Mkuu wa Mkoa wa Kinondoni, Paul
Makonda akisaini kitabu cha wageni katika shule ya sekondari Turian
iliyopo katika wilaya ya Kinondoni wakati wa ziara yake ya kutembelea
miradi ya Maabara katika sekondari za Wilaya yake. Aliyesimama nyuma
yake ni Mkuu wa shule ya sekondari Turiani Mwalimu Betrice Mhando. PICHA
ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
Mkuu wa shule ya sekondari
Turiani Mwalimu Betrice Mhando akitoa maelezo machache juu ya shule yake
mbele ya Mkuu wa Wilaya aliyeongozana na viongozi mbali mbali wa
Wilaya.
Mkurugenzi wa Manispaa ya
Kinondoni, Eng. Mussa Natty akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni, Paul Makonda (wa kwanza kushoto) ambapo alisema miradi ya
ujenzi wa maabara katika shule za sekondari katika wilaya hiyo
itagharimu zaidi ya sh. bilioni 2. na kuwa ujenzi wake unasimamiwa na
waataalamu waliobobea katika shughuli hiyo.
FUPA uliomshinda Waziri wa
zamani wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna
Tibaijuka kuhusu migogoro ya ardhi iliyokithiri katika Manispaa ya
Kinondoni Mkuu mpya wa wilaya hiyo Paul Makonda ameahidi kuutafuna.
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo
Mussa Natty alisema miradi hiyo yote ya ujenzi wa maabara katika shule
za sekondari katika wilaya hiyo itagharimu zaidi ya sh. bilioni 2. na
kuwa ujenzi wake unasimamiwa na waataalamu waliobobea katika shughuli
hiyo.
Mkurugenzi wa Manispaa ya
Kinondoni, Eng. Mussa Natty aakimuonyesha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni
Paul Makonda jinsi maabara hiyo ilivyojengwa kwa ubora wa hali ya juu.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (wa kwanza kushoto) akiongea na baadhi ya madiwani wa Wilaya.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Manzese mara baada ya kumkaribisha shuleni kwake,
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akiweka saini ya kumbukumbu mara baada ya kuwasili.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Eng. Mussa Natty akiendelea kuelezea ujenzi wa maabara.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,
Paul Makonda akishuka kutoka kukagua maabara ya ghorofa inayojengwa
katika shule ya sekondari Manzese.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari
ya Manzese akitoa maelezo machache kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul
Makonda (wa kwanza kushoto) mara baada ya kuingia katika maabara
inayotumiwa kwa sasa.
Mara baada ya kumaliza ziara
yake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (wa kwanza kushoto)
alifanya majumuisho ya ziara, Ambapo ametoa onyo kwa wale wote
waliojenga katika maeneo hayo kuanza kuondoka mara moja kabla
hawajafikiwa.
“Moto ninaokuja nao katika suala
ili hautazimika nitasimamia mimi mwenyewe kwa kushirikiana na polisi
ubomoaji wa majengo yote ambayo yamejengwa katika maeneo ya wazi na yale
yaliyotengwa kwa ajili ya shule” alisema Makonda.
Makonda alitoa maagizo hayo katika ziara ya siku moja ya kukagua shughuli za maendeleo katika wilaya yake Dar es Salaam jana.
“Mimi simuogopi mtu nasimamia
utendaji wangu wa kazi kila mtu anajua msimamo wangu wa kusimamia jambo
na katika suala ili hakuna atakaye salimika ” alisema Makonda.
Makonda aliagiza migogoro yote
ya ardhi ambayo ipo hivi sasa ianze kushughulikiwa na watendaji
wanahusika katika manispaa hiyo kuanzia ngazi ya chini na ametenga kila
Ijumaa migogoro ambayo inashindikana ipelekwe ofisini kwake ili
kuzikutanisha pande zote zinazohusika kwa ajili ya kusuruhisha migogoro
hiyo.
Sambamba na agizo hilo Makonga
amewataka wote wa manispaa hiyo kusimamia ujenzi wa maabara kikamilifu
na kuagiza kuwa Aprili mwaka huu miradi yote iwe imekamilika.
“Hatutasubiri mpaka mwezi wa
sita kama alivyo agiza wazirin mkuu kumaliza miradi yote ndani ya
kipindi hicho nawaagiza mkamilishe maabara zote ifikapo mwezi wa nne na
wale wote watakaoshindwa wajipime utendaji wao” alisema Makonda.
EmoticonEmoticon