JIJI LA TANGA LATAKIWA KUBORESHA SOKO LA MACHINJIONI LA SAHARE

March 15, 2017
HALMASHAURI ya Jiji la Tanga imetakiwa kuboresha miundombinu ya soko la Machinjioni la Sahare lililopo Kata ya Mnyanjani ili liwezekuendana na hadhi ya Jiji kutokana baadhi ya maeneo kuharabika ikiwemo eneo la kushushia ngombe kwa ajili ya kuchinjwa.

Hali hiyo inasababisha wakati mwengine ng’ombe wanaopelekwa kwenye machinjio hayo kukimbia wakati wakishushwa na hivyo kusababisha hatari kwa wakazi wa maeneo jirani hivyo kuomba wajengewe fensi kwenye eneo hilo ili kudhibiti.

Hayo yalibainishwa juzi na Katibu wa chama cha Wachinjaji wa Ngombe Jijini Tanga, Hassani Mohamed wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea machinjio hayo ili kuweza kutambua changamoto zinazowakabili ambapo alisema tatizo kubwa ni machinjio hayo kukosa uzio.

Alisema licha ya kuwepo kwa suala hilo lakini hata eneo ambalo
limekuwa likishushiwa ng’ombe limekuwa bovu kwa muda mrefu bila kutengenezwa jambo ambalo linapelekea eneo hili kuwa na kikwazo wakati wa ushushaji wa mifugo hiyo.

“Kitendo cha kukosekan uzio kwenye machinjio hii ya Sahare Jijini Tanga kinasababisha athari nyingi ikiwemo wakati mwengine ng’ombe wanaofikishwa kwa ajili ya kuchinjwa kukumbia na kusababisha usumbufu mkubwa kwa jamii ya wakazi wa maeneo ya karibu”Alisema

Licha ya hivyo lakini aliitaka kuona namna ya kuboresha mazingira kwenye machinjio hayo ikiwemo katika sehemu za mitaro ya kupitishia maji ambayo itakuwa ikiyapeleka moja kwa moja kwenye bahari ya hindi.

Aidha pia alisema sanjari na hilo lakini halmashauri hiyo iweze
kuangalia namna ya kuimarisha barabara ya kuelekea kwenye machinjio hayo kutoka kwenye barabara inayoelekea eneo la Sahare ili kurahisisha upitikaji wake nyakati zote bila kuwepo na usumbufu.

“Kwani eneo ambalo limekuwa ni barabara ya kuingilia kwenye machinjio haya limekuwa bovu sana hasa nyakati za mvua magari mengine yanashindwa kuingia hivyo tunaiomba Halmashauri iweze kuona namna ya kulikarabati eneo hili “Alisema.

“Sababu kubwa ya kuomba tungewe uzio kwenye machijio haya ni kuepukana na adha ya kuacha kufanya kazi kila siku na kuanza kukimbizana kusaka ng’ombe ambao wanakuwa wamekimbia kwenye eneo letu hasa wale wakali “Alisema.

Hata hivyo alisema kwenye machinjio hayo katika kipindi cha sikukuu wamekuwa wakichinja ng’ombe kati ya 150 mpaka 200 kwa siku huku kwenye kipindi cha kawaida huchinja kuanzia 60 hadi 100.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »