Mbunge
wa Ubungo na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), John Mnyika amuelezea Gwiji la muziki wa Dans
nchini, "Baba ya Muziki", Muhidin Maalim Gurumo aliyefariki dunia juzi
kama "Mbuyu" uliodondoka katika tasnia hiyo.
Mnyika
amesema amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Mwanamuziki huyo
mkongwe ambaye alifariki duni juzi baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Alisema, amekwishawasiliana
na Shirikisho la Wasanii kwa ajili ya kuwasilisha rambirambi zake na kutoa pole
kwa Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania
(Chamudata), kwa kupoteza mshauri na mkuu wake wa Idara ya Fedha.
“Aidha natoa wito kwa
wananchi wa Ubungo na Jiji la Dar es Salaam kwa ujumla, kushiriki katika
kumuaga kesho (leo), nyumbani kwake Mabibo External katika Kata ya Makuburi
kabla ya kwenda kuzikwa kwao Kisarawe Kijiji cha Masaki. Kwa kuwa niko katika
Bunge la Katiba, nitawakilishwa katika kutoa heshima za mwisho na Diwani wa
Kata ya Makuburi alipoishi marehemu,” alisema Mnyika na kuongeza.
Nichukue fursa hii kutoa pole
kwa mashabiki wenzangu wa nyimbo zake kuanzia akiwa Kilimanjaro, Chacha, Rufiji
Jazz, Kilwa Jazz, Sikinde na Msondo Ngoma kuanzia wakati wa Nuta, Juwata mpaka
Ottu".
EmoticonEmoticon