Makamu Mkuu wa Chuo Taalum, Prof. Ganka Nyamsogoro, akizungumza na waandishi wa habari juu ya mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu Morogoro Novemba 30, 2017, Chuo cha Kampasi ya Mbeya Desemba 8 na Chuo cha Kampasi ya Dar es Salaam Desemba 22. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya mahafali hayo, Dk. Mrisho Malipula na katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Mzumbe, Rainfrida Ngatunga.
Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe, Dk. Mrisho Malipula, akitoa ufafanuzi juu ya mahafali hayo.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano Chuo Kikuu Mzumbe, Sylvia Lupembe, akitoa ufafanuzi juu ya mkutano wa Baraza la Masajili ‘Convocation’ utakaofanyika Novemba 29, 2017 Kampasi Kuu Morogoro.
Makamu Mkuu wa Chuo Taalum, Prof. Ganka Nyamsogoro, akizungumza na waandishi wa habari juu ya mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe. Kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Mzumbe, Rainfrida Ngatunga.
Morogoro, Tanzania-Novemba 27
MAHAFALI ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe yanatarajiwa kufanyika kuanzia Novemba 30, 2017, jumla ya wahitimu 3,461 katika mwaka wa masomo 2016/2017 wanatarajiwa kutunukiwa shahada, stashahada na astashahada mbalimbali na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji Mkuu mstaafu, Barnabas samatta, kati ya wahitimu hao ni
*Shahada ya Uzamivu (PhD) ni 4 (0.12%)
*Shahada za Umahiri (Masters) ni 1,005 (29.04%)
*Shahada za Kwanza (Bachelors) ni 2,063 (59.61%)
*Stashahada (Diploma) ni 191 (5.52%)
*Astashahada (Certificate) ni 198 (5.72%).
Kati ya wahitimu wote waliohitimu Kampasi Kuu ni 2,119 (61.23%).
Chuo cha Kampasi cha Chuo Kikuu
Mzumbe Mbeya ni 734 (21.21) na Chuo cha Kampasi cha Chuo Kikuu Mzumbe
Dae es Salaam ni 608 (17.57%).
Mahafali hayo yanatarajiwa
kufanyika Kampasi Kuu Novemba 30, 2017, Chuo cha Kampasi Mbeya Desemba 8
2017 na Chuo cha Kampasi Dar es Salaam Desemba 22 2017.
Mahafali hayo yatatanguliwa na
mkutano wa 17 wa baraza la Masajili Çonvocation’ utakaofanyika Novemba
29 2017 katika ukumbi wa mihadhara wa Fanon, uliopo kampasi Kuu.
Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe kuanzia mwaka 2002 na wahitimu wa Chuo cha
Uongozi wa Maendeleo (IDM) wanakaribishwa kuhudhuria mkutano huo.
Mjadala mahususi na nafasi ya wahitimu na wanachuo katika kuchangia maendeleo ya Chuo Kikuu Mzumbe utafanyika.
Aidha Baraza la Masajili
linaendelea kuwahamasisha wahitimu wote wa Chuo Kikuu Mzumbe na wadau
wengine kuendelea kuchangia kampeni ya ujenzi wa hosteli ya wanachuo wa
kike kupitia ‘Çonvocation Fundraising Account’namba 01o150209448900 iliyopo Benki ya CRDB, Tawi la Mzumbe.
EmoticonEmoticon