Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
wakeze Mama Zakhia Bilal na Mama Asha Bilal, wakitoa heshima zao za
mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu, Kapteni John Komba,
wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika leo Machi 2, 2015
kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Baada ya shughuli hiyo
mwili wa marehemu umesafirishwa kuelekea Kijiji cha Litui Wilayani
Mbinga mkoa wa Ruvuma kwa maziko. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, wakati
walipokutana kwenye Viwanja vya Karimjee baada ya kuhudhuria shughuli za
kuaga mwili wa marehemu Kapteni John Komba leo Machi 2, 2015. Baada ya
shughuli hiyo mwili wa marehemu umesafirishwa kuelekea Jijini cha Litui
Wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma kwa maziko. Picha na OMR
EmoticonEmoticon