NENO LA DK. MWAKYEMBE LIGI YA WANAWAKE, AFANYA ZIARA ARUSHA
Hafla
ya uzinduzi wa Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake imezinduliwa jana na Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe kwenye
Uwanja wa General Tyre jijini Arusha.
Timu zilizokata utepe zilikuwa ni Alliance Queens ya Mwanza iliyoshinda mabao 2-1 dhidi ya Panama FC ya Iringa.
Katika
uzinduzi huo Waziri Dk. Mwakyembe aliwataka wachezaji wa timu zote
kujituma kwa juhudi zaidi kwa kuwa mpira wa miguu kwa sasa ni ajira
kubwa sana kwa vijana.
“Vijana
wangu natambua mnapenda mpiwa wa miguu, naomba mzingatie vitu vitatu
muhimu - nidhamu, juhudi na kujitunza,” amesema Waziri Dk. Mwakyembe
akiwa na Rais wa TFF Wallace Karia, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Kidao
Wilfred na viongozi wa FA Mkoa wa Arusha.
Mara
baada ya kufanya uzinduzi huo, Waziri akiwa na viongozi hao leo
ametembelea Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kutazama maendeleo ya
marekebisho yanayofanyika kwenye Uwanja huo.
Mbali
na uwanja huo pia waziri alifanya ziara fupi kwenye viwanja
wmbalimbali ikiwa ni pamoja na kiwanja cha FFU kwa Morombo, Arusha
ambapo aliwapongeza kwa ukarabati mzuri wa nyasi za kuchezea.
Katika
ziara nyingine Waziri pamoja na Viongozi wa TFF walitembelea shule ya
Trust St. Patric Sports Academy ambacho ni kutuo cha kukuza michezo na
timu zinazoshiriki ligi hiyo, zimeweka kambi.
WAAMUZI 18 TANZANIA WATAPA BEJI FIFA 2017/18
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu Tanzania (FIFA), limetoa beji kwa Waamuzi 18 katika msimu wa mshindano mwaka 2018.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka FIFA, Waamuzi walioteuliwa kwa upande wa
wanaume ni Mfaume Ali, Elly Sasii, Emmanuel Mwandembwa na mkongwe Israel
Nkongo na kwa upande wa wanawake wamo Jonesia Rukyaa na Florentina
Zablon.
Waamuzi
Wasaidizi walipewa beji hizo (Wanaume) ni Soud Lillah, Mgaza Kunduli,
Mohammed Mkono, Mbaraka Haule, Ferdinand Frank Chacha na Frank Komba na
kwa wanawake Hellen Mduma, Dalila Jaffari, Jeneth Balama na Grace
Wamala.
Waamuzi wa mpira wa miguu unaochezwa ufukweni waliopata beji ni Jackson Steven Msilombo na Geofrey Tumaini Mwamboneko.
EmoticonEmoticon