MAKAMU WA RAIS AFUNGUA KIKAO CHA KUJADILI CHANGAMOTO ZA MUUNGANO ZINAZOHUSU SEKTA YA FEDHA NA BIASHARA JIJINI DAR ES SALAAM

November 27, 2017
9
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo afungua kikao cha kujadili changamoto za Muungano zinazohusu sekta ya fedha na biashara katika ukumbi wa ofisi ya Makamu wa Rais ,Luthuli jijini Dar es Salaam.
Pix 00
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akielezea masuala mbali mbali ambayo yamejadiliwa na Mawaziri wa Tanzania Bara pamoja Visiwani.
Pix 01
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati)akiongoza kikao cha  Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kushoto ni Waziri wa Nchi Afisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohamed aboud Mohamed na kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba.
Pix 02
Baadhi ya Mawaziri kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia kwa makini kikao hicho ambacho changamoto mbali mbali zinazohusu Muungano zinajadiliwa.
Pix 03
Baadhi ya Mawaziri kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia kwa makini kikao hicho ambacho changamoto mabli mbali zinazohusu Muungano zinajadiliwa.
Picha na Eliphace Marwa – Maelezo

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »