MNEC SALIM ASAS BADO ANAUMIZWA NA USHINDI WA MBUNGE MSIGWA WA MWAKA 2015

March 10, 2018
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas  akiwahutubia wajumbe wa baraza kuu la umoja wa wanawake manispaa ya Iringa na kusema kuwa bado anaumizwa na matokeo ya ubunge wa jimbo la Iringa mjini baada ya wapinzani kushinda kwa kishindo mwaka 2015 kwa ni kitendo ambacho hakukitegemea.
Mwenyekiti wa umoja wa wanawake UWT manispaa ya Iringa Ashura jongo akimtoa hofu MNEC Salim Asas juu ya kukomba jimbo baada ya kulipoteza kwa kusalitia mwaka 2015
 Baadhi ya wageni waliokuwa wamealikwa kwenye baraza hilo kwa ajili ya kujifunza na kutoa mapendekezo pale wanapopata nafasi
 Baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi mkoani Iringa walipokuwa wakimsikiliza kwa umakini mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas alipokuwa anatoa ya moyo kuhusu kushindwa katika uchaguzi wa mwaka 2015

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas bado anaumizwa na matokeo ya ubunge wa jimbo la Iringa mjini baada ya wapinzani kushinda kwa kishindo mwaka 2015 kwa ni kitendo ambacho hakukitegemea.

Akizungumza wakati wa baraza la UWT manispaa  ya Iringa Asas alisema kuwa usaliti ulifanywa katika uchaguzi wa mwaka 2015 umekuwa ukimuumiza hadi sasa na kitendo anafikiri kitadumu moyoni mwake hata kwa miaka kumi kwakuwa bado anakumbuka mara kwa mara.

“Naombeni niongee ukweli kitendo kilichofanywa na wanaccm wa manispaa ya Iringa katika uchaguzi wa mwaka 2015 kilikuwa kitendo ambacho ni usaliti mkubwa ambao unaumiza sana kichwa changu” alisema Asas

Asas alisema kuwa uchaguzi huo kulikuwa na wanaccm wengi ambao mchana walikuwa ccm na usikuwa walikuwa kwa wapinzani hivyo lazima tuondoe usaliti kwenye chama bila hivyo tutaendelea kushindwa kila siku.

“Unakuta rasilimali zilizokuwa zinatolewa na  chama cha mapinduzi zote zinatumika kwa wapinzani kuhakikisha wanaiangusha ccm,sasa hicho kitu ndio ambacho kinaniumiza sana kichwa hadi hii leo” alisema Asas

Asas aliutaka umoja wa wanawake (UWT) manispaa ya Iringa kufanya kazi kwa umoja unatakiwa na kuhakikisha kuwa ccm inakuwa ila na isiyo na makundi ili kufika mwaka wa uchaguzi wanashinda kwa kishindo kwa kutumia umoja wao.

“Nawaombe muutunze umoja huu ambao sasa mnao hadi kipindi cha uchaguzi wowote ule ambao upo mbele yetu na kuhakikisha kuwa tunashinda kila chaguzi kwa kishindo kwa kuwa nyie akina mama ndio huwa mnakula ambazo haziamishiki” alisema Asas

Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT manispaa ya Iringa Ashura jongo alimuhakikishia MNEC Salim Asas kuwa kosa lilofanyika mwaka 2015 halitajirudia tena katika chaguzi yoyote ambayo itakuwa inafanyika katika manispaa ya Iringa.

“Ndugu MNEC kwa kweli tumejifunza na tunajutia kitu kilichofanyika mwaka 2015 hivyo tunakuhadi kuwa kwenye umoja wetu wa wanawake Manispaa ya Iringa hakitaa tokea kama kilivyotokea,na tutashinda chaguzi zetu kwa kuwa kila mtu anaumia na kilichotokea mwaka 2015” alisema Jongoo

Jongoo alimshukuru MNEC kwa kurudisha umoja kwa wanaccm mkoa wa Iringa kwa kuwa anafanya kazi kubwa kuhakikisha kila kitu kinakuwa kama kinavyokusudiwa na kuhakikisha umoja ambao umetengenezwa na viongozi wapya unadumu hadi watakapomaliza uchaguzi.

“Mheshimiwa MNEC umoja ambao tunao hivi sasa tunatakiwa kuulinda na kuudumisha hadi kipindi cha chaguzi zote na kuhakikisha kuwa ccm inashinda kwa kushinda na kuendelea kuwa ngoja ya chama hicho kama ilivyokuwa hapo awali” alisema Jongoo

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »