Mke wa
Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete akimpongeza Mbunge wa Vitimaalum mkoa
wa Tabora Munde Tambwe baada ya kupokea kiasi cha shilingi milioni moja
kwaajili ya TIKA huku Mbunge huyo Munde Tambwe akiahidi mbele Mama Salma
Kikwete kuchangia jumla ya mifuko Miambili ya Saruji kwa ajili ya
Ujenzi wa Mabweni katika Shule za Sekondari za kata manispaa ya Tabora
na ujenzi wa uzio Kliniki ya Tabora mjini maarufu Town Clinic.
Mke wa
Rais mstaafu wa awamu ya nne Mama Salma Kikwete akizungumza katika
maadhimisho hayo ambapo alisema kuna haja ya kuleta mabadiliko ya
kisekta yatakayoharakisha maendeleo kwa Wanawake kupitia kujenga misingi
imara ya kupata elimu bora itakayotoa fursa kwa Wanawake kuajiriwa na
hata kujiajiri wenyewe.
Mbunge
wa Vitimaalum mkoa wa Tabora Munde Tambwe akizungumza katika Sherehe za
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake zilizofanyika kimkoa mkoani
Tabora,katika maadhimisho hayo Munde aliwalipia Kadi za matibabu maarufu
TIKA Wanawake wasio na uwezo Miamoja wanaoishi manispaa ya Tabora akiwa
anakamilisha idadi kama hiyo kwa Wanawake wengine mia moja kwa kila
Wilaya za mkoa wa Tabora ambazo ni wilaya saba.
Munde
akikabidhi jumla ya shilingi milioni moja kwa Mke wa Rais mstaafu wa
awamu ya nne Mama Salma Kikwete kwa ajili ya kulipia Kadi hizo miamoja
za matibabu kwa Wanawake wasio na uwezo wa kumudu gharama za matibabu
Manispaa ya Tabora.
Maadhimisho
ya Siku ya wanawake duniani mkoani Tabora ambapo Mama Salma Kikwete
alikuwa mgeni rasmi iliyofanyika viwanja vya Chipukizi mjini Tabora.
Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanry akiungana na Wanawake mkoani Tabora kuadhimisha siku hiyo ya Wanawake duniani
Gwiji
na Msanii mkongwe wa muziki wa Taarabu nchini Malkia Khadija Kopa
akitumbuiza katika maadhimisho hayo mjini Tabora katika viwanja vya
Chipukizi.
Wanawake wajasiliamali wakiadhimisha siku yao wakati muziiki wa taarabu ukitumbuizwa na Malkia Khadija Kopa.