Timu
ya Taifa ya Burundi (Intamba M Rugamba) inatarajiwa kuwasili nchini
kesho (Aprili 24 mwaka huu) saa 12 jioni kwa ndege ya Kenya Airways
tayari kwa mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumamosi (Aprili 26
mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Intamba
Mu Rugamba itakuwa na msafara wa watu 28 wakiwemo wachezaji, benchi la
ufundi na viongozi, na itafikia hoteli ya Accomondia. Mechi hiyo
itachezwa kuanzia saa 10 jioni.
Nayo
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ipo kambini
kwenye hoteli ya Kunduchi Beach ikijiandaa kwa mechi hiyo
itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Kenya.
Viingilio
katika mechi hiyo vitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa,
bluu na kijani. Kwa VIP A kiingilio kitakuwa sh. 20,000 wakati VIP B na C
ni sh. 10,000. Mechi hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya
muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
EmoticonEmoticon