wanamziki wa bendi ya mjengoni wakiwa wanafanya mambo ndani ya jukwaa la kiwanja cha nyumbani mjengoni Klabu
Rais wa bendi ya mjengono Robert Mukongya (Digital) akiwa anaimba ndani ya jukwaa |
Habari picha na Woinde Shizza,Arusha
Bendi mpya ya mziki wa dance
ijulikanayo kwa jina la Mjengoni classic
band inatarajia kufanya
utambulisho wao rasmi kwa mara
ya kwanza mapema march 16 katika ukumbi wa Triple A klabu house
uliopo ndani ya jiji la Arusha
Akiongea na waandishi wa habari Rais wa bendi hiyo Robert Mukongya (Digital)
alisema kuwa pamoja kuwa bendi hiyo
imekuwa ikitoa burudani katika uwanja wa nyumbani mjengoni Klabu pamoja na
sehemu nyingine mbalimbali lakini walikuwa awajaizindua rasmi hivyo wanatarajia kufanya uzinduzi ramsi
katika siku hiyo ya alyamisi.
Alisema anapend akuwakaribisha wapenzi wote
wa muziki wa dance wazee kwa vijana kuja kuona jinsi bandi hii inavyofanya kazi
na jinsi bandi hii inavyotoa burudani kwa mashabiki wake huku akisisitiza waje
waone staili mbalimbali za mziki zinazochezwa na wanamuziki wa bandi ya mjengoni
Kwa upande wake mkurugenzi wa bandi hiyo John Mdenye alisema kuwa bendi yake
imeimarika na wanamziki wanajiamini na ndio maana wameamua kufanya uzinduzi kwa
mara ya kwanza rasmi ili wakazi wa mkoa wa Arusha waweze kuaidi mziki wa dance wenye viwango.
Alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wakazi wa
jiji la Arusha wenyeji na wageni pamoja na wale wanaotoka katika mikoa ya
jirani kuhuthuria onyesho hilo kwani
bendi yake imejipanga kuwapa burudani ya nguvu ambayo itaacha historia kwani
show ambayo wataifanya amna bendi ingine yeyote imeshawai kufanya kama hiyo.
Alisema kuwa bendi
hiyo imejipanga kuanza kutoa burudani majira ya saa moja usiku adi
majogoo ,yote hiyo ni kuakikisha wapenzi
wa mziki wa dance wanacheza adi pale hamu yao itakapo isha
EmoticonEmoticon