MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA PWANI AMEWATAKA VIJANA WA BAGAMAYO KUTEMBEA KIFUA MBELE NA KUMSEMEA RAIS MAGUFULI KWA MAMBO MENGI ALIYOYAFANYA TANGU KUCHAGULIWA KWAKE KUWA KIONGOZI MKUU WA NCHI KUPITIA CCM.

March 10, 2018
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro akizungumza na wajumbe wa baraza la vijana wa CCM wa Wilaya ya Bagamoyo wakati wa ziara yake leo mkoani Pwani. Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Bagamoyo,Mkwayu Makota na Katibu UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Kapeto. Picha zote na Elisa Shunda
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro akizungumza na wajumbe wa baraza la vijana wa CCM wa Wilaya ya Bagamoyo wakati wa ziara yake leo mkoani Pwani.
Katibu UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Kapeto akifafanua jambo katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Bagamoyo,Mkwayu Makota akizungumza katika mkutano huo.Kushoto ni Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Pwani,Charangwa Seleman Makwiro na Katibu UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Kapeto.
Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Bagamoyo,Mkwayu Makota akizungumza katika mkutano huo.Kushoto ni Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Pwani,Charangwa Seleman Makwiro
Diwani wa Kata ya Msata,Selestin Semiono (katikati) akichangia hoja kuhusu kumuomba Mwenyekiti Charangwa Makwiro kusaidia vijana wapate kazi katika miradi na fursa zinazotokea katika maeneo yao katika mkutano huo. Walio pembeni kwake ni Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Mkoa wa Pwani,Rashid Likunja (Kulia) na Erasto Makala (Kushoto). 
Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Bagamoyo,Mkwayu Makota wakiteta jambo katika mkutano huo.Kushoto ni Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Pwani,Charangwa Seleman Makwiro 
Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Bagamoyo wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Pwani,Charangwa Seleman Makwirowakati alipokuwa akizungumza nao katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro akimkabidhi Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Bagamoyo,Mkwayu Makota (Kulia) kadi za umoja wa vijana 100 kwa ajili ya kusajili wanachama wapya. Anayeshuhudia ni Kulia ni na Katibu UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Kapeto.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro akimkabidhi Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Bagamoyo,Mkwayu Makota (Kulia) vitabu vya kanuni 100 za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya viongozi wa kata za wilaya hiyo kwa ajili ya utendaji kazi wao kwa ufanisi katika kutoa maamuzi. Anayeshuhudia Kulia ni Katibu UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Kapeto.
Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Bagamoyo wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Pwani,Charangwa Seleman Makwirowakati alipokuwa akizungumza nao katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani,Charangwa Selemani Makwiro (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la UVCCM Wilaya ya Bagamoyo leo baada ya kumalizika kwa mkutano wao.


NA ELISA SHUNDA,BAGAMOYO.

WANACHAMA wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wa Wilaya ya Bagamoyo wametakiwa kutembea kifua mbele huku wakijiamini na kuwaelezea vijana wenzao miradi mbalimbali mikubwa inayofanyika hapa nchini chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais,Dk.John Magufuli katika kutimiza malengo ya Tanzania ya Viwanda kwa kujenga barabara za juu (Fly Over),uboreshaji wa miundombinu,mradi wa umeme vijijini (REA),elimu bure shule za msingi na sekondari,ujenzi wa mradi mkubwa wa reli ya kisasa ya Standard Gauge,ununuzi wa ndege za Bombadier pamoja na kutumbua watumishi vyeti feki.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Makwiro wakati akizungumza na vijana wa UVCCM wilayani Bagamoyo leo kwenye muendelezo wa ziara yake ya kutembelea wilaya zote za mkoa wa Pwani ambapo amewashukuru na kuwakumbusha vijana hao kuishi katika ndoto ya Rais Dk.John Magufuli na malengo ya kuifanya nchi kuwa Tanzania ya Viwanda katika hotuba waliyozungumza katika mkutano mkuu wa vijana hao uliofanyika mjini Dodoma hivi karibuni ambapo katika mkutano huo ulimwezesha Kheri James kuwa mwenyekiti wa UVCCM Taifa.

“Nimekuja katika Wilaya hii ya Bagamoyo kwa ajili ya kutoa shukrani zangu kwa ninyi vijana wenzangu kwa kuniamini na kunipigia kura za ndiyo zilizoniwezesha kushinda nafasi hii ya uenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani hivyo basi nitatumia akili zangu,nguvu,uwezo,rasilimali na elimu niliyonayo katika kuhakikisha natatua changamoto za vijana wa mkoa wetu wa Pwani leo kichama naonekana nawawakilisha vijana wa Chama Cha Mapinduzi peke yake lakini ukweli ni kwamba nitakachokipigania mimi kitawaletea faida vijana wote wa mkoa huu hivyo kwa yale nitakayokuwa nayapambania kwa vijana nanyi muwe bega kwa bega mniunge mkono katika kufanikisha changamoto za vijana” Alisema Mwenyekiti Makwiro.

Aidha Mwenyekiti Makwiro amewasisitiza vijana hao kutembea kifua mbele kwa kuisemea serikali ya awamu ya tano iliyopo chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais.Dk.John Magufuli kulingana na miradi mbalimbali mikubwa anayoitekeleza nchini wao kama vijana wa Chama Cha Mapinduzi ambao ndo jeuri ya chama hicho wanapaswa kuzungumza na vijana wenzao kuwakumbusha kila siku mambo mema yanayofanywa na kiongozi huyo ambapo watu wasio na mapenzi mema na taifa hili wanajaribu kupotosha ukweli na kumsema vibaya Rais huyo na wasaidizi wake katika ngazi mbalimbali.

“Vijana ndo nguvu ya chama hivyo kwa kutumia utashi wenu ni vyema sasa vijana wa Bagamoyo na Mkoa wa Pwani kwa ujumla tupambane kumsemea Rais John Magufuli na serikali yake katika mambo mbalimbali ya miradi mikubwa ya nchi waliyoifanya ambapo wanatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) tutumie vyema mitandao ya kijamii ya facebook,Instagram na Twitter katika kujenga hoja;

“Kuna mambo mengi yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano mfano ujenzi wa barabara za juu (Fly Over),uboreshaji wa miundombinu,mradi wa umeme vijijini (REA),elimu bure shule za msingi na sekondari,ujenzi wa mradi mkubwa wa reli ya kisasa ya Standard Gauge pamoja na ununuzi wa ndege za Bombadier pamoja na utumbuaji wa watumishi hewa na wazembe makazini tusemee miradi hii tuachane na watu wasiotaka kusema ukweli juu ya utendaji kazi usio na mashaka wa rais wetu” Alisema Makwiro.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »