Mkuu
wa mkoa wa Tabora akihutubia wakati wa Uzinduzi wa huduma ya Madaktari
bingwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete,huduma ambayo
inaratibiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF ikiwa ni hatua ya
kuwahamasisha wananchi kujiunga na Mfuko huo.
Mjumbe
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF
Bw.Charles Kajege akitoa maelezo kuhusu kuanzishwa kwa huduma hiyo ya
Madaktari bingwa katika mikoa mbalimbali nchini ambayo imelenga kusaidia
kutoa huduma za matibabu kwa watanzania kulingana na mahitaji ya maeneo
husika.
Mkuu
wa mkoa wa Tabora Bw.Ludovick Mwananzila akikabidhi msaada wa shuka
kwa Mganga mkuu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete Dr.Gunini
Kamba,katikati ni Katibu tawala mkoa wa Tabora Bi.Kudra Mwinyimvua.
Mjumbe
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini NHIF
Bw.Charles Kajege akikabidhi msaada wa vifaa tiba vitakavyosaidia zoezi
la utoaji wa huduma za matibabu zitakazotolewa na madaktari bingwa
kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Taasisi ya Moi jijini
Dar-es-Salaam.
Madaktari
bingwa ambao watatoa huduma za matibabu bure kwa wananchi katika
hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete kwa muda wa siku saba.
Baadhi
ya wananchi wakipanga hospitali ya rufaa Kitete wakisubiri kuonana na
madaktari bingwa kwa ajili ya kupatiwa uchunguzi na matibabu.
Mganga
mkuu wa mkoa wa Tabora Dr.Gunini Kamba akijaribu kuteta na viongozi wa
ngazi ya juu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambapo katikati ni Mjumbe
wa bodi ya Wakurugenzi wa NHIF Bw.Charles Kajege,na kulia ni Kaimu
Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini Bw.Athuman Rehan.