NA MWANDISHI WETU,ABUJA.
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan ameapa kuwa nchi
yake itapambana na mauaji na ukatili unaofanywa na wapiganaji wa kundi lenye
itikadi kali za Kiislamu la Boko Haram.
Kauli hiyo ameitoa wakati alipotembelea kituo cha mabasi
cha Nyanya ambacho kimeshambuliwa na kusababisha mauaji ya watu wapatao 71 na
wengine kadhaa kujeruhiwa.
Rais Jonathan amesema wamepoteza maisha ya watu kadhaa
na kwamba suala la Boko Haram linaleta sura mbaya katika historia ya kipindi
cha maendeleo.
Amesema suala la Boko Haram ni la muda tu na kwamba
watalitatua. Msemaji wa Jeshi la Polisi la Nigeria, Frank Mba, amesema
shambulio la leo limeteketeza mabasi makubwa 16 ya abiria na mabasi madogo 24
ya abiria.
Mwaka 2011, Boko Haram walishambulia majengo ya ofisi za Umoja wa
Mataifa mjini Abuja na kusababisha mauaji ya watu 21 na kuwajeruhi wengine 60.
EmoticonEmoticon