WANAWAKE TANGA WAVUTIWA NA AMANA BANKI

November 27, 2017
Wanawake wanaojishughulisha na shughuli za ujasiliamali Mkoani Tanga wamesema wamevutiwa na programu ya ukopeshaji  wa vitendea kazi badala ya fedha taslimu unaoendeshwa na benki ya Amana na kudai unaweza kusaidia kuendesha miradi endelevu.

Walitoa maelezo hayo  wakati wa kongamano la jukwaa la wanawake wa Mkoa wa Tanga lililofanyika jijini hapa kwa lengo la kujadili mikakati ya kujiendeleza kiuchumi.

Wakizungumza baada ya mkuu wa idara ya miradi ya bidhaa na usimamizi wa mambo ya sheria wa benki ya Amana,Muhsin Mohamed (Pichani Juu) kuelezea kuwa benki hiyo inatoa mikopo ya vitendea kazi na uwezeshaji wa kuendesha miradi badala yafedha,wanawake hao walisema programu hiyo itaweza
kuwaendeleza kiuchumi.

“Sisi wanawake tunajijua wenyewe,ukinikopesha fedha taslimu nitaingia tama ya kwenda kupeleka kwenye vikoba badala ya kufanyia mradi niliokopea,ndiyo maana wengi wetu tunaishi kwa madeni na kunyang’anywa samani za nyumbani”alisema  Sophia Juma mkazi wa Chuda Jijini hapa.

Walisema kama benki hiyo itaweka mikakati mahsusi kwa ajili ya
wajasiliamali wanawake,wanaamini kuwa itawasaidia kuendesha miradi ya maendeleo bila vikwazo.

Akizungumza katika jukwa hilo,Muhsin alisema benki hiyo inayofuata misingi isiyokubali utoaji wa riba na kwamba inakopesha wafanyabiashara wakubwa wa ngazi ya kati,wadogo na hata vikundi.

“Ukiomba mkopo kwetu tutahitaji mpango wa mradi unaotaka
kuendesha,ukishakidhi vigezo  kama wewe ni uanataka kufuga kuku tunakununulia vifaranga,vyakula na kuliweka banda lako katika mazingira rafiki ya kiufugaji”alisema Muhsin.

Mwenyekiti wa jukwaa hilo,Mariam Shamte aliitaka benki hiyo
itakapofungua tawi lake jijini Tanga kutenga dirisha maalumu la
kuwahudumia wajasiliamali wanawake ambalo litakuwa na jukumu pia la kuwapa elimu ya namna ya kuendesha miradi mbalimbali.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »