Ukarabati katika bwawa la Itagata lililoko halmashauri ya Itigi ukiendela, kukamilika kwa bwawa hilo kutasaidia usambazaji wa maji kwa vijiji jirani pamoja na kuwezesha skimu ya umwagiliaji katika kijiji cha Itagata.
Wataalamu kutoka halmashauri na Mkao wakijadiliana baadhi ya mambo huku wakishuhudia ukarabati wa bwawa la Itagata utakaosaidia kusambaza maji katika vijiji jirani na kuwezesha kilimo cha umwaigiliaji.
Utekelezaji wa miradi
ya maji katika Halmashauri ya Itigi umeonekana kuwa wenye kasi inayoridhisha
licha ya halmashauri hiyo kuanzishwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Kaimu Kaibu Tawala
Mkoa wa Singia Buhacha Baltazari Kichinda ametoa tathmini hiyo wakati wa kikao
na wataalamu wa halmashauri hiyo ambapo wamejadili mikakati ya kuboresha huduma
ya upatikanaji wa maji.
Kichinda amesema
ofisi ya Mkuu wa Mkoa haina wasiwasi kuhusu halmashauri kutekeleza na kusimamia
miradi ya maji huku matarajio yakiwa ni ifikapo Juni 2018, asilimia ya
upatikanaji wa maji ipande kutoka asilimia 34 za sasa hadi kufikia lengo la
mkoa la asilimia 72.
“Mkurugenzi na
Mwenyekiti wa Halmashauri mnaonyesha dhahiri mmejitosa kuwapunguzia wananchi
adha ya kutafuta maji huku wakiacha kwa muda shughuli zao za uzalishaji mali,
nina imani mtafikia asilimia 72 hata kabla ya Juni 2018 kwakuwa fedha mnazo na
pia mnafanya usimamizi wa karibu wa miradi”, amesisitiza Kichinda.
Ameongeza kuwa Mkoa
wa Singida na hata halmashauri ya Itigi haina mito inayotiririsha maji mwaka
mzima hivyo kusababisha uhaba wa upatikanaji wa maji katika kipindi cha
kiangazi huku wananachi wakitegemea mabwawa na visima ambavyo vinatakiwa
kujengwa na serikali.
“Kipidi cha Kiangazi
kwakweli utawahurumia wananchi wanavyosumbuka kutafuta maji, wanatumia muda
mwingi huko na kujikuta wana muda kidogo wa kuzalisha mali, hali hii haipendezi
na nina imani pia viongozi wa Itigi hili haliwapendezi ndio maana mmeweka nia
ya dhati kulitatua ili wananchi wapate muda mwingi wa kuzalisha kwaajili ya
maendeleo ya Mkoa na taifa letu”, amefafanua Kichinda.
Naye Mhandisi wa Maji
Mkoa wa Singida Lydia Joseph amesema endapo halmahauri hiyo itasimamia kwa
umakini na haraka kukamilika kwa miradi ya Itigi mijini, Kitaraka na Aghondi
itasaidia ongezeko la upatikanaji wa maji kwa asilimia 20.
Kwa upande wake
Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya Itigi Evaristo Mgaya amesema halmashauri
hiyo inatekeleza miradi ya maji katika vijiji vya Rungwa, Ipande, Sanjaranda,
Itigi, Kitaraka na Aghondi huku kukiwa na mradi wa visima 16 vya ‘windmill’
katika vijiji 12.
Mgaya ameeleza kuwa
miradi hiyo itakamilika ndani ya kipindi cha mwaka huu wa fedha yaani kabla ya
Juni 2018 hivyo kuongeza upatikanaji wa maji kwa zaidi ya asilimia 72.
Naye Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Itigi Luhende Pius Shija amesema wamewajibika sana kuboresha
upatikanaji wa huduma za maji ambazo ni muhimu katika kukuza uchumi.
Luhende amesema licha
ya kuendelea kutekeleza miradi iliyoko kwenye bajeti pia yeye na wataalamu wa
idara ya maji wameongeza jitihada kwa
kuwasilisha maombi mengine ya kuonezewa fedha za miradi ya maji ambapo
tayari wamekubaliwa hali itayaongeza zaidi upatikanaji wa maji.
EmoticonEmoticon