JULIO AITUMIA SALAMU KAGERA SUGAR,ASEMA LAZIMA WATAKAA TU

March 02, 2015
KOCHA MSAIDIZI wa Coastal Union ya Tanga, Jamhuri Kiwelu “Julio”amesema ushindi wa timu hiyo katika mechi ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi yao na Mgambo Shooting imempa nguvu ya kwenda kujipanga vema kuhakikisha timu hiyo inapata ushindi dhidi ya Kagera Sugar.

Julio alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki mara baada ya kumalizika  mechi hiyo ilichezwa jana kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani ambapo ilimalizika kwa Coastal Union kuibuka na ushindi wa bao 1-0,bao hilo likifungwa na Yayo Kato Lutimba baada ya kumalizika kazi nzuri iliyofanywa na Selemani Kibuta.

Alisema ushindi huo umeifungulia milango ya ushindi timu hiyo kwenye mechi zao zilizosalia kwenye michuano hiyo hivyo watafanya maandalizi kabambe ambayo yataiwezesha timu hiyo kutisha kwenye ligi hiyo.

Aidha alisema kuwa dhamira yao ni kuhakikisha timu hiyo inapata ushindi wa kishindo kila mchezo lengo likiwa kuiondoka nafasi iliyopo ili kuweza kusogea kwenye juu kwenye msimamo wa Ligi hiyo kwa kuweka mipango itakayokuwa ikitekelezeka.

    “Nataka kukuambia kuwa safari hii ndio imeanza hivyo tunatoa tahadhari kwa timu tutakazokutana nao kwenye michuano hii kwa sababu tumedhamiria kubadilika na kupata ushindi kwa sababu ya ubora wa kikosi chetu “Alisema Julio.

Hata hivyo ataanza kazi nyengine kuanzia leo mazoezi kwa umakini mkubwa ili kuiwezesha timu hiyo kuendeleza wimbi la ushindi kwenye mechi yao ijayo itakayochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani wikiendi ijayo.

  “Hii ndio kazi tumeianza sasa tunarudi na kufanya kazi kubwa hivyo nataka niwaambie mjitokeze kwenye mechi ijayo dhidi ya Kagera Sugar njoo uone kitakachotokea kwenye mchezo huo “Alisema Kocha huyo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »