Mshambuliaji nyota wa Simba, Amissi
Tambwe amesema anataka kufunga angalau bao moja katika mechi dhidi ya Yanga,
Jumamosi.
Tambwe amesema kwa kuwa wamekosa
ubingwa na nafasi ya pili, anaamini mashabiki wao watakuwa na furaha kubwa
kuwaona wanashinda mechi hiyo.
“Pia ningependa kufunga bao moja au
zaidi kutokana na mchezo utakavyokuwa.
“Napenda kuwafunga Yanga, lakini
napenda kuona timu yangu ya Simba inashinda mechi hiyo ya watani,” alisema
Tambwe.
Tambwe anaongoza listi ya wafungaji
bora akiwa na idadi ya mabao 19.
Idadi hiyo tayari imevuka ile ya
mfungaji bora msimu uliopita, Kipre Tchetche raia wa Ivory Coast.
Mechi hiyo ya Jumamosi itakuwa ni funga dimba Ligi Kuu Bara huku Yanga ikiwa na uhakika wa kushina nafasi ya pili, wakati watani wao wanagombea kubaki katika nafasi ya nne.
EmoticonEmoticon