KOCHA MKUU wa timu ya JKT
Ruvu, Fred Minziro amesema ushindi walioupata wa bao 1-0
dhidi ya wapinzani wao Coastal Union umetokana na mabadiliko makubwa
aliyoyafanya kwenye kikosi hicho baada ya kumalizika mechi yao na Yanga.
Minziro aliyasema hayo jana mara baada ya
kumalizika kwa mchezo huo ambao ulichezwa kwenye dimba la CCM Mkwakwani kwa
kueleza siri hiyo imechangiwa kwa asilimia kubwa na mabadiliko hayo.
Alisema licha ya kupata ushindi huo bado
wanakwenda kujipanga kuhakikisha wanacheza vizuri mechi yao inayofuata dhidi ya Azam FC lengo likiwa
kupata ushindi ili waweze kusogea katika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi
hiyo.
“Tunajua
tunakwenda kucheza na Azam FC hii ni timu nzuri wala sio ya kubeza hivyo nasi
tutahakikisha tunajipanga vilivyo ili kuweza kupata matokeo mazuri kwani hilo ndio lengo letu kwa
kila mchezo uliopo mbele yetu “Alisema Minziro.
Aidha kocha huyo alisema matokeo
hayo waliyoyapata yamewapa nguvu ya kwenda kujipanga wakiamini watafanya vizuri
kwenye mechi zao zilizobakia ikiwemo wa Azam FC.
Aliongeza kuwa licha ya Azam
watakuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani lakini wao watahakikisha wanafanya kazi kubwa ya
kucheza kwa umakini mkubwa ili kupata matokeo ya aina yoyote yale ili kupata
pointi.
EmoticonEmoticon