NA MWANDISHI WETU,KIGALI.
Jeshi la Polisi nchini Rwanda limewakamata watu watatu
wanaotuhumiwa kutishia usalama wa taifa.
Miongoni mwa waliokamatwa ni
mtangazaji wa redio, ambaye awali aliripoti kuhusu kutoweka kwake pamoja na
mwanamuziki aliye mwanaharakati wa amani.
Katika taarifa yake leo, jeshi hilo limesema
watuhumiwa hao wana uhusiano na chama cha upinzani cha Rwanda National
Congress-RNC, chenye mafungamano na Patrick Karegeya afisa wa zamani wa ujasusi
wa Rwanda aliyeuawa nchini Afrika Kusini mwanzoni mwa mwaka huu.
Watu hao pia wanatuhumiwa mara nyingine kufanya kazi
na kundi la waasi la FDLR, linalojumuisha maafisa waliohusika na mauaji ya
kimbari ya mwaka 1994 ambao wako kwenye misitu ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Kongo.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Cassien Ntamuhanga,
mtangazaji wa Redio Amazing Grace amekamatwa leo, mwanamuziki Kizito Mihigo
alikamatwa Ijumaa iliyopita na askari aliyefukuzwa jeshini Jean Paul
Dukuzumuremyi alikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
EmoticonEmoticon