MASOGANGE ASEMA ALIYENIPA MZIGO WA 'UNGA' ALIVAA KININJA

April 23, 2014


‘Video queen’ wa Kibongo, Agness Gerald, ‘Masogange’.

‘VIDEO queen’ wa Kibongo, Agness Gerald, ‘Masogange’, amefunguka  kuwa aliyempa mzigo wa unga  na akakamatwa nao nchini Afrika Kusini, alikuwa amevalia kininja, hali iliyomfanya ashindwe kumtambua.

Masogange amefunguka kuwa aliyempa mzigo wa 'unga', alivaa kama huyu.
Taarifa za uhakika kutoka vyanzo vyetu makini katika kikosi kazi cha kuzuia na kudhibiti madawa ya kulevya nchini (Task Force), zinasema kuwa  mwanadada  huyo alipofika katika nchi hiyo, alipigiwa simu na mtu ambaye hamjui aliyemwambia kuwa atapewa mzigo, hivyo ajiandae kuupokea.

“Alidai kuwa kuna mtu aliyevalia kininja alifika eneo alilokuwepo uwanjani pale ambaye hakumsemesha badala yake alimpatia mzigo wa unga ambao ulikuwa kilo 150 ambao hapa kwetu ni madawa ya kulevya na kuondoka kusikojulika,” kilisema chanzo.

Kwa upande wake, Kamanda wa Kudhibiti na Kupambana  na Madawa ya Kulevya nchini,  Godfrey Nzowa alipohojiwa na gazeti hili alithibitisha kuwa Masogange aliwaeleza polisi wa Afrika Kusini kuwa aliyempa unga ule ni mtu aliyekuwa amevalia kininja. 


“Unajua watu hawa wanaojihusisha na madawa ya kulevya wana mbinu nyingi na wamekuwa wamejiandaa kwa lolote litakalotokea. Naamini alisema vile ili kukwepa kushurutishwa kumtaja aliyempa.

“Aliwaambia kuwa mtu huyo alimpa mabegi yale palepale uwanjani na hawezi kumtambua kwa sura labda kwa fulana aliyokuwa amevaa kwa sababu alikuwa amevaa kininja,” alifafanua Kamanda Nzowa. 

Alisema unga huo ulifanyiwa uchunguzi kwa mkemia mkuu wa serikali wa nchi hiyo na ikagundulika kuwa si Crystal Methamphetamine bali ni Ephedrine ambayo si unga ila ni kemikali hatari ambayo ikichanganywa na dawa nyingine hupatikana unga halisi wa madawa ya kulevya. 

Aliongeza kuwa, mtu yeyote akikamatwa na malighafi  kama  hizo hapa nchini  adhabu yake haizidi  faini ya shilingi milioni 5 au kifungo cha miaka 30 ama zaidi. 
CDT:GPL

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »