Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara, Tanzania, Mheshimiwa Janeth
Mbene(kulia), akiongea na Mwakilishi wa Serikali ya Uingereza katika
masuala ya Biashara na Uwekezaji nchini Tanzania, Lord Clive Hollick,
walipokutana kuzungumzia masuala ya Biashara ya kati ya nchi mbili ya
Tanzania na Uingereza na juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya
Uingereza kusaidia wawekezaji wa Kiingereza kuwekeza Tanzania.
Mheshimiwa
Janeth Mbene, akiongeza na Wawekezaji na Wafanyabiashara wa Kiingereza
alipokutana nao kwa mwaliko wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London
na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa East African Association. Mheshimiwa
Naibu Waziri alikutana na Wafanyabiashara hao kwa lengo la kuwashawishi
kuja kuwekeza nchini Tanzania
Mheshimiwa
Waziri Janeth Mbene(kulia), alipokutana na Mwakilishi wa Serikali ya
Uingereza na Chama cha Wafanyabiashara na Wawekezaji wa nchini Uingereza
(UKTI) (kati mwa picha), kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara
cha Tanzania nchini Uingereza, Bwana Yusuf Kashangwa.
Wawakilishi
wa Jumuiya za Wafanyabiashara na Wanachama wa chama cha Wafanyabiashara
wa Tanzania nchini Uingereza (Tanzania Business Group) wakimsikiliza
Naibu Waziri wa Viwanda, Mheshimiwa Janeth Mbene, alipokutana na
kuzungumza nao siku ya Ijumaa tarehe 28 Februari 2015, mkutano
uliofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, London.
Mheshimiwa Waziri alikutana nao kuzungumzia hali ya Siasa na Uchumi na
maendeleo ya nchi kwa ujumla. Mheshimiwa Waziri aliwakumbusha
Wafanyabiashara hao kutumia fursa zilizopo na kuwekeza nyumbani
Tanzania, kwa lengo la kuongeza ajira na kuinua uchumi wa nchi.
Balozi
wa Tanzania nchini Uingereza Mheshimiwa Peter Kallaghe, akiongea
machache kumkaribisha Mheshimiwa Naibu Waziri Janeth Mbene, kwenye Ofisi
za Ubalozi huo zilizopo London. Naibu Waziri Mbene ameondoka usiku wa
jumapili tarehe 1 kurejea Tanzania, alikuwa nchini Uingereza kwa ziara
ya kikazi na kutembelea Vituo vya Kibiashara vya Tanzania na Dubai.
Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Janeth Mbene, akiwa pamoja na
Viongozi wa Jumuiya ya Saccoma, Mhe. Waziri alipokutana Viongozi wa
Jumuiya hiyo ya Saccoma kuangalia jinsi gani inaweza kushirikiana na
Tanzania kuwawezesha Wafanyabiashara wa Tanzania kuleta bidhaa zao
nchini Uingereza kama ilivyo kwa Wafanyabiashara wa nchi nyingine za
Afrika, ambazo bidhaa zao zimejaa nchini Uingereza tofauti na bidhaa za
Tanzania ambazo hazipo. Pichani(kulia) Mheshimiwa Waziri Janeth Mbene,
Mama Perez Ochieng (Saccoma - CEO), Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha
Tanzania, London, Bwana Yusuf Kashangwa, Mwakilishi wa Saccoma na Dada
Magdalena Hall, msaidizi wa Waziri.
Mheshimiwa
Waziri Janeth Mbene(nne kushoto), Naibu Balozi wa Tanzania, Bwana
Msafiri Marwa (tano kushoto),wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya
Wafanyakazi wa Ubalozi, alipokutana nao kwa mazungumzo mafupi kwenye
ofisi za Ubalozi, London.
Mheshimiwa
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene akiwa kwenye Ofisi za
Kituo cha Biashara cha Tanzania, London. Pichani kulia ni Bwana Yusuf
Kashangwa, Mkurugenzi wa Kituo na Dada Magdalena Hall msaidizi wa
Waziri.
Waziri
Janeth Mbene (pili kulia), alipokutana kuzungumza na Wafanyabiashara wa
Tanzania waishio nchini Uingereza na baadhi ya Wawakilishi wa Jumuiya
za Watanzania. Pichani (kushoto), Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini
Uingereza, Peter Kallaghe, Bwana Msafiri Marwa (pili kushoto) na Bwana
Khaki, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kitanzania waishio
nchini Uingereza.
Naibu
Waziri wa Viwanda, Mhe. Janeth Mbene akiongea na Wawekezaji wenye nia
ya kuwekeza Tanzania, alipokutana nao katika Mkutano ambao uliandaliwa
na Chama cha Biashara na Wawekezaji wa Afrika kijulikanacho kama
Business Council for Africa (BCA). Picha zote na Ally Rashid Dilunga