Timu
ya Taifa ya Tanzania ya Sola la Ufukweni (Beach Soccer) iliyoingia
kambini mwishoni mwa wiki Bamba Beach Kigamboni, inaendelea na mazoezi
kujiandaa na mchezo dhidi ya timu ya Taifa Soka la Ufukweni ya Misri
mwishoni wiki ijayo.
Maandalizi ya mchezo dhidi ya timu
ya Misri yanaendelea vizuri Bamba Beach Kigamboni chini ya kocha mkuu
John Mwansasu ambaye aliingia kambini mwishoni mwa wiki na wachezaji 14.
Mchezo wa kwanza unatarajiwa
kufanyika Ijumaa ya Machi 13 katika klabu ya Escape 1 Msasani jijini
Dar es salaam na marudio yake kufanyika baada ya wiki moja nchini
Misri.
Tanzania ilifanikiwa kufuzu hatu
ya pili baada ya kuitoa timu ya Taifa ya Kenya kwa jumla ya mabao 12- 9,
mchezo wa awali Mombasa Tanzania ilishinda kwa mabao 5-3, na mchezo wa
marudiano uliofanyika klabu ya Escape 1 kuibuka na ushindi wa mabao 7-6.
Fainali za Mataifa Afrika kwa Sola
la Ufukweni (Beach Soccer) zinatarajiwa kufanyika mwezi April 2015
katika Visiwa vya Shelisheli.
EmoticonEmoticon