Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akisalimiana na Makamu wa Rais wa
Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato walipokutana
kwa mazungumzo katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akisalimiana na Mwakilishi Mkazi
Mwandamizi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan –JICA nchini Tanzania
Bw. Toshio Nagase, alioambatana na Makamu wa Rais wa Shirika hilo Bw. Hiroshi
Kato (katikati) walipowasili katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini
Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kushoto) na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la
Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato (wa pili kulia) wakijadili masuala
mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Japan katika Nyanja mbalimbali
ikiwemo miundombinu, nishati, kilimo na maji, walipokutana Jijini Dar es
Salaam.
Makamu wa Rais wa Shirika la
Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato akizungumza kuhusu kuwepo
kwa ushirikiano mzuri kati ya Tanzania na Japan katika suala la Maendeleo alipokutana
na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor
Mpango (Mb), Jijini Dar es Salaam.
Wajumbe walioambatana na Makamu
wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato
wakifuatiia kwa makini majadiliano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo pichani) na mgeni wake ambaye ni Makamu wa
Rais wa JICA Bw. Hiroshi Kato, Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) akisisitiza jambo alipokutana na
kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la
Japan (JICA) Bw. Hiroshi Kato (hayupo pichani) katika Ofisi za Wizara ya Fedha
na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Kodi za Ndani wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Elijah Mwandumbya akizungumzia mabadiliko
ya Sheria ya Kodi yaliyofanywa hivi karibuni ambayo yanalenga kutoa misamaha ya
kodi yenye tija kwa umma wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na
Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw.
Hiroshi Kato (hawapo pichani), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango
Jijini Dar es Salaam.
Kamishina Msaidizi wa Sera wa
Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Shogholo Msangi akielezea kuhusu masuala ya kodi
katika maendeleo ya Taifa katika mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na
Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw.
Hiroshi Kato (hawapo pichani), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango
Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), wa nne kushoto na Makamu wa Rais wa Shirika la
Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA), Bw. Hiroshi Kato (wa tano kushoto)
wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa waandamizi kutoka Wizara ya
Fedha na Mipango na Serikali ya Japan, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na
Mipango Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango)
Benny
Mwaipaja, Dar es Salaam
SHIRIKA
la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) limesema liko tayari kushirikiana na
Serikali kujenga miundombinu ya kisasa ya usafiri, Nishati ya umeme, maji na
usafi wa mazingira katika Makao Makuu ya nchi, Dodoma.
Ahadi
hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Shirika hilo Bw. Hiroshi Kato wakati
alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip
Mpango, Jijini Dar es Salaam.
Bw.
Kato alisema kuwa mradi mwingine wanaotaka kuutekeleza katika mji wa Dodoma ni
udhibiti wa taka ngumu na kwamba wanachosubiri ni Serikali kuainisha maeneo ya
vipaumbele vilivyoko katika mpango mji wa Dodoma.
Aidha
Makamu huyo wa Rais wa JICA alisema kuwa Shirika lake litaendelea kusaidia eneo
la kilimo hususan kilimo cha mpunga ili kuongeza thamani ya zao hilo na
kuwakomboa wakulima.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amelishukuru Shirika hilo kwa kuonesha
nia ya kusaidia ujenzi wa mji wa Dodoma ambao ndio Makao Makuu ya nchi.
Alisema
kuwa mradi huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuupanga mji wa Dodoma mapema ili
kuondoa changamoto za msongamano wa huduma za jamii kwenye eneo moja kama
ilivyo Jijini Dar es Salaam.
“Pamoja
na umuhimu wa miundombinu ya maji, umeme, usafiri wa mjini, lakini pia tunataka
tujenge mapema njia za juu (ring roads) ili kudhibiti msongamano wa magari”
alisema Dkt. Mpango.
Aliongeza
kuwa mradi mwingine wa kipaumbele katika mji huo ni ujenzi wa uwanja wa ndege
wa kimataifa katika eneo la Msalato, karibu kilometa 20 kutoka katikati ya mji
huo ili kurahisisha usafiri kwa njia ya anga.
EmoticonEmoticon