Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina katika picha
akiongea na wataalam wanahabari na viongozi wa Wizara hiyo kutoka katika sekta
ya Uvuvi, baada ya kuonyeshwa zana zilizokamatwa katika oparesheni maalum ya kupambana
na uvuvi haramu, katika kanda ya Dar es Salaam.
Katika picha baadhi ya zana zinazotumika katika uvuvi haramu
zilizokamatwa katika oparesheni maalum ya kupambana na uvuvi haramu katika kanda ya Dar es Salaam.
Kushoto Bw. Obadia Mbogo, Afisa katika sekta ya uvuvi
aliyeshiriki katika oparesheni maalum ya kupambana na uvuvi haramu,
akimuonyesha Waziri Mpina na ujumbe wake aina ya baadhi ya vilipuzi
vilivyokamatwa katika zoezi hilo katika kanda ya Dar Es Salaam.
NA MWANDISHI MAALUM
Akiwa katika zoezi la kupongeza kikosi maalum kilichoanza
oparesheni ya kupambana na uvuvi haramau katika bahari ya hindi leo, zoezi
lililokwenda sambamba na kuonyeshwa vifaa vinavyotumika katika uvuvi haramu
vilivyokamatwa katika zoezi hilo lilioanza mwezi Julai mwaka huu, Waziri
wa mifugo na Uvuvi Mhe. Luahaga Mpana
amezitaka halmashauri ambazo shughuli za
uvuvi zinafanyika kutenga fedha ili kuweza kupambana na uvuvi haramu.
Mpina ambaye ameshangazwa na kitendo cha Halmashauri hizo
kukusanya fedha za ushuru zitokanazo na shughuli na uvuvi na kujisahau kabisa
kuingia katika zoezia la kupambana na uvuvi haramu kwa kutenga fedha hususan za
kufanya doria.
Aidha, Mpina Amewataka viongozi wakuu wa Wizara yake, Katibu
Mkuu Dkt. Yohana Budeba na Kaimu Mkurugenzi wa maeneleo ya Uvuvi Bw.
Magese Bulayi kutembea na barua rasmi katika ziara zao za kikazi kwenye
halmashauri husika zilizokuwa tayari
kuwawajibisha watumishi wazembe katika zoezi zima la kupambana na uvuvi haramu.
“Mkurugenzi wa maendeleo ya uvuvi na katibu Mkuu,nawaagiza
mtembee na barua zilizotayari kusimamisha au kufukuza kazi watumishi wazembe
katika halmashauri, barua hizo zibaki wazi katika sehemu ya kujaza majina yao
tuu, na ndani ya mwaka mmoja nataka tukomeshe kabisa uvuvi haramu. “
Alisisitiza Mpina.
Awali akieleza madhara ya matumizi ya kitoweo cha samaki
waliyovuliwa kwa njia ya vilipuzi na mabomu, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.
Yohana Budeba alisema kuwa samaki wanaovuliwa kwa njia hiyo huleta madhara
makubwa kwa walaji ikiwa ni mapoja na magonjwa ya tumbo na Saratani
EmoticonEmoticon