Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Kampuni za Quality Group Limited (QGL), Nicholas Ralph akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam, kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi na juhudi za kuliletea Taifa maendeleo endelevu katika nyanja mbalimbali. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Ralph akielezea jinsi uongozi ulivopanga mikakati ya kuboresha kampuni zilizopo na kuanzisha nyinginezo nchini na nje ya nchi.
Sehemu ya wanahabari wakiwa katika mkutano huo
Suleiman
Msuya
KAMPUNI
ya Quality Group Limited (QGL), imesema inaunga mkono jitihada za Rais John
Magufuli katika mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi na juhudi za kuliletea Taifa
maendeleo endelevu katika nyanja mbalimbali.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za kampuni hiyo Barabara ya
Nyerere, Dar es Salaam leo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa QGL, Nicholas Ralph alisema
katika kuunga mkono vita dhidi ya ufisadi wameanzisha mfumo unaotambua na
kudhibiti uhalifu huo kwenye taasisi (e-Governance).
Alisema
mfumo huo wa utambuzi na udhibiti unapaswa kuwepo katika idara zote za Serikali
kwani una utija ni salama zaidi hasa katika kulekea katika Tanzania ya
maendeleo endelevu.
Ralph
alisema QGL imewekeza katika sekta mbalimbali
kama afya ambapo wanatarajia kujenga vituo 4,000 vya afya nchini kote
pamoja na vioski vya kutoa afya ili kuendana na teknolojia ya sasa na
kurahisisha kila mwananchi anapata huduma bora ya afya.
Alisema
pia wamekubaliana na kampuni kutoka nchini Urusi ili kusambaza vifaa tiba na
kampuni nyingine kutoka Marekani itatoa huduma ya ndege katika huduma ya
dharura.
“Pia
kampuni ya QGL imeingia makubaliano na kampuni kutoka nchini Ireland kujenga na
kuwekea uongozi katika utawala ambapo itasaidia kuongeza teknolojia kwa kampuni
za ndani,” alisema.
Mkurugenzi
huyo alisema kampuni ya QGL imekuwa ikisadia wavuvi katika Kanda ya Ziwa kwa
kuwapatia vitendea kazi na matibabu, kusaidia elimu na pia ilisaidia mapambano
ya ugonjwa wa Ebola.
Alisema
kampuni yao imefanikiwa kuongeza ajira, mafunzo, kukuza uchumi ili kuhakikisha
inaunga mkono mpango wa maendeleo wa
Serikali wa 2025.
Ralph
alisema wamekuwa wakitoa mafunzo kwa viongozi na waajiriwa vijana kupitia
program ya Moreh Derech ambayo imekuwa na mafanikio makubwa.
Aidha,
alisema katika kuhakikisha kuwa wanapanua ushirikiano na taasisi za kimataifa
wamesaini makubaliano na Kampuni ya
Solanika International Tractors Limited ya India ambao watakuwa
wanaingiza matrekta 1,000 kwa mwaka hivyo kuongeza ajira 1,200 ifikapo mwaka
2018.
“Pia
tumesaini barua katika miradi ya madini ambapo tunarajia kuuzungumzia vizuri
pindi hatua zote zikiwa zimekamilika,” alisema.
Halikadhalika
alisema wamewekeza katika viwanda vya sukari na maziwa ambapo wananchi wengi wa
Kitanzania ndio watafaidika kwa kuuza bidhaa husika katika viwanda hivyo vyenye
teknolojia ya kisasa na uongozi kutoka Israel, Ulaya na Afrika Kusini.
Ralph
alisema QGL imekuwepo kwa zaidi ya miaka 30 ambapo inashirikiana na kampuni
kubwa duniani kama General Motors (GM), Honda, Isuzu, Bridgestone na Chevrolet.
Alisema
kutokana na ushirikiano huo QGL imeajiri zaidi ya watu 667,300 na kupata faida
ya dola za Marekani bilioni 348.6 hayo yakichangiwa na uwajibikaji, uwazi,
uaminifu na mafanikio.
Alisema
mikakati yao ni kuhakikisha kuwa wanakuwa ni sehemu sahihi ya kuchochea
maendeleo ya nchi na wananchi wa Tanzania.
EmoticonEmoticon