Wajumbe
mbalimbali kwenye bunge la katiba wameendelea kuwasha vipaza sauti vyao
kuchangia, kutoa ya moyoni kwa kujadili sura ya kwanza na ya sita huku
ishu ya serikali mbili au tatu ikizimiliki headlines zaidi.
Zifuatazo ni kauli za mjumbe Mh. Joseph Mbilinyi ambae pia ni mbunge wa Mbeya mjini April 15 2014
1. ‘Wabunge
Wakristo hii ni kwaresma, ni kipindi cha toba… mnatumia kipindi hiki
kufanya unafiki mbele ya Wananchi mtakuja kuhukumiwa siku itakapofika,
wameharibu mchakato wakati tumeshatumia mabilioni mengi ya hela’
2. ‘Ukarabati
tu wa jengo la bunge hili ili sisi tukae zimetumika BILIONI 8.2 alafu
leo kwa sababu ya hotuba moja tu ya Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi
wote wamegeuka, wanaharibu kabisa tunashindwa kufanya mambo ya maana,
wanaacha kupanga mkakati wa hoja wanapanga mkakati wa kuzomea,
wameishiwa mikakati mpaka wanazomea kimkakati’
3. ‘Unakutana
na mbunge tena Waziri kama rafiki yangu Mwigulu Nchemba tunataniana
ananiita mzee wa Maandamano mi namuita mzee wa kuteka, ananiambia wewe
Sugu sijui unataka serikali tatu sijui vipi na vipi, namwambia kwani
hutaki kabisa Tanganyika anasema mi nataka Tanganyika ila nataka
serikali moja, sasa kama mnataka serikali moja kwa nini uibuke kwenye
hoja ya serikali mbili?
4. ‘Kuna
watu ambao wanajadili vitu ambavyo hawaviamini na havipo kwenye mioyo
yao na hao watu wanadhamana kwenye uongozi wa taifa hili na hii ni
hatari’
5. ‘Tuko
kwenye nafasi nzuri sana ya kujadili hili swala, tulijadili wakati
tunaheshimiana kuliko siku tuje kulazimisha mabadiliko ambayo
hatukuyapanga, tusifikie sehemu Wazanzibari hao wanaosemwa elfu sitini
ndio waingie barabarani na jeshi’
6. ‘Mwenyekiti
alikuja hapa akatutisha oooh sijui serikali tatu jeshi, Mwanajeshi
atakuja atachukua nchi… Mwenyekiti mwenyewe alikua ni Mwanajeshi akavua
uniform, Nyerere aliposema vueni uniform akavua na leo ni rais, kuna
ubaya gani Mwanajeshi akitawala kama ana akili? hakuna ubaya, wanajeshi
ni ndugu zetu’
7. ‘Hakuna
tatizo lolote siku Mwanajeshi akija kuwa Rais kwa sababu tunae
Mwanajeshi Rais Kikwete na anaendelea tu, asiweke vikwazo kwa Wanajeshi
wengine ambao watakua na tija kwa taifa hili’
8. ‘Wanasema
serikali tatu gharama, hivi kama gharama inaongezeka alafu tija
inaongezeka kuna tatizo gani? ukifanya biashara rejareja ukitaka kuwa
mkubwa ni lazima uongeze mtaji, kama huu mfumo wa serikali mbili
umeshindwa kutuondolea matatizo mwengine anasema Znz wana hiki wana
kile, mbona hamsemi kama mpaka umeme tunawalipia?? lakini sisi huku
tunalia’
9. ‘Tuna
serikali mbili na hakuna aliesimama hapa akasema serikali mbili gharama
zake zipi, Wizara ngapi hapa zinapanga majengo kila siku yanatolewa
furniture? serikali tatu gharama against what? against tija? against
maendeleo? against kwenda mbele?
10.
‘Sababu akili yenu ni fedha ndio maana mnaangalia faida kwamba ni fedha
tu, hamuangalii faida nyingine za kijamii ambazo zitaleta tija kwa
taifa hili’
11. ‘Kuna
hawa ndugu zangu viongozi wa dini, tunasema hivi mara nyingi viongozi
wa dini wamekosea walipochagua kuwa upande wa dola dhidi ya matakwa ya
nchi, hii imetokea mfano ni Padri wa Rwanda, leo hii yukwapi? kwa hiyo
viongozi wa dini wawe makini wanavyoangazia haya maswala’
12. ‘Mungu
ibariki Tanganyika, Mungu ibariki Zanzibar , Mungu bariki mchakato huu
wa shirikisho la Zanzibar na Tanganyika, acheni kutupiga mkwara eti
tutagawana mbao… ni heri kugawana mbao kuliko kwenda kuzinguana huko
mbele ya safari’
CHANZO http://www.babamzazi.com
EmoticonEmoticon