Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akizungumza na
wafanyabiashara wa soko la Matola katika Manispaa ya Sumbawanga katika
ziara yake ya kutembelea masoko na kuongea na wafanyabiashara ili kujua
changamoto zao.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa tatu toka kushoto) akizungumza
na wafanyabiashara wa samaki wa soko la Sabasaba katika Manispaa ya
Sumbawanga katika ziara yake ya kutembelea masoko na kuongea na
wafanyabiashara ili kujua changamoto zao.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (kushoto) akizungumza na
wafanyabiashara wa soko la OTC Kizwite katika Manispaa ya Sumbawanga
katika ziara yake ya kutembelea masoko na kuongea na wafanyabiashara ili
kujua changamoto zao.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akinunua bidhaa alipotembelea Soko
la Soweto, kata ya Chanji Manispaa ya Sumbawanga katika ziara yake ya
kutembelea masoko na kuongea na wafanyabiashara ili kujua changamoto zao
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo alipotembelea Soko la Soweto, kata
ya Chanji Manispaa ya Sumbawanga katika ziara yake ya kutembelea masoko
na kuongea na wafanyabiashara ili kujua changamoto zao.
………..
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ameitaka Manispaa ya Sumbawanga
kuhakikisha wanaboresha mazingira ya masoko yaliyopo kwenye Manispaa
hiyo ili wananchi waweze kupata huduma kwenye maeneo hayo bila ya
kulazimika kufika katikati ya mji kupata huduma hiyo.
Amesema
kuwa wakuu wa idara katika Manispaa hawanabudi kuhakikisha wanashuka
kuwafuata wananchi na wafanyabiashara wa masoko hayo na kusikiliza kero
zao na kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya masoko hayo ikiwemo
majengo, usafi wa mazingira na vyoo.
“Nimeambiwa
changamoto nyingi sana na wafanyabiashara wa soko la sabasaba na
wamekuwa wakifanya biashara zao kwenye mazingira machafu hali ambayo
haizoeleki na haifai kuendelea kuwepo, hivyo manispaa lazima iweke kambi
kusikiliza kero zao na kuzitatua, kwani lipo kwenye uwezo wao,” Mh.
Wangabo alisisitiza.
Aidha,
ameitaka manispaa hiyo kuhakikisha usalama wa biashara za
wafanyabiashara hao unaimarika ili kupunguza malalamiko yao na kuongeza
kuwa atahakikisha malalamiko hayo yanafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo.
Akielezea
changamoto za soko la sabasaba, Mwenyekiti wa soko hilo Feston Mwilema
amesema kuwa changamoto kubwa ya soko hilo ni usalama na kuwa hakuna
kituo cha polisi na wala hawana mgambo wa kulinda soko hilo, na kuomba
kusafisihiwa mazingira kutokana na uchache wa vifaa vya kuzolea uchafu
unaozalishwa katika soko hilo.
“Tumelazimika
kuchimba shimo la muda la kutupia uchafu unaozalishwa na wauza samaki
kutoka na kutokuwepo kwa shimo la kisasa, na tuna kontena moja badala ya
matatu ambalo huzidiwa na soko kukosa uzio ni jambo linalotoa mwanya
kwa vibaka kuendelea na wizi,” Alisema Mwilema.
Mh.
Wangabo alitembelea masoko nane yaliyopo kwenye manispaa ya Sumbawanga
na kubaini kuwa masoko mengi hayatumiki kwa kukosa miundombinu bora na
usimamizi na hatimae wananchi kuanzisha masoko yasiyorasmi na
kuhatarisha usalama wa bidhaa zao na usalama wa vyakula kutokana na
kuvidandaza chini na kuhatarisha usalama wa wanunuzi.
EmoticonEmoticon