Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akionyesha hati mbele ya Waandishi wa
Habari alipokuwa akikagua maendeleo ya Mradi wa Mfumo Unganishi wa
Taarifa za Ardhi(ILMIS) leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi
wa TEHAMA wa Wizara hiyo Bw. Shaban Pazi. Mradi huo utakapo kamilika
unaondoa matumizi ya karatasi katika kuhifadhi taarifa za ardhi badala
yake zitakuwa zianhifadhiwa katika Kompyuta.
Afisa Mipango Miji wa Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Irene Sarwat akimuelezea jambo
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi
(kushoto) alipokuwa akikagua maendeleo ya Mradi wa Mfumo Unganishi wa
Taarifa za Ardhi(ILMIS) leo Jijini Dar es Salaam. Mradi huo utakapo
kamilika unaondoa matumizi ya karatasi katika kuhifadhi taarifa za ardhi
badala yake zitakuwa zianhifadhiwa katika Kompyuta.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (kushoto) akisikiliza maelezo toka
kwa mmoja wa wafanyakazi katika cha Mradi wa Mfumo Unganishi wa Taarifa
za Ardhi(ILMIS) alipokuwa akikagua maendeleo ya mradi huo leo Jijini Dar
es Salaam. Mradi huo utakapo kamilika unaondoa matumizi ya karatasi
katika kuhifadhi taarifa za ardhi badala yake zitakuwa zianhifadhiwa
katika Kompyuta.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (kushoto) akisikiliza maelezo kuhusu
urejeshaji wa ramani unavyofanyika toka kwa mmoja wa wafanyakazi wa
Taasisi inayoratibu uhimarishaji Mradi wa Mfumo Unganishi wa Taarifa za
Ardhi(ILMIS) alipokuwa akikagua maendeleo ya mradi huo leo Jijini Dar
es Salaam. Mradi huo utakapo kamilika unaondoa matumizi ya karatasi
katika kuhifadhi taarifa za ardhi badala yake zitakuwa zianhifadhiwa
katika Kompyuta.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (katikati) akionyesha faili lenye
taarifa za Ardhi ya Kiwanja Kimoja mbele ya Waandishi wa Habari
alipokuwa akikagua maendeleo ya Mradi wa Mfumo Unganishi wa Taarifa za
Ardhi(ILMIS) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Mipango Miji wa
wizara hiyo Bi. Irene Sarwat. Mradi huo utakapo kamilika unaondoa
matumizi ya karatasi katika kuhifadhi taarifa za ardhi badala yake
zitakuwa zianhifadhiwa katika Kompyuta.
Picha na: Frank Shija – MAELEZO
……………
Jonas Kamaleki- MAELEZO
Serikali itaanza kutoa hatimiliki
za viwanja kati ya siku moja na siku saba kwa kutumia mfumo wa
kielektroniki ifikapo Juni 1, 2018.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es
Salaam na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendelo ya Makazi, Mhe. William
Lukuvi wakati wa ziara ya kutembelea ofisi za Mfumo Unganishi wa Taarifa
za Ardhi.
“Tunataka kupunguza urasimu na
kuongeza ufanisi katika kutoa hati kutoka ilivyo sasa ambapo hati
hutolewa kati ya mwezi mmoja hadi miezi mitatu”, alisema Lukuvi.
Ameongeza kuwa mfumo huo utaondoa
udanganyifu katika kutoa hati kwa watu wawili au zaidi katika kiwanja
kimoja na kuondoa migogoro ya viwanja ambayo imekuwa kero kwa wananchi.
Lukuvi amesema Serikali ya Awamu
ya Tano imedhamiria kuondoa utapeli uliokuwa ukifanyika kuhusu ardhi na
ndio maana imeanzisha mfumo huo ambao ameuita muarobaini wa migogoro ya
ardhi.
Aidha, Waziri Lukuvi alisema kuwa
hati ya kisasa itakuwa na ukurasa mmoja badala ya zamani ambayo ilikuwa
na kurasa zaidi ya ishirini.
Kwa mfumo huo, maafisa ardhi
hawatatumia tena karatasi bali watakuwa na kompyuta ambamo taarifa zote
zitahifadhiwa, aliongeza Lukuvi.
Lukuvi amesema kuwa mfumo
utaiwezesha Serikali kuwafahamu wamiliki wote wa viwanja na kuwakumbusha
muda wa kulipia viwanja vyao, hivyo mapato ya Serikali yataongezeka.
Kwa mujibu wa Waziri Lukuvi, Mfumo
huo utatumika kutunza taarifa za ardhi za nchi nzima na hauwezi
kuchezewa na mtu yeyote kwani kutakuwepo na nywila (password) ya
kuingia kwenye mfumo ambayo itatolewa kwa maafisa wachache na hivyo
kupunguza uwezekano wa kutoa hati zaidi ya moja kwa kiwanja kimoja.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na wataalam kutoka Kampuni ya IGN
FI wanatekeleza, uundaji, usambazaji, usimikaji na uendeshajiwa mradi wa
mfumo unganishi wa taarifa za ardhi unaodhaminiwa na Benki ya Dunia.
Dhumuni la mradi huo ni kuimarisha
usalama katika umiliki wa ardhi kwa kuboresha usalama na usahihi katika
manunuzi ya ardhi pamoja na kuanzisha mfumo sahihi na imara wa taarifa
za ardhi.
Mfumo huo utakamilika ifikapo Juni
1 mwakani (2018) na hati ya kwanza ya kielektroniki ndipo itatolewa
rasmi. Na wenye hati za zamani watatakiwa kubadilisha hati zao na kupewa
za kielektroniki.
EmoticonEmoticon