa na
vijana wengi waliojitokeza na kuona ongezeko la washiriki waliojitokeza
kwaajili ya usaili wa kushiriki katika Shindano hili kubwa na la kwanza
Afrika Mashariki na Kati.
Hii
nikutokana na ukweli kwamba washiriki wote wanaofika kwaajili ya Usaili
hawatozwi kiasi chochote cha pesa kutoka timu ya Tanzania Movie Talents
na pia kufurahishwa na uamuzi wa Majaji wa Timu ya Tanzania Movie
Talents, niwazi kabisa kuwa kutotozwa kwa kiasi chochote cha pesa kwa
washiriki kumekuwa ni kivutio kikubwa kabisa hivyo kuongeza idadi ya
washiriki katika kila Kanda tunayoenda"alisema Mtawa Kaparata Mkazi wa
Mkoa wa Mbeya, Eneo la Soko Matola.
Shindano
hili kwa kanda ya nyanda Ya juu kusini limehitimishwa rasmi jana kwa
washindi watatu kupatikana na hatimaye shindano hili litahamia Kanda ya
Kusini na Usaili utafanyika Mkoani Mtwara
Shindano hili limelenga kuinua na kukuza vipaji vya kuigiza Tanzania na hatimaye kuendeleza vipaji hivi vya kuigiza Tanzania.
Usaili wa Shindano hili ni bure kabisa na fomu hupatikana eneo la usaili.
EmoticonEmoticon