UMOJA WA WATU WA MWANGA WAFANYA MKUTANO MKUU NA KUFANA TANGA

March 02, 2015
JAMII imetakiwa kuwa na mshikamano katika kujiletea maendeleo  na kuacha mifarakano isiyo na tija jambo ambalo linaweza kurejesha nyuma nguvu kazi katika kujileta kipato

Akizungumza katika mkutano mkuu wa mwaka, Umoja wa Wanamwanga (Uwamwa) waishio Tanga jana,  mgeni rasmi katika mkutano huo, Simba Msuya, alisema vikundi vya umoja ni jambo muhimu na lenye kuleta maendeleo.

Alisema umoja ndani ya taasisi na jamii za watu ziko na msaada mkubwa katika kuharakisha maendeleo yakiwemo ya elimu na vituo vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

“Fursa ya kuwa mgeni rasmi katika mkutano huu wa mwaka wa umoja wa wanamwanga ni jambo la kufurahisha na kuweza kutoa neno ambalo linaweza kuwa msaada kwa wengine” alisema Msuya na kuongeza

“Mimi niwaombeni katika umoja wenu huu pia iwe msaada kule mutokako kwa kusaidia shughuli za maendeleo kama upungufu wa vyumba vya madarasa na madawati” alisema

Alisema imekuwa ada kwa baadhi ya watu wanaounda umoja  kuacha kuchangia huduma za maendeleo katika maeneo yao na hivyo kusema kuwa huko hakutoweza kuleta maana ya umoja wao.

Akizungumza katika mkutano huo, Makamo Mwenyekiti wa Umoja huo, Yahya Mruma, alisema wanachama wake wamekuwa wakishiriki katika kazi za maendeleo zikiwemo za ujenzi wa maabara.

Alisema wamekuwa wakishiriki kikamilifu ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali na nguvu za wananchi katika ujenzi wa taifa na kuhakikisha malengo ya Serikali yanatimia.

“Mbali na kazi za umoja wetu lakini pia tumekuwa tukishiriki katika kazi za maendeleo kama ujenzi wa maabara kwa baadhi ya shule hapa Tanga na kule Mwanga” alisema Mruma

Amevitaka vikundi vyengine vinavyounda umoja kutumia fursa wanazozipata kusaidia jamii na kushiriki katika kazi mbalimbali za maendeleo ili kurahisisha huduma maeneo yao.


 Mlezi wa Umoja wa Wanamwanga (Uwamwa) waishio Tanga, akizungumza katika mkutano mkuu wa umoja huo uliofanyika ukumbi wa Tanga hoteli jana.
 Mwanachama wa umoja wa Wanamwanga (Uwamwa) waisho Tanga , Geofrey Msuya, akitoa ushauri wa jambo katika mkutano mkuu wa mwaka wa umoja huo uliofanyika jana Tanga.


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »