Meneja wa Udhibiti na Sayansi wa Vyakula wa Nestle Tanzania, Marsha Macatta-Yambi akizungumza wakati wa mkutano wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyoandaliwa na taasisi ya Soring Women International iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Soring Women International, Luphurise Lema akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani 2018 aliyoandaa jijini Dar es Salaam.
Mtangazaji wa Clouds FM/TV na mchoraji katuni mahiri, Ali Masoud 'Masoud Kipanya' (katikati) akiwa katika moja waendesha mjadala wa nafasi ya mwanamke katika maadhimisho ya siku wanawake Duniani leo jijini Dar es Salaam. Kutoka ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mikocheni, Salama Ndyabura, na Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa Soring Women International, Luphurise Lema (kushoto).
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mikocheni, Salama Ndyabura (katikati) akichangia mada ya nafasi ya mwanamke katika jamii katika maadhimisho ya siku Wanawake Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mchoraji wa Katuni na Mtangazaji wa Clouds Radio/TV, Ali Masoud 'Masoud Kipanya' (kushoto) na Mratibu wa UN Global Compact Network Tanzania, Emmanuel Nnko (kulia) na Dk. Florence Temu kutoka AMREF (wa kwanza kulia).
Mchangiaji wa Shirika la AMREF, Dk. Florence Temu akichangia mada katika siku wanawake duniani.
Mratibu wa UN Global Compact Network Tanzania, Emmanuel Nnko akichangia mada katika siku wanawake duniani.
Waendesha mjadala wa nafasi ya mwanamke wakiwa katika picha ya pamoja.
Meneja wa Udhibiti wa Sayansi wa Vyakula wa Nestle Tanzania, Marsha Macatta - Yambi akitoa shukrani zake kwa wageni waalikwa katika maadhimisho ya siku Wanawake Duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa taasisi ya Soring Women International, Luphurise Lema akitoa shukrani za pekee kwa wadau waliojitokeza kumuunga mkono katika shughuli yake ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Dunia aliyoiandaa jijini Dar es Salaam.
Mwasisi wa Vikoba nchini Tanzania, Devota Likokola akichangia mada.
Akinamama waliohudhuria katika maadhimisho ya siku Wanawake Duniani iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Wanawake wanaweza kuleta mabadiliko ya maendeleo katika jamii ikiwa watasimama imara kwa pamoja na kuwezesha wenzao ambao hawana elimu ya kutosha.
Hayo yamesemwa na mapema leo Machi 10, 2018 na Meneja wa Udhibiti na Sayansi wa Vyakula wa Nestle Tanzania, Marsha Macatta-Yambi wakati akizungumza katika mkutano wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyoandaliwa na taasisi ya Soring Women International iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa wanawake wanaweza kufanya mabadiliko kwa kila mmoja kuwa imara na kuamsha wanawake wengine ambao hawajafikiwa na fursa zikiwemo cha uchumi au za ubunifu za kuweza
Marsha amasema kuwa kuadhimisha siku ya wanawake lazima kulete mabadiliko sio kuadhimisha tu halafu hakuna matokeo chanya yanayoonekana kwa wanawake tutakuwa hatujatenda haki katika kujipambanua ili kuweza kufikia malengo kwa wale wale walioasisi.
Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Soring Women International, Luphurise Lema amesema kuwa wakati alipokuwa anafanya kazi aliona kuwa watu waliosoma nje ya ndio wana akili lakini alitambua kuwa sio hivyo tofauti yake ni kujiamini tu na kuamini kila kinachofanyika hata mwanamke anaweza.
Luphurise amesema kuwa kila mwanamke asimame imara na kuamini kila anachofanya anaweza kuleta mabadiliko hata ya dunia.
Nae mtangazaji wa Clouds FM/TV na mchoraji katuni mahiri Ali Masoud ‘Masoud Kipanya’ ambaye ni mchora katuni na mtangazaji wa Cloud Radio/Tv ja ya Watengeneza mjadala, Ali Masoud ‘Masoud Kipanya’ amesema kuwa wanawake ni watu muhimu na majukumu anayofanya mwanamke akipewa mwanaume hawezi kuyafanya isipokuwa alioanzisha kauli kuwa hawawezi ndio imewafikisha wanawake lakini wakaze buti wanaweza kuleta mabadiliko.